Nimegundua Watanzania wengi ni wapole kwa Sababu ya umaskini, ujinga na maradhi

Kama kawaida yako,simple facts na kufanya generalization
 
"Njaa inadhalilisha heshima na uhuru wa nchi, njaa inatweza utu wa binadamu".Bashiru

Watanzania tuna njaa ya kimwili, kiakili na kiroho.
 
Nafika kwenye hiyo nchi ila nakuta kila mtu analaumu watanzania ,najiuliza je waliopo ni raia wa nchi gani 🤔

Kwenye Filamu Mawazo yako tunaweza kuiita Tanzania kama nchi ya kusadikika ambayo watu wanaoishi humo kila Mmoja anawashutumu wa Tanzania kama watu wajinga, malofa na wasiojielewa.

Kwenye Katuni, inaweza leta tafsiri mbaya zaidi
 
Kwenye Filamu Mawazo yako tunaweza kuiita Tanzania kama nchi ya kusadikika ambayo watu wanaoishi humo kila Mmoja anawashutumu wa Tanzania kama watu wajinga, malofa na wasiojielewa.

Kwenye Katuni, inaweza leta tafsiri mbaya zaidi
Na ndio hiyo tafsiri ambayo mimi naifikiria kwamba watanzania hata hatujielewi kuwa sisi ni wajinga 😁
 
Kiini kikubwa cha hali hii ya “upole wa Watanzania” ni mfumo wa elimu na matumizi ya ujinga wetu kisiasa. Watanzania wengi siyo wapole kwa asili, bali ni watu waliokata tamaa, waliodhoofishwa kiakili na kiuchumi. Elimu yetu haijengi fikra huru, bali inatufundisha kutii. Hii ni hatari sana kwa taifa. Mfumo huu wa kutengeneza raia wapole na watiifu umetumiwa na CCM kwa miaka mingi ili kuendeleza utawala wake bila upinzani wa maana. Natambua mchango wa CCM katika historia, lakini kwa sasa wamepoteza dira ya dunia ya kisasa.

Tatizo kubwa la CCM sasa ni woga. Woga wa kupoteza madaraka umezaa propaganda isiyokidhi mahitaji ya kizazi cha sasa. Badala ya kufikiri mbele, wamebaki kwenye mfumo wa zamani wa kuongoza kwa vitisho na porojo. Wanapoteza uhalali wa kisiasa, lakini kwa sababu wanajua Watanzania wengi ni maskini na wajinga, wanatumia udhaifu huo kama silaha. Wameanzisha mfumo wa kutoa ‘reward’ kwa watu wachache waliobobea kwenye kupindisha mifumo,wachuuzi wa akili za watu kama machawa, influencers wa kipropaganda, na baadhi ya viongozi wa kidini na mastaa.


Ni kwamba CCM imemaster sana balance ya kudhibiti matarajio ya wananchi kwa kutoa ahadi na propaganda zisizoisha. Lakini sasa kizazi cha leo kimebadilika, kinatazama dunia kwa mtandao. Tatizo ni kwamba, watu maskini huconsume content nyingi, na kwa kuwa hawana elimu ya kuchuja, wanageuzwa kuwa followers wa uongo. Upo mfumo wa kihaini wa kuwafanya Watanzania waendelee kuwa wanyonge kupitia makundi ya “influencers” wanaowarubuni kwa stori, siasa za kihisia, na ndoto za uongo.


Watanzania wengi wanajifanya wapole, wanaongea kwa sauti ya chini, wanajidai watiifu, lakini ukweli ni kwamba wanaumezwa ndani kwa ndani. Ukali wao umenyamazishwa kwa njaa, na upole wao siyo utulivu bali ni kukosa namna. Kuna chuki nyingi zilizojificha mtaani, kuna hasira za kimya, kuna vilio visivyosikika. Taifa likiwa na watu kama hawa, linakua na watu wa kuogopa. Si kwa sababu ni hatari, bali kwa sababu hawajui wapi waelekee wakiamua kulipuka.

Kama tunataka Tanzania yenye utu, haki, na nguvu ya kweli, lazima tufumue mfumo wa elimu na propaganda. Lazima tuache kuongozwa kwa hofu na porojo. Kila Mtanzania aelewe thamani yake,bila kujali elimu wala uwezo wa kifedha. Maana Uhuru wa kweli hauanzi na kura, unaanza na akili iliyo huru kufikiri.
 

Kuna kitu zaidi ya CCM watu wengi hawakioni.

Unajua CCM haipo Kenya, Burundi, Zambia, na nchi zingine za Afrika
 
Kuna kitu zaidi ya CCM watu wengi hawakioni.

Unajua CCM haipo Kenya, Burundi, Zambia, na nchi zingine za Afrika
Hicho kimekuzwa na CCM angalia mfumo wetu wa Elimu. Kila mtu anajua ukivo mbovu na madhara yake na pia Kila mtu mwenye nafasi flani hivi ataongea tu lakini hakuna mwenye guts wa kuubadilisha sababu utaharibu vitu vingi in long term. Hivi unajua mwanangu CCM target Yao ni kua chama Cha milele?
 
Taikon,kuna haja upigwe muda mrefu hadi uchakae na kuchoka.Nimecheka sana.Karibu upate hata dengelua mkuu..
 

Siyo rahisi kuzijua haki zako mkuu endapo unaandaliwa kuwa roboti la serikali na wanafalsafa!
Unajua kwanini somo la history limekuwa ni option katika shule zetu?
Serikali inataka kuzalisha watenda kazi wengi wasio na uwezo wa kuhoji mambo!miaka ijayo wanaharakati watapungua sana katika nchi yetu!

Nchi ina maajabu hii mkuu,kama huniamin tembelea shule ya kata ya sekondari halafu chagua wanafunzi 30 wa kidato cha tatu au nne kisha wape hesabu hii 6788÷3=?
Watakaopata hesabu hiyo bila msaada wa calculator wakizidi nusu hiyo shule ni nzurii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…