Nimejisikia uchungu sana nyimbo za taifa zilipopigwa wakati mechi kati Kili Stars vs Zanz Heroes inaanza


Umetamka mengi sana ambayo kwa kila mwenye akili timamu, yanafikirisha na kuleta hasira na kuuona Muungano wa namna hii ni uhayawani.

Ifike mahali, lazima uamuzi ufanyike: Ama Serikali 3 au Serikali 1. Kama yote hayawezekani, Zanzibar iachiwe, iwe tu kama Rwanda au Burundi, tukutane nayo kwenye EAC.

Tukishindwa kuyafanya haya kwa amani, kukiwa bado kuna upendo, yatakuja kufanyika kukiwa na chuki na uhasama, halafu mtakuwa mataifa mawili jirani yaliyo maadui, ambayo ni mbaya sana.

La kujiuliza zaidi, hivi hawa viongozi wa CCM wa bara wamekuwa walevi wa madaraka kiasi cha kukosa hata akili ya kawaida ya kuyatafakari haya. Mbona ile G55 ya akina Kasaka, tena chini ya Bunge la chama kimoja, walijenga hoja, walisimama imara katika akili zao, na hatimaye Bunge kuridhia kwa kauli moja kuwa lazima tuwe na Serikali tatu? Kama usingekuwa ushetani wa CCM, kwa azimio lile la Bunge, huu upuuzi unaoendelea usingekuwepo sasa hivi.
 
Una hoja ya Msingi,, hili nalo mkalitizame
# mtoto wa mama kizimkaz na hapa ipo
 
Minilijua utaanza kushangaa kwann kuna timu mbili za taifa ndani ya taifa linalojiita taifa moja?
Job truetrue/kazi kwelikweli cc Mjanja M1
 
Kazae tuu uchungu utaisha maana shule ulikuwa unasomea upumbavu
 
Nadhani swali la 3 ambalo umeliacha ndo lingekuumiza zaidi!
3. Tangayika ipo wapi?
 
Minilijua utaanza kushangaa kwann kuna timu mbili za taifa ndani ya taifa linalojiita taifa moja?
Job truetrue/kazi kwelikweli cc Mjanja M1
Alafu kwenye hizo timu za mataifa mawili, timu moja inatumia kits zile zile zinazotumiwa wote wakiungana!
Meaning kwamba Zanzibar wanajitambua sana!
 
Muungano ni shida bara ndio kama tunalazimisha hivi
 
Zanzibar hawana jeshi. Jeshi lililopo huko ni JWTZ!
 
Alafu kwenye hizo timu za mataifa mawili, timu moja inatumia kits zile zile zinazotumiwa wote wakiungana!
Meaning kwamba Zanzibar wanajitambua sana!
Yaani inafikirisha mnooo.
Kiasi kwamba unabaki kusema daah!ngoja tuupe mda useme tuu.
Tulidhani tumewawin kumbe walijua wanachofanya.mwenye muungano wake ashakwenda zake tangu enziiii
 
Tujitahidi kuiondoa ccm ndiyo aliyetukwamisha.Heri John Malechela kuliko Nyerere.
 
Umetamka mengi sana ambayo kwa kila mwenye akili timamu, yanafikirisha na kuleta hasira na kuuona Muungano wa namna hii ni uhayawani.
Kuna mengi yanayoshangaza. Mfano kupitia TCRA kila simu inayopigwa kuna kodi inakwenda Zanzibar.
Ukimpigia rafiki yako Ifunda kutoka Musoma kuna kodi inakwenda visiwani. Watumiaji Zanzibar ni wachache sana.

Zanzibar wapewe +259 yao ili wapate kodi. Si haki mtu wa Kigoma akiongea na wa Mwanza kodi iende Pemba na Unguja. Tena wana asilimia kabisa ya fedha zinazotokana na kodi za Watanganyika.

Bajeti ya SMZ haina fungu la kulipa madeni. Mikopo wanayopewa inalipwa na JMT ambayo ni Tanganyika.

