Nimeishi na Watanzania kwa muda mrefu nimegundua idadi kubwa ina tatizo la (non sequitur), tatizo la kutoa majibu yasiyoendana na maswali yaliyoulizwa

Mkuu unadhani ni kwanini wa tz wako hivyo,nini chanzo na lipi suluhisho lake??,,na haya ndo upelekea kuongea umbea,majungu na fitina kati yao,hivyo siku nzima mtu anakua non productive,,anamaliza mwaka au kuanza mwaka hana hata wazo lakuwa na malengo katika maisha yake.
 
Kuna aina tatu za kujibu swali.
1. Swali kwa swali
2.Swali kwa jibu
3.Swali kwa maelezo
 
Kwenda zako huko, hiyo sio shida ya watanzania tu bali ni suala mtambuka la binadamu wote

Kuna sheria maalum za arguing ambazo unatakiwa ujifunze

Hizo sheria ziliwekwa ili kudhibiti hayo mambo ya sequitir yanayotokana na hisia
Sikubaliani hoja yako mkuu.
Kama huna shida nyingine e.g. unahisi kufuatiliwa, ulifanya jambo ovu mahali na ukimbia, au unadaiwa i.e. una RB n.k. kwa nini usitoe jibu sahihi na fupi kabisa? Ku- argue ni kubishania hoja kwa kutoa hoja inayoonesha mtizamo wako na uelewa wako juu ya hoja iliyombele yenu mnapokuwa ni watu wengi na hoja ipo moja. Ni sawa na kusema ni mdahalo (Debate) Unaunga mkono na unawashawishi na wengine waone kama unavyoona wewe. Lakini majibu ya waTz ni swali kwa swali e.g. Swali: Hapa ni Tanzania? utajibiwa: Kwani ww ulikuwa unaenda wapi😰😰
 
hapo itabidi watu wa psychology waje watuambie
 
Naamini ni dhihaka imechukua nafasi kubwa kwenye maisha yetu
Mfano mtandao wa Facebook umeharibiwa na dhihaka ndiyo maana utawasikia watu wakisema bidhaa za mtandaoni achana nazo au mchumba wa mtandaoni hafai
 
Hilo tatizo kweli lipo, hata kwenye mada za humu lipo sana tu.
 
Kwenda zako huko, hiyo sio shida ya watanzania tu bali ni suala mtambuka la binadamu wote

Kuna sheria maalum za arguing ambazo unatakiwa ujifunze

Hizo sheria ziliwekwa ili kudhibiti hayo mambo ya sequitir yanayotokana na hisia
Huwa naingia baadhi ya forums, namna wanavyojadili mada zinazoletwa na namna sisi tunavyofanya ni tofauti kabisa mkuu. Mfano ni hapa jf.

So, ni kweli hata kama ni tatizo la kidunia ila kwetu limezidi huenda.
 
hapo itabidi watu wa psychology waje watuambie
Tusubiri wakija watasema. Wakati tunasubiria.. kwani hujaiona mifano e.g. watu wanazungumzia hapa Jf yaliyojiri katika vita huko Gaza lakini ghafla bin vuu anakuja mtu anasema USA na Myahudi ni mashoga. Sasa unajiuliza; vita ni mauaji na uharibifu mkubwa; sasa habari za ushoga zinaingiaje? Hilo ni nje kabisa ya mada(Hoja).
 
kwangu binafsi mijadala ya kihisia naiona kila mahali kuanzia youtube, reddit, quora mpaka hapa

hiyo ndo mitandao ninayotumia, labda huko kwingine watu ni wastaarabu

mimi naona ni asili ya binadamu tu kubisha na kuwa mkorofi mkorofi
 
Kuna mtu alikuja sehemu tuliokua tumekaa kabla hajafika ati anauliza haya mavi ya mbuzi nani kanya hapa?
Haloo kilichomkuta ilibidi tena tugharimie matibabu yake.
 
Unawa compare Watanzania na mataifa gani tuseme? Logical fallacies exist in court judgements, bureaucratic decisions, academic theses and such. Real life has no need for them, and still most people make the correct choices in daily life.
 
Unajua hiyo kitu inasababishwa na nini? UJINGA ULIOTOPEA.
 
Maisha hayako serious kiasi hicho, kaa bar agiza castle lite relax mkuu, kwan huu uzi unahusu nn
 
Kila binadamu ana matatizo.

Sio watanzania tu. Hata wazungu, wahindi, wafilipino, wachina n.k

Hakuna universal formula ya kumjibu mtu.

Mtu atatoa jibu kulingana na mood na uelewa wake.
 
Hiyo kitu iachie AI sababu it's purely logical, soul-less, void of any sense of culture and without any human feelings
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…