Nimegundua ni hatari kuhifadhi pesa benki ukiwa unafanya biashara Tanzania

Hii mamlaka toka walivyoonja nyama ya mtu kwenye utawala uliopita hawataki kuacha. Wanazama kwenye akaunt hata bila sababu. Walipumzika hapo katikati baada ya Bank kulia na huo mtindo,naona wameanza tena. Wamenogewa. Wakikufungia inaingia kukubariana nao.
Kwa kweli haina haja ya kuweka hela bank.
 
Diamond "Kama Mimi muwekezaji wa ndani nimefanyiwa hivi, vipi kwa mgeni "?
 
Huu mtindo ulishikia kasi enzi za Jiwe.
 
Hapo dawa ni kuwa na akaunti nyingine ambayo haijulikani kwenye biashara zako na wala haina jina lako
Unafunguaje akaunti ya aina hiyo kwa kipindi hiki ambapo karibia kila kitu kinataka namba ya nida?
 
Hatari sana
 
Utaalamu wa kukusanya kodi bado uko chini Sana, wakubali kuwatumia wataalamu wa Deloitte au KPMG au PWC wawashauri na kuwajengea uwezo wa kukusanya kodi kwa ufasaha
 
Tatizo wenye nguvu kwa sasa miguru ni ana tamaa ya hatari. Mama aliwapiga stop kuingia kwenye akaunt ya mtu,lakini naona wamerudi kwa kasi,hata wakikuta milioni 30 wanaitamani. Na mama kalala usingizi
 
Sio kwa wafanyabiashara tu, hata kwa wafanyakazi na waajiriwa, ukizinguana na mwajiri wako tu boss anakwenda ku bloki akaunti yako. Hatari!!!
Kivipi? Haki za mteja ni zipi? Je mteja hana haki ya usiri na usalama wa fedha zake?
 
Diamond "Kama Mimi muwekezaji wa ndani nimefanyiwa hivi, vipi kwa mgeni "?
Alipewa barua ya wito huyu kapuku lkn akaona mitandao ya kijamii ndio kimbilio na kupost ushenzi..Ila elimu muhimu sana hata kama una pesa nyingi pasipo elimu utabaki kuwa zumbukuku..
 
Mkuu upo kwenye industry ya biashara?
 
Alipewa barua ya wito huyu kapuku lkn akaona mitandao ya kijamii ndio kimbilio na kupost ushenzi..Ila elimu muhimu sana hata kama una pesa nyingi pasipo elimu utabaki kuwa zumbukuku..
Sikujua! Maana nimesikia anasema angeitwa angeenda Mara moja! Lakini pia washauri wake wa masuala ya kodi wanafeli wapi?
 
Point taken
 
lamBrianLeeSnr umeongea ukweli kwanini uogope kama upo safi? Kweli mbona kina Mo,Bakresa, au Fei toto ,Manula hawalalamiki ,ni sababu inaonekana wanalipa kodi.sasa dogo kabanwa naona anakimbilia mitandao ili apate huruma mara ooh sijui wapinzani sasa upizania gani hapo? Juzi kapiga shoo tiketi m7,m5, na m3 unategemea kama ulisema mapato yako ni kidogo na hutaki lipa watu wakufanyanye? aliminywa mesi sembuse yeye. Lipa kodi uone kama hao jamaa watashughulika na wewe.Eti mimi nataka jiachia wanaifanyia wasafi hivi sasa kama hutaki lipa kodi unategemea nani alipe.
 
Sina ushahidi wa hili lakini nadhani lina ukweli asilimia 99. Kama mambo yako yako straight hata kama hao jamaa wanataka kukuonea watakosa pa kuanzia...
Nchi za kiafrika viongozi ndiyo sheria.

Hata kama una kosa ndiyo wafunge account yako bila kukamata?

Ukifanya kosa unakamatwa, unapelekwa mahakamani kujibu mashitaka ndiyo sheria inavyofanya kazi siyo unafunguwa hujui kosa.

Kisa wameona pesa mingi na kuhisi hisi.

Ina maanisha serikali haitaki watu wawe na hela
 
lamBrianLeeSnr umeongea ukweli kwanini uogope kama upo safi? Kweli mbona kina Mo,Bakresa, au.. .
Sheria inasemaje kuhusu mhalifu? Huyo feitoto ana hela nyingi kuliko Diamond?

Kutolipa kodi ni kosa kisheria. Kwanini asikamatwe akajibu mashitaka mahakamani?

Mbona yule mama wa vitenge alipelekwa mahakamani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…