Nimeibiwa gari na majambazi nyumbani, msaada tafadhali

Maswali hayana msaada hayo.
Funguo walimpokonya kwa nguvu wakaondoka
 
Pole sana ndo maana mm nikipak lazma nizime swichi ya waya ya pump ya mafuta ili hata ukiwasha utawasha adi ufe haliwaki
Unajidanganya.
Mwenzio amepokonywa kwa nguvu, hajaibiwa. Hata ungekua wewe hio switch ungeonesha kwa lazima. La sivo wakusambaze ubongo
 
Kuna wapuuzi hapa hawajawai kukutwa na matukio.
Kuna kipindi niko na bibi mmoja ana hela na nyodo sana.
Ikafika siku mi nirudi kwake kutoka job.
Nampigia yupo bar sa nane usiku anacheza pool zamani hizo.
Hapo sa nane usiku.
Nafika pale bar e bana tuondoke aaah akawa mkali huyo kanipa key nenda nyumbani ntakukuta duh.
Mi nikajiondokea.
Sasa ile nafika home kwake nikakuta majambazi wamengoa dirisha zima wameweka pembeni wanahamisha kila kitu.
Jamaa walikua na mkokoteni bajaj hamna enzi hizo.
Wanasomba wanapeleka wanarudi wanasomba tv cm,hela chochote kinachobebeka .
E bana nilivyowakurupua mbinu sisemi wakatoka baruti na mkokoteni wao walikua wa4.
Nikaacha vile vile nikamrudia huyu mwanamke bar.
Namkuta bado anacheza pool.
Najaribu kumwambia huko home majanga twende ukaone.
Ndo kwaanza ananambia "we wivu tu unakusumbua"
Mama umeibiwa kila kitu pale kwako hapafai
Ndio anashtuka "unasema"
Namjibu"nimefika nimekuta wezi wamengoa dirisha lote wanatoa vitu pale.
E bana akatupa fimbo ya pool ingia kwenye gari twende.
Tukafika kweli kakuta kile nilichomwambia ndio kilivyo.
Ayayaya dem kaanza kilio,nikaanza kazi kubembeleza.
Yule mwanamke uchungu ule wa kuibiwa wakati ye ni mtoto wa mjini ilimuuma sana.
Nilikodi rum hotel wiki atulie kidogo maana alikua anaweweseka tu then kilio.
Ikabidi ahamie kwangu tu maisha yaendelee
 

Haya matukio ya wizi recently yamekua mengi Sana.....

Juzi sista kavamiwa wamekomba kila KITU...
Nyumba ipo ndani ya uzio...
Ufunguo wa gari ulikua juu ya dressing hawakuchukua.....

Watakua waliwa spry maana wali ingia mpk chumbani wakiwa wamelala......

Tuna mshukuru Mungu hawakuwaumiza....Maana uhai ni muhimu kuliko Mali...
 
Pole sana mkuu....kwanini hukuweka steering lock?....halafu hayo maboya yanakujaga kamili na wese ya kutosha na wanawekea kule fuel pump kwa lita tano tano
 
Kamata mchoma dirisha.
 
Tatizo kubwa la kufunga Gps module hapa kwetu ni location za kuficha hicho kifaa , hii ilitakiwa iwe siri kuu , ila watu wameshindwa kuweka miiko ya kazi , kila mtu ikiwemo wezi , wanajua ni location ipi kwa gari ipi ,Gps module inawekwa.

Kuna raia huwa wanafunga hata GPS mbili at least kama mchongo umetoka kwa watu wa kampuni mojawapo, ya pili itakuwa inafanya kazi...
 
Nchi zetu za kibongo hizi yaani kila mahali ni tabu tu...

Pole sana mkuu, bila shaka kwa kudra za Mungu utafanikiwa kulipata...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…