Nimeguswa na wale wananchi waliookoa watu ajali ya ndege

Huu nao ni Upumbavu. Kwa hiyo ukipata ajali Barabarani karibu na waendesha Bodaboba wasikusaidie mpaka kikosi cha uokoji cha Serikali kije??
Kwa akili yako ndogo ajali ya boda boda unaona inalingana na ajali ya meli kuonga mwamba..
 
Ajali zinapotokea zinataka utulivu na subra kidogo ili uokozi ufanyike pasi na kuleta madhara zaidi..papara na haraka haraka mara nyingi zinaongeza madhara.
Ajali inahitaji Subira kidogo? Ipi hasa? Umegongana ba Fuso uso kwa uso subira gani inasubiriwa?
 
Aisee Una matatizo Mkuu, Yaani ajali itokee watu washindwe kuokoa wasubiri dk 20 wataalam waje? Are you serious? Hivi unajua changamoto ya miundombinu tuliyonayo?

Sidhani Kama ulishawah kupata ajali hapa Bongo.
 
Ndio maana nikasema cha kwanza ni kusubiri hata dk 20 basi ili polisi wafike kwenye tukio maana hata wao ni wataalam na wana nyezo muhimu kuharakisha zoezi la kuanza uokozi kufanyika, lakini hata tu wakiona ajali ilivyotokea wana ufahamu kuelekeza uokozi wa awali ufanyike vipi..watu wawe na kusubiri kidogo kuliko kuanza uokozi wanavyojua wao wenyewe kwa sababu tu wako kwenye tukio.
 
Kwa akili yako ndogo ajali ya boda boda unaona inalingana na ajali ya meli kuonga mwamba..
Kwa akili yako kubwa kifo cha Binadamu kitokanacho na Meli kugonga mwamba ni zaidi ya Kile cha Mwendesha Baiskeli kugongwa na Boda?,
 
Aisee Una matatizo Mkuu, Yaani ajali itokee watu washindwe kuokoa wasubiri dk 20 wataalam waje? Are you serious? Hivi unajua changamoto ya miundombinu tuliyonayo?

Sidhani Kama ulishawah kupata ajali hapa Bongo.
Ujinga unakusumbua wewe..hujui kitu chochote, bongo bongo..nonsense kabisa.
 
..kwenye nchi za wenzetu ikitokea ajali ndani ya dakika 10 gari ya wagonjwa, zimamoto, na polisi wanakuwa wameshafika. Na kama kuna majeruhi walio na hali mbaya helikopta inaletwa kuwawahisha hospitali.

..Kwanini hatuwekezi kwenye vyombo vyetu vya uokoaji? Masuala ya usalama wa nchi ni pamoja na utayari wa vyombo vyetu kufanya shughuli za uokoaji kunapotokea ajali.

Cc Nguruvi3
 
Una uhakika gani hao Polisi watakuja baada ya hizo dk 20?. Kwamba kuna ajali halafu mnakaa kusubiri Watu ambao huna uhakika nao. Huu ni ujuha.
 
Uko kinadharia zaidi.
 
Hakuna muda wa kusubiri, walipaswa kufika ndani ya muda mfupi. Hivi wewe ukiwa ndani ya ndege halafu unaona wavuvi wamesimama wanasubiri Polisi ungejisikiaje! Fikiria unahitaji dk 3 za Oksijeni halafu unasubiri Polisi wakusanyane kwanza. Hapana! dharura ina maana moja kikosi kiwe tayari na muda unaotakiwa ni kufika eneo.

Kwa mazingira ya Bukoba kikosi kingalikuwa bandarini isingechukua dakika 10 kufika katika ajali.

By the way kuna akari Polisi na Wanajeshi walisimama pembeni, je ulitaka wavuvi nao wakunje mikono!

Hapana, hili ni uzembe wa kutokuwa tayari na majanga! hatuwekezi kunakohitajika tupo bize kununua V8

Tunawalaumu wavuvi kwa lipi? waliotakiwa kufika hawakuwepo!
 
