Nimegundua ni hatari kuhifadhi pesa benki ukiwa unafanya biashara Tanzania

Sina ushahidi wa hili lakini nadhani lina ukweli asilimia 99. Kama mambo yako yako straight hata kama hao jamaa wanataka kukuonea watakosa pa kuanzia. Mtu hata akikutafuta kisa huwa anaangalia penye weakness ndipo anapokuzolea. So am sure hao jamaa kuna jinsi mapato yao hawaeleweki kabisa. Ila huwa hakuna mkosaji anayekubali kosa😀😀
 
Huu uhuni unapaswa kukemewa vikali mno, kinachosikitisha wanafunga Hadi account zisizohusika na biashara husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ndio ulikuwa wakati wa kupaza sauti kwa umoja wetu. Tatizo tuaangalia vitu kichama sana. Tazama Diamond wengine walivyotekwa na Makonda yeye akaimba kukaa kimya. Leo yamemfika
Kufunga account ni upuuzi
 
Nunua assets kama ardhi n.k au nenda kahifadhi uswisi kama wanasiasa wanavyofanya.
Hizo ardhi zenyewe hukawii kuambiwa ni hifadhi ya barabara au kumepita bomba la kinyesi hivyo ni mali ya serikali.

Huko Uswiss rate ya kumaintain account ukute ndio akiba yako yote ya maisha.

Kwa kifupi ni kumuomba Mungu yasikukute tu maana nchi hii kila mtu analia kivyake. Maskini analia kwa ugumu wa maisha na tajiri analia kwa kutaka kufilisiwa na serikali.

Nahisi kipaumbele cha serikali hii japo hawajakiweka wazi ni kuwa kila mwananchi awe fukara. Utajiri uwe wa wachache tu waliojichagua.
 
Ahsante kuanzia sasa naweka fedha zangu zote kwenye kibubu.

Hao TRA wakachukue fedha za Baba zao waliowaajiri.
 
Hapo dawa ni kuwa na akaunti nyingine ambayo haijulikani kwenye biashara zako na wala haina jina lako
 
Sio kwa wafanyabiashara tu, hata kwa wafanyakazi na waajiriwa, ukizinguana na mwajiri wako tu boss anakwenda ku bloki akaunti yako. Hatari!!!
 
Ndiyo maana nchi haiendelei. Mtu kuwekeza nje ya nchi na serikali wala haina habari na wewe ni hatari
 
Pointtless kabisa!
Kama kuna changamoto ya kodi, mteja aitwe ahojiwe, ikishindikana mahakama ya kodi ipo. Siyo mtu mmoja anaamua kublock account yako!
Sasa nimeelewa kwa nini waarabu hawapeleki pesa Bank
 
Ila tuongee ukweli, walichofanya kitaligharimu sana taifa, maana watu wataanza kuondoaha pesa zao bank kwa kasi, na wengine watazihamishia nje ya mchi pesa zao, tena baada ya kuzibadilisha kuwa dollar, madharavyake ni kama yafuatayo

1.) Benki nyingi kufa

2. Mzunguko wa pesa kupungua mtaani

3.) Pesa yetu kushuka thamani

4.) Ajira na uwekezaji kupungua

5.) Mdororo wa uchumi
 
Hela inatakiwa izungushwe sio ichimbiwe Uswiss
Rule number one katika uwekezaji, Never lose money, yaani hutakiwi kupoteza pesa. Ni Mara Mia uichimbie sehemu salama kuliko kuiacha, iliwe na binadamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…