Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Jamaa anadanganya waziwazi utadhani hakuna ushahidi…Du kweli jamaa noma
Labda alikuwa anataka attention yangu tu 🤷♂️ 🤣.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamaa anadanganya waziwazi utadhani hakuna ushahidi…Du kweli jamaa noma
😀ila mimi naona njia nzuri ya kutambuana kwa jina ni una za naitwa fulani ex Athuman naye amalizie naitwa like Amina AshaMwingine unamuuliza unaitwa nani ,naye anakuuliza mm hapa au ..
Badala ajibu tu naitwaa Athumaniiiiii
na swali kwa mfanoKuna aina tatu za kujibu swali.
1. Swali kwa swali
2.Swali kwa jibu
3.Swali kwa maelezo
Kweli kabisaa!Nimeishi na Watanzania kwa muda mrefu nimegundua idadi kubwa ina tatizo la (non sequitur), tatizo la kutoa majibu yasiyoendana na maswali yaliyoulizwa
Hili tatizo linawasumbua sana Watanzania wenzangu inawezekana hawajafundishwa shuleni namna ya kujibu maswali kama sivyo wamejawa na dhihaka
Hili tatizo linasumbua sana hasa kwenye kuchangia hoja au kujibu maswali
Mfano mtu anaweza kuuliza hivi??
Ni nani msanii bora wa muziki Tanzania?
(Non sequitur)
1: Mziki wa Tanzania hauleweki
2: Hivi Tanzania kuna wasanii?
3: Wasanii wenyewe wako wapi
(Correct answers)
1: Nadhani Diamond Platnumz
2: Binafsi nadhani ni Alikiba
Hata katika jamii zetu hili tatizo linasumbua sana
Madhara yake makubwa ni watu kutokupata majibu ya maswali yao
Mimi Mr Why ni mpenzi wa mitandao ya kijamii huwa kichwa kinaniuma sana pale naposoma nyuzi za maswali yaliyoulizwa na wadau lakini hakuna jibu hata moja alilojibiwa zaidi ya majibu yasiyoendana na maswali
Ndani ya jamii mtu anaweza kuuliza Simba au Yanga wanacheza lini?
Non sequitur
1: Simba au Yanga wamechoka msimu huu
2: Watachezaje na hawana lolote
3: Mpira wa siku hizi hamna kitu
Sahihi
1: Wanacheza kesho
2: Watacheza tarehe 5
3: Tarehe tano saa tisa
Niliacha kabisa kutumia Facebook kwasababu ya dhihaka zilizoshamiri katika mtandao huo hakuna ninachojifunza zaidi ya kuumiza macho yangu kwa mwanga wa Device
Kwahiyo nitatizo kubwa sana linalotusumbua Watanzania
Njia ya kufanya nikujibu swali moja kwa moja
Mfano wa swali
Nitapata wapi bidhaa kwa bei nzuri?
Jibu
1: Kariakoo
2: China, nakadhalika
Badala ya hizo bidhaa unapeleka wapi? au biashara utaiweza? Biashara ya sasa hivi haitoki, una mtaji au unauliza tu bei?