Kuna utaratibu siku hizi, Rais anasafiri na Mawaziri wa serikali zote yaani JMT na SMZ. Hivi huyu wa JMT ni ipi hiyo?
Gharama za usafiri zinabebwa na Tanganyika kwa jina la JMT.

Hili la kulipa Watumishi wa Uhamiaji kwa jina la JMT halafu kukusanya mapato kwa jina la SMZ linafikirisha.

Ifike mahali, lazima uamuzi ufanyike: Ama Serikali 3 au Serikali 1. Kama yote hayawezekani, Zanzibar iachiwe, iwe tu kama Rwanda au Burundi, tukutane nayo kwenye EAC.
Wazee hawa waliona ulazimia huo. Jaji Warioba, Mzee Butiku na DR Salim. Hawa ni 'vijana' watiifu wa Mwalimu.
Ni watu wanoujua Muungano lakini walipendekeza serikali 3 ili uendelee. Waliyaona malalamiko hasa ya Tanganyika kubeba mzigo. Hawa waliofuata wamepuuza maoni ya Wazee hao
Tukishindwa kuyafanya haya kwa amani, kukiwa bado kuna upendo, yatakuja kufanyika kukiwa na chuki na uhasama, halafu mtakuwa mataifa mawili jirani yaliyo maadui, ambayo ni mbaya sana.
Hili lipo dhahiri,kama hawatatafuta suluhu ipo siku Muungano utavunjika kama glass, na Wazanzibar watakuwa na wakati mgumu. Tanganyika ina eneo, watu na mipaka na wala haitegemei Zanzibar kwa lolote au chochote

Rwanda ina watu milioni 9 kama ilivyo Burundi. Hawa wanafaida kwa Tanganyika kiuchumi.
Soko la watu milioni 18 ni zuri kiuchumi. Zanzibar ina watu milioni 2 nusu wanaishi Tanganyika!
Una hoja nzuri. Matatizo yalianza miaka mingi na G55 ni uthibitisho. Mambo yalikuwa mtindo huu, kuuza rasilimali na mapato. Ilifika mahali wanasema Zanzibar kwema atakaye aje. Watu waliacha kazi mipesa ilikuwa ina miminika.

Haya yote tunayojadili G55 waliyaona

CCM wanajua lakini matumbo mbele. VP ni mteuliwa wa Rais, anapewa maagizo tu ongeza asilimia za fedha hadi 9% , tatua kero za Wazanzibar haraka na anakaa vikao bila uwepo wa Watanganyika. Kujikomba Urais wa JMT???

Mawaziri wanajua. Waziri wa fedha anaidhinisha zitoke na kupelekwa huko. Waziri wa Muungano anajua pia, Wabunge wanajua.Tatizo, wanaogopoa matumbo yao, si Wazalendo na wenye uchungu kama wale wa G55

Habari njema, Tanganyika inarudi, waliokaa kimya na walioshiriki kutosimamia rasilimali tunawajua, tutawauliza

Tunataka Tanganyika ijisimamie, isimamie rasilimali zake iongozwe na wenye uchungu na wivu

Kama Muungano unahitajika, waulizwe Wazanzibar!
 
RIP mchungaji Christopher Mtikila hakuwahi shusha bendera ya Tanganyika kwenye ofisi yako.

Watanganyika wamejaa unafiki na uroho wa madaraka.Kupitia vitu hivyo viwili hawaoni umuhimu wa uwepo wa Tanganyika.
 
Kuna watu wanafikiri bila muungano wangekuwa mbali sana kimaendeleo

Maskini anajua kulalamikia kila kitu ili ajifariji
Hebu waachieni visiwa tuone kama haijawa Hongkong
Kila leo lawama
Sio kwa ubaya ila tumezidi
Kwa akili hizi tusubiri another 100 years
 
Sina uhakika unasimamia wapi, nadhani unasema tuache kulalamika kuhusu Muungano na mchango wa Z'bar.

Hakuna kulalamika bali kuonyesha ukweli. Ki uhalisia walalamishi ni Wazanzibar '' mamlaka kamili''
Nasi tunawaunga mkono, lakini mamlaka kamili hayaji bila Tanganyika, ndiyo maana tunataka Irudi.

