Nimeingiza faida ya 1,092,600 baada ya siku 90 za biashara yangu

Nimeingiza faida ya 1,092,600 baada ya siku 90 za biashara yangu

Siku tisini (90) baada ya kufungua Biashara.

Habari wana JamiiForums, leo nimekuja kwenu kupata maoni kuhusu mwenendo wa biashara yangu hii niliyoianza siku 90 zilizopita.

Nilifikiria kuanza biashara hii baada ya kazi niliyokuwa naifanya kufa. Wakati nafikiria kufungua biashara nilikuwa sina mtaji na sikujua nitaupata wapi lakini niliamua kutafuta wapi wanauza bidhaa hizo kwa jumla ili nikifanikisha kupata pesa nisiangaike kutafuta mzigo unapopatikana.

Badaye niliamua kuuza kiwanja changu kwa shilingi 2,000,000/= baada ya makato ya dalali na wakili (wakili tulichangia na mnunuzi) nikabakiwa na 1.9 ku-cut story short, nilikwenda kununua mzigo baada ya kulipia chumba, nauli, nilifanikiwa kuanza na mzigo wa 900,000+

Baada ya kufungua biashara nilianza kwa taabu maana wanasema mwanzo mgumu, lakini nilipambana nikawa kila shilingi ninayouza naagiza mzigo Dar, hivyo hivyo baada ya siku kadhaa mahitaji ya wateja (wanaoulizia) bidhaa fulani ikawa kubwa ikabidi nitafute sehemu nikope pesa niongezee mtaji nikapata 800,000 nikaongeza mtaji dukani.

Ikumbukwe kwamba hapa dukani sitoi matumizi zaidi ya matumizi ya kulihudumia duka kama umeme, mlinzi nk.

Hivyo mpaka leo siku tisini nimeingiza faida ya 1,092,600/= .

Swali langu kwenu: Je, ninakwenda vizuri na biashara hii au napiga mark time tu?
hongera sana! Baada ya mwaka utakuwa mbali kama ukiwa na nidhamu ya pesa. Ama kweli biashara ni mchezo wa aina yake
 
Kumbe watumishi wa umma huwa wanatukanwa bure
Mkuu ulikuwaga hujui? Na wanaobeza sana watumishi wa umma mi natambua kabsa hawajai kujiajiri wanajua kujiajiri ni very simple. Mi nimejiari kwa biashara ndogo ndogo ambapo mtaji huwa sizidishagi 50,000 kwa kuchukulia mzigo wa kuuza cku hyo. Ila nikipiga mahesebu kwa mwezi faida huwa haizi 350k lkn bado mtu anakwambia et kujiajiri n kuzuri. Wakati mwalimu analipwa zaidi ya 600k

Tuache utani kujiajiri n kuzuri but kuna changamoto sana kuzidi za kuajiriwaaa
 
Kila la kheri mkuu kwenye ajira yako ila usisahau kujiajiri
 
UPDATE

From JANUARY TO MARCH

Hiki ndicho nilichokivuna 747,050/=

Habarini wana jamvi wengi walitamani kusikia mambo yapoje baada ya miezi mitatu mingine. Kiukweli biashara ni ngumu lakini Mungu ni mwema hicho ndicho nilichovuna
Najua wapo watakao beza Karibuni

Picha naleta soon
Hongera mzee kwa hicho cha halali upatacho,kuna matahira watakuja hapa na kukwambia hiyo faida ndogo sana wanadhani watanzania wote wanafanya kazi BOT au wanamiliki biashara kubwa kama Mo Dewji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba nikushauri kitu biashara is matter of location kuna mdau alisema humu kwamba usiogope ukubwa wa kodi as long as ukipata sehemu nzuri wewe amia hapo believe me utafikia kwenye ndoto zako.

Umesema upo kanda ya ziwa ila hujasema upo mkoa gani. Ningekushauri hapo ungeongeza na nguo za kina Dada vibode pamoja na nguo za watoto .
Hapa mwanza ukitaka wanapouza nguo kwa jumla nitakuelekeza hapo pamba road nimeona machinga wengi wamefanikiwa walianza kama wewe ukiwa na laki mbili tu unatoka na mzigo mkubwaa wengi walianza Chini zaidi yako but now wanayo maduka makubwa tu hapo mwanza.
 
Faida y laki tatu kwa mwezi mkoa aisee hapo komaa biashara inalipa sana hiyo endelea kuongezaa mzigo na mali zingine mbele huko utajikuta unaingiza laki 3 kwa siku,achana na yule bishoo pale juu anadai unaingiza pesa kwa tabu,usikute yuko mtu wa kutumwa tu.
 
nakupongeza ila iyo faida ni ndogo sana ukilinganisha na muda hivyo usibweteke kujiona umefika na fanya biashara kuna watu kwa siku wanapata faida ya sh 50,000 na mtaji mdogo chini ya huo wa kwako piga
hesabu kwa siku 90
 
Mkuu ungetaja na biashara yenyewe ingependeza zaidi sio kuweka figures tu
 
Faida y laki tatu kwa mwezi mkoa aisee hapo komaa biashara inalipa sana hiyo endelea kuongezaa mzigo na mali zingine mbele huko utajikuta unaingiza laki 3 kwa siku,achana na yule bishoo pale juu anadai unaingiza pesa kwa tabu,usikute yuko mtu wa kutumwa tu.
Asante Babu
 
Back
Top Bottom