Uchaguzi 2020 Nimegundua hizi kampeni zinafanyika kwa upendeleo “hazina usawa”

Uchaguzi 2020 Nimegundua hizi kampeni zinafanyika kwa upendeleo “hazina usawa”

Utakuwa unaishi sayari nyingine,
Taja nchi moja tu inayosema ikishafika wakati uchaguzi rais aliyeko madarakani anaacha madaraka hayo! Hakuna kabisa. Ila rais alyeko madarakani akishindwa wakati wa uchaguzi, basi anasimamia uapishwaji wa aliyemshindwa na kumkabidhi nchi halafu yeye anajiondokea kurudi mtaani kwake.
 
Katika kampeni zinazoendelea, nimeona zinakibeba chama cha mapinduzi kwa sehemu kubwa, kwani viongozi wanaogombea bado wanako madarakani na wamekuwa wakiendelea kutoa maagizo kwa mamlaka zilizo chini yao,

Mfano: Unakuta mgombea urais anatoa maagizo ya kujenga barabara na pia kutoa pesa hadharani kama zawadi, Makamu wake akiagiza halmashauri kuongeza pesa za mikopo kwa vikundi mbalimbali, huku Waziri mkuu akiagiza kurejeshwa kwa baadhi ya mashamba huko Singida.

Hivi hao wapinzani wakitoa misaada wakati huu wa kampeni si watachukuliwa wanatoa rushwa?

Natamani katiba ibadilike tu, kikifika kipindi cha kampeni kila aliyekuwa na madaraka avuliwe ili waingie uwanjani wakiwa katika kiwango kimoja tofauti na sasa.
Kumbe majibu unayo halafu unajitoa akili, maagizo wanayatoa kwa vile bado wapo madarakani. Hao wapinzani watatoa misaada gani wakati wao wenyewe wanaomba kusaidiwa?
 
Pia na haya
IMG-20200916-WA0012.jpg
 
Ina maana haujaona wapinzani wakiomba michango toka kwa wananchi waliotoka kuwaita masikini muda mfupi uliopita. Huoni kama huo nao ni ujambazi wa kisiasa?
Sasa kuomba kunakuwaje ujambazi duu kweli lumumba mmepoteana 😄😄😄
 
mh. Lissu tume haitakutangaza wala polisi hawatakulinda Ninakuomba kwa dhati kabisa kama hakuna mkakati wowote wa lazima kuhusiana na ujinga huo wa tume tafadhali acha kutuchosha wapiga kura maana yasijekutokea kama ya lowasa zee tulilipigia kura nyingi likashinda lkn likadhulumiwa ushindi kizembe
 
Taja nchi moja tu inayosema ikishafika wakati uchaguzi rais aliyeko madarakani anaacha madaraka hayo! Hakuna kabisa. Ila rais alyeko madarakani akishindwa wakati wa uchaguzi, basi anasimamia uapishwaji wa aliyemshindwa na kumkabidhi nchi halafu yeye anajiondokea kurudi mtaani kwake.
Yap ni kweli, I am wrong nilifikiri argument yako ipo kwamba unatakiwa kutoka madarakani ktk kipindi hicho.
Mimi nimekujibu vibaya , sorry
 
Taja nchi moja tu inayosema ikishafika wakati uchaguzi rais aliyeko madarakani anaacha madaraka hayo! Hakuna kabisa. Ila rais alyeko madarakani akishindwa wakati wa uchaguzi, basi anasimamia uapishwaji wa aliyemshindwa na kumkabidhi nchi halafu yeye anajiondokea kurudi mtaani kwake.
Yes.Vurugu.nyingi.ni.za kugomea kukabidhi.madaraka baada. ya matokeo kutangazwa na kushindwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ina maana haujaona wapinzani wakiomba michango toka kwa wananchi waliotoka kuwaita masikini muda mfupi uliopita. Huoni kama huo nao ni ujambazi wa kisiasa?

Wewe unaweza kuwa ni maskini wa kufikiri.
 
Naona unalalamika tu bila kuja na alternative,

Jambo hili lipo dunia nzima Rais anabakia kuwa madarakani na ni mgombea.

Hivyo atumie rasilimali za nchi kwa manufaaya chama chake?
Kama kuna miradi alishindwa kuitekeleza, anakuja kutoamaagizo ya kuitekeleza kwenye kampeni si sawa kabisa
 
Pale tume kuna yule sijui mjita au mkurya anaitwa mahela, yaani ushabiki wake kwa ccm haufichwi kamwe.Leo katishia kumsimamisha lissu kwenye kupiga kampeni kisa eti katishia kuvunja amani, wakati magu kanda ya ziwa katwanga kilugha mwanzo mwisho kinyume cha maadili ya tume. Tume wako kimya tu

Labda kama yule kamanda wa A=B=C, yeye huyu anakazia A=B=C=D?
 
Back
Top Bottom