Village-in
JF-Expert Member
- Aug 30, 2022
- 2,184
- 4,517
Hii mamlaka toka walivyoonja nyama ya mtu kwenye utawala uliopita hawataki kuacha. Wanazama kwenye akaunt hata bila sababu. Walipumzika hapo katikati baada ya Bank kulia na huo mtindo,naona wameanza tena. Wamenogewa. Wakikufungia inaingia kukubariana nao.Wafanyabiashara wengi, wakubwa, wa kati kwa wadogo huu mwisho wa mwaka wamekutwa na dhahama la kusikitisha na kuhuzunisha, wamefungiwa account binafsi za benki na zile za biashara na mamlaka moja yenye nguvu.
Kwenye mazingira kama haya ambapo unaporwa hela zako zote, kuna haja gani ya kuweka pesa benki?
Waswahili wanasema tunajifunza kutokana na makosa. Makosa ya walioporwa pesa zao zilizopo benki tanatufundisha nini?
Weka pesa bank, at your own risk
Kwa kweli haina haja ya kuweka hela bank.