Wazanzibar kupitia Wasomi kama VP Masoud wameaminisha Umma wanakandamizwa na Tanganyika.
Kwa mfano, hakuna tume ya pamoja ya Fedha kwasababu Watanganyika wanataka kuinyonya Zanzibar.

Rais H.Mwinyi kaweka wazi Dec 11 2022 kwamba wanaonkataa Tume ya pamoja ni Wazanzibar. Mwinyi anasema uwepo wake utalazimu Zbar kuchangia huduma kama za Jeshi , Polisi na Taasisi za Muungano.

Taasisi Muungano zinagharamiwa na Tanganyika. Mfano, Bajeti ya Ulinzi ni 2.7T, mambo ya ndani ni 1. 2T n.k.
Kwa udogo wa Zbar nje ya Muungano watakuwa na bajeti hizo., kwasasa hawana !

Bajeti ya JMT Zanzibar ina 9% kutoka 4.5% kwa ushahidi wa Katibu wa CCM Zanzibar.
Mapato ya kodi na huduma zitokanazo na Muungano yanabaki Zanzibar

Asilimia 21% ya ajira za Muungano ni za Wazanzibar lakini hatuoni asilimia za mishahara ya Watumishi hao.

Kwa lugha nyingine Zbar wanatoa ''Wataalam' kazi ya kuwalipa ni ya Tanganyika.
Tungalielewa laiti wangesema kuna asilimi X ya mishahara ya Watumishi kutoka Zanzibar wanaopatikana kwa 21%.

Ni utaratibu huo kwa uhamiaji, Watumishi wanalipwa na JMT, fedha zinazotokanzo na huduma ni za SMZ.

Kuna asilimia za Mikopo kutoka JMT kwenda SMZ, tusichokiona ni asilimia ya SMZ kulipia mikopo hiyo.
Mwisho wa siku mwenye mkopo ni JMT na mzigo huo anaubeba mlipa kodi wa Tanganyika .

Simu ya mtu na mkewe wakiwa Musoma wanalipa kodi TCRA na kuna asilimia inakwenda Zanzibar !!!
Wapewe 259 yao tutalipa kodi tukipiga nao watalipa wakiga Tanganyika. Kinyume chake ni uporaji


Ni yale ya Mbunge wa Zbar akwa ajii ya Wazanzibar kwa idadi ya watu 2,500 anapewa fedha za mfuko wa Jimbo kutoka Tanganyika kupitia Bunge la JMT. Fedha za mbunge wa watu 2,500 ni sawa na Mbunge wa Ubungo, Ilala, Ilemela, Kasulu, Hanang au Kibondo. Na kwanini Jimbo lisihudumiwe na BLW!

Orodha ni ndefu inatosha kuishia hapo.

Hoja ni ya ''abuse' ya Muungano. Tunakumbuka deni la Umeme la Bilioni 60 tangu Kikwete hadi Magufuli limefutwa. Zanzibar walikataa kulipa. Ni mwananchi gani wa Manzese anayepewa umeme bure kama wale wa Zanzibar?

Deni hilo ni hasara kwa Tanesco au limefidiwa na mlipa kodi wa Buguruni, Isevya, kidogobasi au Naliendele.

Hatuwezi kuendelea na utaratibu huu ambao Zanzibar inakuwa mzigo kwa kutokuwa na mchango wowote lakini inachukua kuliko eneo lolote la Tanganyika ikiwemo Dar es Salaam.

Hakuna anayekataza Zanzibar isiwe Hong Kong, kinachosemwa ni ''abuse' ya Muungano.

Tutaweza kuikabili '' abuse ''ikiwa tutakuwa na Tanganyika itakayosimamia masilahi yake.

Hoja ya Tanganyika imeletwa na Wazanzibar ndiyo maana tunaunga mkono Zanzibar yenye mamlaka kamili.

