Nimegundua ni hatari kuhifadhi pesa benki ukiwa unafanya biashara Tanzania

Nimegundua ni hatari kuhifadhi pesa benki ukiwa unafanya biashara Tanzania

Sheria inasemaje kuhusu mhalifu? Huyo feitoto ana hela nyingi kuliko Diamond?
Kutolipa kodi ni kosa kisheria. Kwanini asikamatwe akajibu mashitaka mahakamani?
Mbona yule mama wa vitenge alipelekwa mahakamani?
Walifuata taratibu zote za kisheria na wakatuma barua ya wito lkn huyo pimbi akaona haitoshi akaleta hoja kwenye mitandao ya kijamii..
D02ECC9B-BDD1-436B-8EE3-36D554C29924.jpeg
 
Nchi za kiafrika viongozi ndiyo sheria. Hata kama una kosa ndiyo wafunge account yako bila kukamata?
Ukifanya kosa unakamatwa, unapelekwa mahakamani kujibu mashitaka ndiyo sheria inavyofanya kazi siyo unafunguwa hujui kosa. Kisa wameona pesa mingi na kuhisi hisi.
Ina maanisha serikali haitaki watu wawe na hela
Hivi ingelikua ni wewe ndio mhusika wa maswala ya ukusanyaji wa kodi utoaji wa taarifa juu ya ulipwaji wa kodi ungelifanyeje juu ya mbadhilifu wa sheria za ulipaji kodi kama huyu..
47E504FC-11F6-4028-9A51-00F6C2675F70.jpeg
 
Walifuata taratibu zote za kisheria na wakatuma barua ya wito lkn huyo pimbi akaona haitoshi akaleta hoja kwenye mitandao ya kijamii..View attachment 2466791
Mbona hapo hawajaonesha kama walishamtumia barua hapo kabla akagoma?
Barua inaonesha baada ya Diamond kulalamika mtandaoni ndiyo wamemtumia barua.
Soma aya ya mwisho wa barua
 
Hivi ingelikua ni wewe ndio mhusika wa maswala ya ukusanyaji wa kodi utoaji wa taarifa juu ya ulipwaji wa kodi ungelifanyeje juu ya mbadhilifu wa sheria za ulipaji kodi kama huyu..View attachment 2466792
Mimi ningefanya hivi.
1. Nafanya uchunguzi wa kina nikashabaini ana kosa
2. Natuma polisi wanaenda kumkamata
3. Anapandishwa mahakamani kujibu mashitaka siyo tuhuma. Huwezi kumkamata mtu ukimtuhumu halafu hauna ushahidi wa uhakika.
Ndiyo sheria ilivyo. Usipolipa kodi umeenda kinyume na sheria na hapo umekuwa mhalifu. Je, wamefanya hivyo?
Tangu lini mhalifu akawa na mapatano mpk anatumiwa barua?
Mbona yule mama wa vitenge hawakumtumia barua ila walimpandisha mahakamani?
 
Haya mambo ni mageni hapa Tanzania ila huko mbele ni kawaida sana.

With time tutazoea.
Ndio watu hawajazoea na mamlaka zilikuwa hazifuatilii hiki kitu.
Ni kwamba kwenye benki kama una pesa ambazo hazina maelezo yaliyonyooka au kodi hujalipia inavyopaswa account yako itablokiwa mpaka watakapojiridhisha mambo yote ni safi.
 
Wafanyabiashara wengi, wakubwa, wa kati kwa wadogo huu mwisho wa mwaka wamekutwa na dhahama la kusikitisha na kuhuzunisha, wamefungiwa account binafsi za benki na zile za biashara na mamlaka moja yenye nguvu.

Kwenye mazingira kama haya ambapo unaporwa hela zako zote, kuna haja gani ya kuweka pesa benki?

Waswahili wanasema tunajifunza kutokana na makosa. Makosa ya walioporwa pesa zao zilizopo benki tanatufundisha nini?

Weka pesa bank, at your own risk
Pesa zako zifukie kwenye mtungi, kisha utazipta salam kwa mchwa 😀😀
 
Ulishaambiwa: Mayai yote kapu moja? Man karibu una bugi...

Kaa kwa kutulia mwisho wa mwaka fagio linapita kila Bank ukikutwa hueleweki eleweki unapigwa komeo
 
As long as unafanya biashara pasipo kona kona sasa wasiwasi wa nini...Kwa kati ya hao umesikia Bakhresa,Mo Dewji, au hata wamiliki wa biashara za mashule na hotels wanalalamika kuzuiliwa pesa zao bank..Hao wanaolalamika ni wapumbavu kwenye industry business na ni watakatishaji wa pesa haramu, Hakika huwezi kuwa Mfanyabiashara mzuri katika nchi yako na mlipaji wa kodi kwa wakati halafu ukasumbuliwa na mambo kama hayo, Mara nyingi huwa serikali yako itakulinda kwa hali yeyote ile kwani tayari umeshakua ni faida kwao...Achana na wapumbavu wachache wasikufanye ukapoteza ufikiri wako kwa upuuzi wao..
Unakumbuka sakata la sukari ya MO awamu ya 5? Unakumbukuka sakata la Maziwa fresh ta Bakharesa awamu ya 5?
 
Unakumbuka sakata la sukari ya MO awamu ya 5? Unakumbukuka sakata la Maziwa fresh ta Bakharesa awamu ya 5?
Ndugu yangu Mpinzire yaliopita si ndwele, Tugange yajayo...

Angalizo:
Kuna tofauti kubwa sana kati ya hayo matukio uliorodhesha hapo na hili linaoendelea kwa sasa, Ukiniambie nikufafanulie nitakuona unajambo unalitafuta au unataka tuendelee kupiga soga hapa kwenye huu uzi wa ndugu Bujibuji Simba Nyamaume labda yeye pia anaweza akawa na jambo la kuongeza juu ya hili..
 
Back
Top Bottom