Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Nimefuta Biblia kwenye simu yangu

Bora uamini yupo af ukifika usimkute..Kuliko kuamini hayupo mara paap!! Yule paleee sijui itakuaje??
Hata ukiamini Mungu yupo mbona haikuzuii kufanya mambo yoyote unayotaka!???
Binadam aliyekamilika anapaswa kuishi kwa ustaarab flan na utaratibu hata kama haamini Mungu.

Haya sasa umeamua kutoamin, inakusaidia nini??au inakuongezea nini ambacho hukua na fursa kuki parsue...Ulipokua ukiamin, ni kitu gan ulikua unapungukiwa??

Una unaishi kwa kukariri??
Kuna maelfu ya miungu

Unaposema ni bora uamini yupo, una maanisha Mungu gani?
 
Utadhibitishaje kitu ambacho hakipo kua hakipo Arif?
Halafu unaamini Ili vitu viwepo lazima kuwe na kitu kiwe kimetengeza haya nikuulize nani aliyemtengeneza aliyetengeneza vitu?
Kwanza kuna tofauti ya kusema tu kuwa kitu fulani hakipo na hicho kitu kuwa kweli hakipo, mimi nipo zangu Tz naweza kusema tu rais Kagame hayupo ikulu huko nchini Rwanda, sasa kasema kwangu hivyo ndio utakubali tu kuwa ni kweli Ikulu ya Rwanda hayupo Kagame kwa sababu haiwezekani kuthibitisha kisichokuwepo?
 
Mkuu Mungu yupo ila binadamu ndo wanavuruga mambo.

Mungu anahitaji medium/chombo ili kujidhihirisha, tatizo vyombo vingi ni vichafu kama sio vyote, nazungumzia wanaojiita watumishi wa Mungu.

Hata Mimi kuna wakati nawaza huenda hakuna Mungu lakini badae nasema Mungu yupo lakini hafanyi kazi na kwakujiuliza maswali kama yako...

Bado akili inanirudisha kuamini mediums ni chafu...
Hiyo ni imani ambayo haikutofautishi na imani zingine ambazo hukubaliani nazo
 
Kwanza kuna tofauti ya kusema tu kuwa kitu fulani hakipo na hicho kitu kuwa kweli hakipo, mimi nipo zangu Tz naweza kusema tu rais Kagame hayupo ikulu huko nchini Rwanda, sasa kasema kwangu hivyo ndio utakubali tu kuwa ni kweli Ikulu ya Rwanda hayupo Kagame kwa sababu haiwezekani kuthibitisha kisichokuwepo?
Huo mfano wako upo nje ya maada hapa habari za kagame zinaingiaje kamanda,kagame tunajua yupo Kigali Rwanda na ni kitu real huyo Mungu yupo wapi acha kujumba jumba Lete uthibitisho tukamwone kamanda!
 
Dunia hii ilitekelekezwa baada ya binadamu kujifanya mjuaji.

Hayo uliyoyasema kuhusu wanadamu kuhangaika ni sehemu ya wao kupambana kuokoa jahazi.

Mungu yupo sema Inategemea na ufahamu wako tuu.

Pia hajihusishi na wanadamu baada ya wao kumuasi na kujifanya wajuaji.
Tufahamishe kwa ufahamu wako umejuaje yupo?
 
Soma andiko lake kwa umakini.Anadi kuwa mpaka leo hakuna aliyethibitishwa uwepo wa Mungu.Amefanya tafiti na kaona watu wote tangu babu zake ni wajinga kwa kuamini kuwa kuna uwepo wa Mungu. Kwa vile Mungu anapinga uzinzi, ulawiti , umalaya , uzandiki na uonevu yeye kaamua kuachana na haya matakwa ya Mungu ili aponde maisha kwa uhuru zaidi.
Hongera kwake
Akili zako kama za mjingamimi tu.
 
hahahahah hii Kali Sasa Yale Yale ya Atake asitake tutamuongezea miaka Magufuli tutamlazimisha
unataka uyaaply hapa kwenye vitu seriously au sio?
😁😁😁
Sijakulazimisha hapo naona hujaelewa, nimezungumzia hiyo tabia ya kuuliza nani kamuumba Mungu pale linapozungumziwa suala la Mungu kuwa ndio muumbaji na ndio kaumba huu ulimwengu, ndio hapo nimesema kwamba hata kama hatumjui huyo aliyemuumba huyu Mungu ila hoja ya msingi ni uumbaji wa Mungu hilo ndio la kujadili kama ni kweli au si kweli.
 
