Nimeibiwa milioni 5 Stendi ya Mabasi ya Magufuli

Nimeibiwa milioni 5 Stendi ya Mabasi ya Magufuli

Sijui ni karma au ni nini mpaka sasa wala sijui nifanyeje daaah nashindwa sijui nifanyeje wakuu na hapa ninapoandika navuja machozi nipo kwenye gari langu nimepaki nalia mwenyewe wakuu.

Nilifika na gari langu dogo aina ya Toyota crown athelete(namba za usajili kapuni) nilikuwa namsindikiza wife alikuwa anaelekea kondoa huko kwao kusalimia na pesa niliziweka kwenye briefcase yangu sasa nikashuka na wife kwenda kumsindikiza kwenye gari ABM coach la Dodoma nikasahau kufunga mlango wa gari aisee lahaula kurudi nikakuta mlango upo wazi briefcase yangu haipo na kila kila kitu hakipo na halafu ukizingatia hizo pesa ni za mapato ofisini nilikuwa napeleka ofisi za halmashauri x😩😩😩😩😩

Wakuu naombeni kama kuna mtu ataiona please mnicheki Pm tafadhali wakuu.

Nafwa nitafungwa mie😫😫😫
Nilikuonea wivu ulipokuja na hiyo gari nkaona nikuibie na mimi nikanunue crown,usijali nikilichoka nitaliuza pesa nitakayopata nitakupa
 
Toyota crown athelete(namba za usajili kapuni)
Unatufikirisha unajua?
ukizingatia hizo pesa ni za mapato ofisini nilikuwa napeleka ofisi za halmashauri x
Unajua ulichoandika juu na unachokifanya hapa haviendani unajua Bei ya Crown ni kiasi gani?
Nafwa nitafungwa mie
Unatembelea Crown alafu unalialia hivi mboni unaishusha thamani Crown?
Toyota-Crown-Athlete-2014-1.JPG
 
Sijui ni karma au ni nini mpaka sasa wala sijui nifanyeje daaah nashindwa sijui nifanyeje wakuu na hapa ninapoandika navuja machozi nipo kwenye gari langu nimepaki nalia mwenyewe wakuu.

Nilifika na gari langu dogo aina ya Toyota crown athelete(namba za usajili kapuni) nilikuwa namsindikiza wife alikuwa anaelekea kondoa huko kwao kusalimia na pesa niliziweka kwenye briefcase yangu sasa nikashuka na wife kwenda kumsindikiza kwenye gari ABM coach la Dodoma nikasahau kufunga mlango wa gari aisee lahaula kurudi nikakuta mlango upo wazi briefcase yangu haipo na kila kila kitu hakipo na halafu ukizingatia hizo pesa ni za mapato ofisini nilikuwa napeleka ofisi za halmashauri x[emoji30][emoji30][emoji30][emoji30][emoji30]

Wakuu naombeni kama kuna mtu ataiona please mnicheki Pm tafadhali wakuu.

Nafwa nitafungwa mie[emoji31][emoji31][emoji31]
Crown Athletes, Briefcase, Mil.5, dah! Mkuu wewe ndio Kabila la kulekule eeenh!?
 
Uza au weka Bondi hiyo gali ulipe pesa ya ofisini
 
Una Tembea na hela zote Za nini na siku hizi mambo yamerahisishwa?

Ukinikuta na hela nyingi kwenye pochi ni 20,000
 
Yaani aibiwe 5 milioni halafu apate nguvu za kuanzisha uzi na kujibu comments ..

NJAA MBAYA Sana [emoji1787][emoji1787]
Hapo ndipo nilipojua ni chai, majuzi tu nilidondosha walleti ikiwa na elfu60 nilihisi kichwa kuwaka moto Hadi Leo naugulia
 
Hufungwi.

Hivi Stand kubwa kama Magufuli haina cameras?

Bila shaka wanayo. Nenda wakuangalizie. Pengine wanaweza wasitambulike ila ikakuhakikishia usalama wako.

Ila ulichokifanya ni uzembe wa hali ya juu.

Uza crown lipa pesa za ofisi.
Nilikuwa nafikiri kama wewe mpaka tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu lilipotokea na hatua zilizochukuliwa.
 
Embu jisachi vizuri hujajiibia kweli au hujampa wife ukizani ni mzigo wake embu muulizw vizuri
 
Ahaa... kumbe mkuu Mzimu wa Kolelo umetag post ya Koses ya May 21, 2023 ambayo alipost akionyesha yeye ni mwanamke anatafuta mwanaume jobless kumjoin London, leo anapost akiwa mwanaume aliyeibiwa ela kwenye briefcase Magufuli Bus Terminus akimsindikiza mkewe kupanda basi la kwenda Kondoa.

Kwahiyo Koses ni Hermaphrodite!

Astaghafilullah Wahariri waongezwe JF ili kuchuja, kubaini na kukataa posts za kuchafua watu na taasisi.
Halafu lilivyo PUUZI kiwango cha LAMI
linatumia ID mbili tofauti
Sasa MOD wameziunganisha hiyo @koses na ya Bilionaire kekeman

anazidi kuumbukaJINGA lisilokuwa na AKILI
 
Sijui ni karma au ni nini mpaka sasa wala sijui nifanyeje daaah nashindwa sijui nifanyeje wakuu na hapa ninapoandika navuja machozi nipo kwenye gari langu nimepaki nalia mwenyewe wakuu.

Nilifika na gari langu dogo aina ya Toyota crown athelete(namba za usajili kapuni) nilikuwa namsindikiza wife alikuwa anaelekea kondoa huko kwao kusalimia na pesa niliziweka kwenye briefcase yangu sasa nikashuka na wife kwenda kumsindikiza kwenye gari ABM coach la Dodoma nikasahau kufunga mlango wa gari aisee lahaula kurudi nikakuta mlango upo wazi briefcase yangu haipo na kila kila kitu hakipo na halafu ukizingatia hizo pesa ni za mapato ofisini nilikuwa napeleka ofisi za halmashauri x😩😩😩😩😩

Wakuu naombeni kama kuna mtu ataiona please mnicheki Pm tafadhali wakuu.

Nafwa nitafungwa mie😫😫😫
OGOPA SANA TEKNOLOJIA

Thread zako za nyuma zinaonesha mada zako ni chai tena isiyo na sukari
 
Fanya utafiti Kwa akili tu hapo hapo stendi watakuonyesha wezi maana maagent na hao wapiga debe wa mabasi wengi wanawajua wezi na Hadi wanaweza wakakwambia wanamhisi ni Nani maana huwa wanaangalia mienendo Yao wakiona mwenzao analewa Sana na starehe ujue kapiga mtu.
 
Back
Top Bottom