Nimeipenda hii kutoka X. Watanganyika tukitafakari, kila mmoja kwa dhamira yake

Hakuna watu wanafiki kama waarabu.
Angalia Middle East.
 
Ni watanzania lakini kati ya hao watanzania kuna kiongozi yoyote wa chama tawala au upinzani ndugu yake au mtoto wake amefariki?

Kila mmoja mbinafsi anaangalia maslahi yake..!

Msichojua ni kwamba veggies wamesimika mizizi yao kila taasisi ya umma na huko ndipo shida ilipo..!!
Hao mtandao wote wapo kwenye majeshi yetu mnategemea nini kitatokea?

Watanzania wengi wameridhika muhimu wanapata muda wa kukumbatiana na kuzaliana hawashtuki..!!
 
Unafikiri ni rahisi kuchukua nchi kijeshi?
Unajua mfumo wa jeshi ulivyo?

Hapo kwanza angekuwa na kesi ya kuvunja katiba ingeonekana kapindua nchi.

Swali; Je, kama angefanya hivyo angeungwa mkono na wanajeshi wenzie wa ranks tofauti? Kumbuka mtandao ni kikundi cha watu wapo mpaka jeshini.
 
Watanzania wengi wameridhika muhimu wanapata muda wa kukumbatiana na kuzaliana hawashtuki..!!
Unarudi huko huko kana kwamba hukusoma na kuelewa kilichoandikwa.

Kwani waTanzania wote ni lazima wawe viongozi wa kisiasa wa CCM au upinzani?

Kwa nini huwaoni hao waliouliwa kuwa ni miongoni mwa waTanzania, ambao wewe unashikilia tu kuwabeza?

Ni waTanzania ndio watakaoleta mabadiliko ndani ya nchi hii; mabadiliko hayataletwa na mtu yeyote toka nje.

Ukweli ni kwamba sasa nashindwa kujuwa unachong'ang'ania hasa ni nini katika mada hii.

Kwa hiyo wewe unachoona pekee miongoni mwa waTanzania ni unafiki tu basi; huwezi kuona kitu kingine chochote?

Bahati nzuri angalau unasema/bainisha "...waTanzania wengi..."; na nimekwisha kueleza huko juu huwezi hata siku moja kutegemea waTanzania "WOTE" washiriki katika kuleta mabadiliko. Hao wachache watayaleta; na "WENGI" hata hao unaowadharau watayafaidi mabadiliko hayo.
 
Miaka hii 10 wazanzibar wanakula wanashiba hadi wamevimbiwa, Watanganyika wamenawa ila wanasubiri kula, ndiyo maana hutamsikia mzanzibar akilalamikia muunguno.
 
Jeshi likipindua nchi yoyote, kitu cha kwanza hufuta hicho kijitabu chenu mnachokiita Katiba.

Kifuatacho mtacheka au mtalia, inategemea upande upi uko.
 
Miaka hii 10 wazanzibar wanakula wanashiba hadi wamevimbiwa, Watanganyika wamenawa ila wanasubiri kula, ndiyo maana hutamsikia mzanzibar akilalamikia muunguno.
Hili ninalielewa mkuu 'mkwelitu', wala halina ugumu wowote wa kueleweka.
Labda nikukumbushe tu kuwa siyo miaka mingi iliyopita wakati tulipokuwa hatutuliii kwa kuimbiwa "KERO ZA MUUNGANO" kila mara kutoka upande huo.
Samia Suluhu kamaliza "kero zote" zilizokuwa zikiwasumbua; na badala yake kazihamishia upande wa pili!

Hii haikuwa kazi ndogo, na anaifanya waziwazi bila hata ya kuwa na uoga wowote!

Tatizo ni moja tu kwa upande wangu; hasa kuhusiana na maudhui ya mada kama ilivyoletwa.

Je, ni kweli kwamba lawama yote ya haya yanayotokea tuwapelekee waZanzibar wote au tuyaelekeze kwa viongozi wanaoyasababisha na kwa hao wanaoungana nao kuyatekeleza?

Hata wakati ule wa kelele nyingi toka Zanzibar kuhusu 'kero za Muungano", hizo kelele zilitoka kwa kundi la watu waliojulikana; ambao sasa hivi wapo kimya kabisa kwa sababu midomo yao imejaa minofu; hawawezi kuzungumza.

Hawa siyo waZanzibar wote; na ninayo hakika hawawasemei waZanzibar wote.

Kuwahusisha waZanzibar wote kutowafanyia wema waTanganyika siyo sahihi.

Hilo pekee ndilo ninalotaka lieleweke.
Kuhusu kufaidika kwao na matokeo ya kukandamizwa waTanganyika, hili sijui tungetaka wafanye nini, wakatae huduma zinazotokana na hujuma hiyo kwa waTanganyika? Hii inawezekana?

Kuna wanachama wa CHADEMA toka huko, na wao wanafaidika na huduma hizo, na sijui kama nao tuseme kuwa wanaungana na Samia katika hujuma hizi bila ya kuwa na dukuduku mioyoni mwao!

Tunachotakiwa kufanya; na hasa vyama vya siasa kama CHADEMA, ni kuwasaidia hawa wanachama wao ili na wao waweze kupaza sauti zao kadri iwezekanavyo (hata kama hawataeleweka kwa jamii kubwa inayowazunguka).

Kutoa lawama tu, na kushutumu bila ya kushirikisha hao, hata kama wakiwa ni wachache, ni kuwaonea, na kuongeza mfarakanyo zaidi ndani ya taifa

Tuweke bayana palipo na ubovu, kila mwananchi auone ubovu huo. Atakayeufumbia macho kwa maksudi kwa vile tu unamnufaisha, huyo ndiye adui; na tumtambue hivyo hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…