Hakuna anae weza kuthibitisha juu ya uwepo wake
ila kwangu mimi ninaishi kwa furaha zaidi kutokana na Imani ya uwepo wa Mungu kwani hata nikipitia magumu naamini yupo na iko siku atanisaidia, inaongeza kiwango changu cha uvumilivu na kuniepusha kwenda kupora mali ya mtu.

Imani ya uwepo wa Mungu inanifanya nifanye ibada na ibada inanikataza na maovu, inanifundisha kuwahurumia binadam wenzangu,kuamini kuwa Mungu yupo inanifanya nisikate tamaa, na kufanya mambo mengine mengi

Kuamini Mungu yupo inanipa faida nyingi sana, Licha ya kua kwa Sasa dini zimegeuzwa biashara lakin maandiko kuhusu Mungu yamefundisha ni jinsi gani ya kutoa sadaka, maana sadaka siyo lazima kuipeleka msikitini au kanisani, unaweza ukamlisha mwenye njaa, kumvalisha asie na nguo, kuwasomesha mayatima na zote zikawa sadaka na ikawa ni njia ya kutenda wema..

Hata kama siwezi kuthibisha uwepo wake lakin mafundisho juu yake yamejaa wema hivyo sion hasara kuamini juu ya uwepo wake.
Kwako uwepo wa Mungu ni faida kwasababu inakupatia tumaini la kinafki

Pale ambapo mambo yako yameenda vibaya na hutaki kuikubali hali hiyo basi ndio unatumia dhana ya mungu kama comfort kua yeye ndio kapanga si ndio?

Hakuna sababu nyingine shawishi yenye kufanya ukubali Mungu yupo zaidi ya hiyo?
 
Kumekucha...kumekuuuuuucha. mkianza issue za Mungu hayupo mi nakuwaga mpole tu. Nawaomba kwenye huu muadhara mjadili bila jazba
 
Utadhibitishaje kitu ambacho hakipo kua hakipo Arif?
Halafu unaamini Ili vitu viwepo lazima kuwe na kitu kiwe kimetengeza haya nikuulize nani aliyemtengeneza aliyetengeneza vitu?
Sisi tumeamua kwenda kwa imani kuwa kuna Mungu na yy ndo chanzo na me I should WA yote

Ww ambaye huamin katika hilo ndo utueleze sasa tumefikafikaje hapa
 
Huo mfano wako upo nje ya maada hapa habari za kagame zinaingiaje kamanda,kagame tunajua yupo Kigali Rwanda na ni kitu real huyo Mungu yupo wapi acha kujumba jumba Lete uthibitisho tukamwone kamanda!
Unaweza kuthibitisha kuwa kweli Kagame bado yupo na yupo Rwanda?

Narudia tena kuna tofauti ya kusema tu kitu fulani hakipo na uhalisi wa hicho kitu hakipo.
 
Kwako uwepo wa Mungu ni faida kwasababu inakupatia tumaini la kinafki

Pale ambapo mambo yako yameenda vibaya na hutaki kuikubali hali hiyo basi ndio unatumia dhana ya mungu kama comfort kua yeye ndio kapanga si ndio?

Hakuna sababu nyingine shawishi yenye kufanya ukubali Mungu yupo zaidi ya hiyo?
Asante

Pia uwepo wa Mungu hauna athari hasi kwa maisha ya mwanadamu.Sijaona faida ya upagani.Dini huwafanya wanadamu waishi kwa pamoja kwa amani kwa kusaidiana.Upagani shabaha yake ni watu wasiishi kama jumuiya.Katika maisha ya mwanadamu hakuna kitu chema kama kuishi katika jumuiya.

Uliza wapagani huwa wanakutana kujadili kutokuwepo mungu na kushirikiana kijamii? Utaambiwa sisi hatuna makanisa ila huwa tunakutana mitandaoni kumpinga Mungu🙂

Kwa uelewa wangu mdogo ni bora ya FREEMASON kuliko upagani.Yaani upagani ni TAKATAKA
 
Back
Top Bottom