Jeshi la uokozi lilikuwa linamalizia weekend kwa Beer bariid na nyama choma
 
W
Kwa akili yako kubwa kifo cha Binadamu kitokanacho na Meli kugonga mwamba ni zaidi ya Kile cha Mwendesha Baiskeli kugongwa na Boda?,
Kwa akili yako kubwa kifo cha Binadamu kitokanacho na Meli kugonga mwamba ni zaidi ya Kile cha Mwendesha Baiskeli kugongwa na Boda?,
Kifo ni kifo, wewe ndio utofautishe wapi na kwenye mazingira gani unaweza kutoa msaada wakti ajali inatokea..ndio sabab ya kukupa mfano wa ajali ya boda na meli, si kila ajali unaweza kutoa msaada hata kama uko tayari kufa ukisaidia majeruhi.
 
Hii ndio point! nashangaa eti kuna mtu anasema ''dakika 20'' . Juzi Spika Pelosi alipokuwa attacked nyumbani kwake California ilichukua dakika 3 kwa Polisi kufika na kumkabili mhalifu.

Leo kuna mtu anatushawishi eti tuwalaumu Wavuvi badala ya kuwapongeza. Wananchi wa Bukoba wameonyesha moyo mkubwa , upendo na mapenzi makubwa kwa wananchi wenzao. Ahsante sana

Tunawalaumu wavuvi badala ya wale wa Dodoma wanaosema huduma za jamii zimeirika. Hivi uokozi siyo huduma za jamii! na kwa hili kulikuwa na huduma gani pale.

Kesho utawasikia wameahirisha kikao au wanatoa rambi rambi1 hapana! wakae kimya watuache tuomboleze, mafao yao yapo salama, waendelee na ngojera zao.

Ni aibu sana miaka 60 ya Uhuru.,
 
Una uhakika gani hao Polisi watakuja baada ya hizo dk 20?. Kwamba kuna ajali halafu mnakaa kusubiri Watu ambao huna uhakika nao. Huu ni ujuha.
Kila kitu unachofanya wewe huwa una uhakika nacho..unauliza maswali ya kijinga kabisa, halafu kwa nini hamuongelei mfano niliotoa wa meli ya mv bukoba..ilizama kwa sabab watu waliowahi kufika kwenye tukio walitoboa upande mmoja wakatoa watu hata 10 hawafiki halafu watu zaidi ya 500 wakapoteza maisha sabab ya haraka haraka bila hata kufahamu madhara ya wanachokifanya..
 
Ajali zinapotokea zinataka utulivu na subra kidogo ili uokozi ufanyike pasi na kuleta madhara zaidi..papara na haraka haraka mara nyingi zinaongeza madhara.
jifunze kupitia nchi zilizoendelea, kwanza all the time magari ya fire yako attention on runways, vifaa vyote vya uokozi viko tayari kwa lolote. Tanzania walileta mbwembwe pale MWL. NYERERE AIRPORT eti kwamba tulikuwa tunapiga mazoez ya kama hatar imetokea ad kuwaweka watu pressure juu kumbe mavi matupu wahuni awa.
masoko yanaungua wanakuja na magari ya maji matupu
 
W

Kifo ni kifo, wewe ndio utofautishe wapi na kwenye mazingira gani unaweza kutoa msaada wakti ajali inatokea..ndio sabab ya kukupa mfano wa ajali ya boda na meli, si kila ajali unaweza kutoa msaada hata kama uko tayari kufa ukisaidia majeruhi.
Kwa hiyo wewe unalaumu wavuvi waliotoa msaada leo? Wakati wanatoa msaada na kuokoa watu 26 wewe ulikuwa unakunywa mbege wapi au ulikuwa unachat na kufoward matukio tu.
 
Pongezi nyingi kwao. Nasikitika kuona niliyoyaona. Tunakosa ubunifu. Tunakosa vifaa. Tunakosa uongozi.

Ile excavator kama wangefunga kamba mapema, pengine hadithi ingekuwa tofauti.

Naamini ipo haja sasa ya kufanya serious self assessment kama nchi. Tusijidanganye, kama tumesimama. Tusije anguka
 
Hapana tuweke facts mezani

Wavuvi walipofika eneo la meli walikataza kutoboa meli , wakasema itazama
Aliyelazimisha kutoboa ni kiongozi wa serikali.

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Yanaonekana maswali ya Kijinga kwa sababu yanajibiwa na Mtu Mjinga kama wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…