Nachangia nini' jamani?!!!! Mpaka Sasa sina hoja hata Moja. Msaada tafadhali enyi wazoefu. Kukaa tu kimyaaa Huku ukiishia kuitikia tu kama ndondo haipendezi!
Poleni kwa msiba.
Mazungumzo na majibu yatatokana na yatokanayo kwenye msiba husika, mila na desturi.
Mfano:
1: Ni nini hitaji la msingi kwenye msiba husika unalolifahamu? Mfano: kuna deni la matibabu au shughuli nzima ya msiba/mgawanyo wa mali za marehemu? nk.
2: Kwa jamii husika, utaratibu wa kushughulikia misiba ukoje/wewe unapewa jukumu lipi kulingana na msiba husika/aliyefariki?
3: Unashirikiana vipi na familia husika kwa ujumla katika mambo ya kijamii?
4: Ulishiriki vipi kwenye msiba husika au unajipanga kushiriki vipi kwa kadri ya mila na desturi? Simama kwa kadri ya unavyojifahamu na toa ombi kwa kadri ya hali halisi?
5: Msiba ni wa nani na ameacha majukumu yapi?
6: Kuna sintofahamu yoyote kwako binafsi kifamilia? Andaa majibu?
7: Si yote yanakamilika siku moja, yaliyo ndani ya uwezo timiza, yaliyo nje ya uwezo omba ukatafakari na kufanyia kazi, yaliyo kinyume na taratibu eleza mtizamo wako kwa heshima na adabu na yasiyoeleweka, omba ufafanuzi.