Nuel27
JF-Expert Member
- Jul 3, 2026
- 461
- 915
Vitu vyangu kabisa hivi ,Kuna wadau kadhaa naona wanaiwakilisha vyema hii tasnia ni vizuri na wewe ungetupia link tukasubscribe .Wakuu, niaje?
Mwaka Jana mwezi September, nilikua na road trip ya Dar - Kigoma - Dar, nilidrive na nilikua na vituo kila mkoa/mji njiani. Nikaleta mrejesho hapa:
Mrejesho wa Safari yangu ya Dar Kigoma na kurudi Dar. Nimetumia Mafuta ya Tsh 230,000/= tu!
Wengi wanaulizia maswali mbalimbali na kushare experience mbalimbali, ikawa poa. Ila Kuna Jamaa anaitwa Kiranga akaongea like ushauri, kwamba ningeigeuza hii kua documentary narecord njiani na kuonesha miji na njia mbalimbali, ingekua poa.
View attachment 3683534
Niliichukulia poa, ila nikasema why not? Ukichukulia napenda sana kudrive na kuvisit new places daily. Ngoja nijaribu, maybe Kuna mtu atavutiwa au anapqta inspiration ya kwenda nilipo pita. Nikaanza.
Sikutaka kuingia gharama, nikastick na iPhone yangu, nikanunua dash mount na kuanza kurecord, for reason of anonymity, nikawa nafanya silent tours, just naweka subtitles siongei.
Kiutani kufika mwezi wa saba mwaka huu, YouTube wakanitumia email kwamba nimekua monetized na naweza kuanza kulipwa. Nikasema No way.
Nikamuambia shemeji/wifi yenu, akanipongeza, kama zawadi akanipa camera (GoPro 12) ili niache kutumia simu wakati wa kurecord.
So nikawa nikisafiri au nikiwa misele mjini naweka GoPro pale kwenye dash nakula nafanya silent tour. So Kuna fans/subs wakapenda, wanashauri iki na kile, na Mimi nikawa najaribu ushauri, just ikawa my new hobby.
How much napata, ni kiasi kidogo hadi sasa. Sio cha kulipia kodi Wala nini. Ndio maana nafanya kama hobby, siendi trip yoyote just kurecord, narecord ninavyoenda sehemu so nisiingie unnecessary gharama. Mfano tokea niwe monetized hiki ndio nimepata:
View attachment 3683540
Ukiwa more serious na ukachagua interesting niche, unaweza pata zaidi. Niche yangu Haina wadau wengi, ila ukiwa na niche za burudani, za umbea unatoboa mapema.
Kuna video moja unaweza kukuingizia ata $5 kwa views 1.5k wakati nyingine same views ata isivuke $1 kwahiyo ni hit and miss. Factors kama RPM, niche, urefu wa video, short au long form zina matter.
Kwahiyo kama hauna mishe na hauna aibu, siku Yako, mic na akili unaweza pata pesa ya mlo.
Pamoja.
Kuna mwamba wa kuitwa Explore with Bertin jamaa yuko vizuri sana kiasi cha kuanza kuvuka mipaka na kutuonesha uzuri wa majiji ya Afrika ,now yupo anaexplore Congo Republic if am not mistaken.
Then kuna upocoming anafanya vizuri sana kwa sasa wakuitwa Navigator Chindule ,kijana alianza na routes za daladala na mwakyembe train ndani ya jiji la Dar ,now naona naye kaanza kuvuka mipaka mfano now yuko anaexplore Kampala UG ,shoutout kwake.
Pia kuna mwamba wa kuitwa Allen The Explorer yeye naye ni wa mda kiasi ,yeye huwa anapiga trip ya mkoa kwa mkoa na huwa anakaa kwenye mkoa zaidi ya wiki mbili kuonesha vivutio,uzuri na historia mbalimbali ndani ya mkoa husika ,majuzi juzi alikuwa Zenji.Bigup kwake.
Pia kuna jamaa wa kuitwa Assad Mzururaji ,jamaa katumia hobby yake ya kusimulia na travelling .Huwa anasafiri mikoa mbalimbali hasa kwa bus ,juzijuzi alikuwa Mtwara jamaa ni bonge la story teller.
So natamani nikuongeze kwenye hii list mkuu kwa maana explore yako inaonekana iko tofauti na zote hapo juu.
LINK LINK LINK or username🫡🫡🫡