Ikiwa Muungano unatakiwa, wakuulizwa ni Wazanzibar.
Ikiwa watataka Muungano lazima waonyeshe kuwajibika, siyo watu wa kudai wasichotengeneza! wasiwe mizigo

Hawana Bajeti za Wizara kubwa na Taasisi bado tunawapa fedha nyingi kuliko Bajeti yao.

Hakuna tatizo na maendeleo ya Zbar kwa rasilimali zao, kuna tatizo wanapo abuse Muungano ambao wao hawautaki ila pale tu penye mafao kupitia Tanzania. Tunaitaka Tanganyika sasa hatujaishika Zanzibar.
 
Kiufupi tu ni kuwa Tanzania tunaongozwa na mkoloni mpemba
Sio mpemba ni mnguja kwao kizimkazi hako hawstoki wapemba .ila wazenji ile akili ya kutawaliwa huwa wanalazimisha kujisogeza kwa waarabu .kama walivo wakongo kujisogeza kwa wafaransa.nlikaa msumbiji kila tajir anadsngsnywa mspain .hata faizafoxy mweusi tii anaamini yy muarabu wakati wazee wake ni waha wa kigoma.kisirisiri wanaamini zanzibar taifa la kiarabu hahahah
 
Rais Mwinyi alipongeza ZRA kwa kukusanya Takribani Bilioni 288 kwa miezi 5. (55.4 Bilioni) kwa mwezi
Ni kwa mujibu wa Gazeti la 'The Citizen'. Akitoa pongezi hizo Rais anasema mafanikio mengi katika ujenzi wa Barabara, maji, afya na elimu ni matokeo ya ukusanyaji mzuri wa kodi wa 'SMZ'

Jana Naibu Waziri mkuu Biteko amezindua Jengo la Uhamiaji Pemba lililogharimu Takribani Bilioni moja.
Katika uzinduzi huo alikuwa na kamishna wa Uhamiaji wa Tanzania na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani
Jengo limejengwa kwa gharama za Uhamiaji JMT, yaani kutoka Bajeti ya Wizara ya mambo ya ndani

Kama tulivyowahi kujadili, fedha za huduma za Uhamiaji Zanzibar zinabaki SMZ, lakini gharama za Uhamiaji zinabebwa na JMT ambayo ni kodi za Tanganyika. Kwanini SMZ isijenge jengo hilo kwavile wanakusanya fedha za Uhamiaji ?

Zanzibar inapata 10% ya Bajeti ya JMT, ina mgao wa fedha ziwe ni Mikopo au misaada na makusanyo ya kodi hayavuki bahari. Zanzibar haina mchango katika Muungano.

Gazeti la Mwananchi limetoa kanda na michango yake ya kodi kwa Taifa, Dar es Salaam ikibeba 84% , ikifuatiwa na Kanda ya Kaskazini, Ziwa, Kati , kusini na Nyanda za Juu. Zanzibar haikuonekana.

Pamoja na hayo fedha zinazokwenda Zanzibar kutoka Tanganyika a.k.a Tanzania ni nyingi kuliko kanda yoyote iliyotajwa hapo juu licha ya ukweli kwamba Zanzibar haina Bajeti za Wizara nyeti na zenye gharama

Hoja inabaki pale pale kwamba rasilimali za Tanganyika zimegeuzwa za Tanzania na hapo zinakuwa 'abuse'.
Hakuna msimamizo wa rasilimali za Tanganyika! Na abuse imekuwa kubwa sana awamu hii.

Tunahitaji Tanganyika isimamie rasilimali zake, kama Muungano unahitaji waulizwe Wazanzibar!
 
Nimekusoma vyema mkuuu tatizo linakuja kwenye utekelezaji kwa viongozi wetu
 
Nyerere alaniwe huko alipo katupotezea Tanganyika yetu.
Nyerere sio Mungu tatizo ni viongozi wa juu wa ccm,siku nchi ikienda upinzani Muungano utakoma maana watawapa wananchi wapige kura ya maoni km wanataka muungano au la,na hapo amini muungano utakuwa umefika mwisho,ipo sku moja tusiyoijua muungano huu utavunjika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…