Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Naona sasa umeamua kuwa FREEMASON
 
Huyu ndugu yetu anataka kuhalilisha maisha yake ya dhambi ( Uzinzi, wizi, uongo na ulafi)😀
 
Huyu ndugu yetu anataka kuhalilisha maisha yake ya dhambi ( Uzinzi, wizi, uongo na ulafi)😀
Sasa hayo maisha mbona watu wnayaishi licha ya kwamba wanaamin kabisa Mungu yupo na mambo hayo ni dhambi kwa mujib wa imani zao..ila hawapotez muda kushawish wengine wasiamin Mungu yupo.Cha msing jamaa yy aishi tu anavyotaka wala sio kesi cz for whatever anybod do, they will be accounted for responsibility regarding the same..whether it is good or bad..whether there is God or Not!!!
 
Mkuu Mungu yupo ila binadamu ndo wanavuruga mambo.

Mungu anahitaji medium/chombo ili kujidhihirisha, tatizo vyombo vingi ni vichafu kama sio vyote, nazungumzia wanaojiita watumishi wa Mungu.

Hata Mimi kuna wakati nawaza huenda hakuna Mungu lakini badae nasema Mungu yupo lakini hafanyi kazi na kwakujiuliza maswali kama yako...

Bado akili inanirudisha kuamini mediums ni chafu...
 
Mimi ninakupa pole kwa Hilo,lakini kaa Chini na utafakari upya.
 
watu wanaendelea kujitambua, safi sana
 
Kitu cha ajabu yule ambae anasali saana unakuta anayo roho mbaya tu wala hawezi kukusaidia (sio wote lakini), na yule ambae hana time na Mungu au anasali lakini sio kivileee anakua na roho nzuri.
Dini sio kigezo cha watu kua wema au wabaya cha muhimu katika maisha ni kutenda mema tu kwa nafasi yako, kuepuka makuu na kwasaidia wahitaji.

Nimeona watoto Wa wachungaji wengi wakiwa na matendo mabaya tu pia nimeona watu wasiokua na Mungu wakifanya mambo makubwa tu ya maendeleo na wakiwa na matendo mazuri tu.

MUHIMU
bora uamini Mungu yupo ukifika mbinguni ukimkuta fresh tu kuliko kutokuamini alafu ufike umkute katulia aisee believe me utapigwa fire unaambiwa ujazo wake ni Mara 1000 ya moto Wa duniani just imagine, na moto wake hauzimiki yani daily ni maumivu tu dadeki...........
 
Muungu YUPO. Na uthibitisho UPO, ila sio unaoutaka wewe. Upeo wa Mungu ni wa juu sana, kuliko unavyoweza fikiria. Binafsi, BIBILIA inanisaidia kupata fununu ya Upeo huo kwa imani (naamiini ndio moja ya malengo yake).

Tuanze hapo, nitajitihidi kujushirikisha uthibitisho wa uwepo wa Mungu kadri nitakapo weza, kama utahitaji.
 
Umechelewa Sana kutambua Hilo mkuu,
Kwanza hongera kwa kujitambua
Pili nakazia
Mungu ni propaganda za zama za Giza
(Dark ages)
Kuamuni Kwamba Kuna Mungu muweza wa yote na muumbaji wa mbingu na ardhi ni Uwendawazimu
Ambao hata unishawishi Kwa kutumia maneno Gani siwezi kuukubali
Mungu,shetani,malaika,mizimu,majini &co ni fiction characters walobuniwa kama
Marvel movies walivyobuni nchi ya Wakanda na Azgard na kiuhalisia hakuna kitu kama hicho!
 
maneno meengi jombi Thibitisha kama huyo Mungu wenu yupo acha kutuaminisha kitu ambacho hata Wewe huna uthibitisho Bali hisia zako tu zinakuongoza uamini kipo,
Unapomthibitisha huyo Mungu hatutaki utuletee Quotes za kitabu Cha hekaya za kiyahudi kiyunani na kiarabu Ili kutuaminisha Lete ushahidi proved wa huyo Mungu sio hearsay!
 
Duuuh hatari sana hii,kila mtu na uelewa wake na anavyoamini
 
Hakuna anae weza kuthibitisha juu ya uwepo wake
ila kwangu mimi ninaishi kwa furaha zaidi kutokana na Imani ya uwepo wa Mungu kwani hata nikipitia magumu naamini yupo na iko siku atanisaidia, inaongeza kiwango changu cha uvumilivu na kuniepusha kwenda kupora mali ya mtu.

Imani ya uwepo wa Mungu inanifanya nifanye ibada na ibada inanikataza na maovu, inanifundisha kuwahurumia binadam wenzangu,kuamini kuwa Mungu yupo inanifanya nisikate tamaa, na kufanya mambo mengine mengi

Kuamini Mungu yupo inanipa faida nyingi sana, Licha ya kua kwa Sasa dini zimegeuzwa biashara lakin maandiko kuhusu Mungu yamefundisha ni jinsi gani ya kutoa sadaka, maana sadaka siyo lazima kuipeleka msikitini au kanisani, unaweza ukamlisha mwenye njaa, kumvalisha asie na nguo, kuwasomesha mayatima na zote zikawa sadaka na ikawa ni njia ya kutenda wema..

Hata kama siwezi kuthibisha uwepo wake lakin mafundisho juu yake yamejaa wema hivyo sion hasara kuamini juu ya uwepo wake.
 
Akili ya Mungu ipo juu sana.Kujaribu kumfikiria Mungu kwa akili iliyokata tamaa,ni sawa na mtoto mchanga kumfikiria baba kama mtu katili kwa vile hamnyonyeshi maziwa.

Mungu akurehemu sana,huenda ukakutana naye kwa urahisi kuliko sisi wengine ambao hatujafuta biblia kwenye simu zetu.Kwani sifa kuu ya Mungu ni Mungu mwenye REHEMA.
 
Ipinge hoja yake kwa hoja yenye nguvu zaidi badala ya kumshambulia. Maisha ya dhambi uliyoyaandika hapa yanafanywa na watu wenye dini na wanaomtaja Mungu kila dakika.
Soma andiko lake kwa umakini.Anadi kuwa mpaka leo hakuna aliyethibitishwa uwepo wa Mungu.Amefanya tafiti na kaona watu wote tangu babu zake ni wajinga kwa kuamini kuwa kuna uwepo wa Mungu. Kwa vile Mungu anapinga uzinzi, ulawiti , umalaya , uzandiki na uonevu yeye kaamua kuachana na haya matakwa ya Mungu ili aponde maisha kwa uhuru zaidi.
Hongera kwake
 
Dadeki
Nje ya maandiko hawezi kukuthibitishia uwepo wa Mungu.
Hata afanye nini, hawezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…