Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kuna mambo yanayostaajabisha katika Muungano kwa bahati nzuri au mbaya Watanganyika hawayajui.
Kwa muda mrefu Wazanzibar waliaminisha Umma Tanganyika imevaa koti la Muungano na kuwanyonya.
Hoja imedadavuliwa na kuonekana ni ya kijinga na kipuuzi ikienezwa na watu wasio na Elimu, hata wenye elimu.
Kuvaa koti la Muungano ni hasara kwa Tanganyika. Rasilimali kila pato la Tanganyika limefanywa la Muungano.
AFCON Pamoja Bid ni kazi ya TFF wakishirikisha Kenya na Uganda. Waliokwenda Cairo ni Waziri wa Tanganyika na viongozi wa TFF. Gharama zote za maandalizi ya ' Pamoja Bid' zilibebwa na Walipa kodi wa Tanganyika
Ni haki AFCON kuchezwa viwanja vya walipa kodi wa Tanganyika katika miji yenye Viwanja kama Arusha na Mwanza
Ujanja umetumiwa , kwamba AFCON ni Bid ya Tanzania na hilo jina linatoa uhalali wa Zanzibar kuwa mshiriki.
Chama cha Mpira Zanzibar ni cha nchi jirani. Mchezaji kutoka Tanganyika anapewa hadhi sawa na yule wa kutoka Cameroun, India au Moldova. Katika mazingira hayo ushirika wa Tanganyika na Zanzibar AFCON unatoka wapi?
Ni utamaduni ule ule wa Wazanzibar kuzuia hata ndizi kwa kudai zinatoka Tanganyika. Katika mazingira ya kustaajabisha ni Wazanzibar hao hao wanaosema ikiwa sisi ni Tanzania kwanini wao wasiingize bidhaa bila kodi Tanganika! Wameruhusiwa sasa hivi uchochoro wa bidhaa kutoka nje ni kupitia Zanzibar! hatupati kodi za kutosha
Ni utamaduni ule ule wa kudai Uhamiaji ni chombo cha pamoja, lakini maduhuli na kila pato linalotokana na huduma kule Zanzibar linabaki Zanzibar. Malipo ya mishahara ya Wafanyakazi wa Uhamiaji Zanzibar yanatoka Tanganyika. Kwamba, tunalipa Wazanzibar wakusanye kodi !
Ni uhuni ule ule wa kuchukua fedha za kodi za Tanganyika kwenda kwenye kinachoitwa mfuko wa Jimbo.
Huko Zanzibar kuna Wwawakilishi na serikali yao, kwanini mfuko wa jimbo utoke Tanganyika?
Uhuni ule ule wa kodi zetu za simu kwenda Zanzibar kwasababu wanatumia 255. Kwanini wasipewe 259 yao!
Tanganyika haipotezi chochote kwa Zanzibar kuwa na country code yao, wapewe. Kuchukua kodi zetu si sahihi
Kuna mambo mengi sana ya kushangaza, akina Mwigulu na Mpango wanajua, ni washiriki
Wabunge wanajua lakini ni mwiko kuitetea Tanganyika! wanaruhusiwa kusema Mbowe akitoa kauli tu.
Ipo siku watu wote wanaoihujumu Tanganyika tutawauliza. Kazi moja tu tunayo, Kuirejesha Tanganyika.
Kama Muungano utahitajika si suala la Tanganyika, Waulizwe Wazanzibari.
Umetamka mengi sana ambayo kwa kila mwenye akili timamu, yanafikirisha na kuleta hasira na kuuona Muungano wa namna hii ni uhayawani.
Ifike mahali, lazima uamuzi ufanyike: Ama Serikali 3 au Serikali 1. Kama yote hayawezekani, Zanzibar iachiwe, iwe tu kama Rwanda au Burundi, tukutane nayo kwenye EAC.
Tukishindwa kuyafanya haya kwa amani, kukiwa bado kuna upendo, yatakuja kufanyika kukiwa na chuki na uhasama, halafu mtakuwa mataifa mawili jirani yaliyo maadui, ambayo ni mbaya sana.
La kujiuliza zaidi, hivi hawa viongozi wa CCM wa bara wamekuwa walevi wa madaraka kiasi cha kukosa hata akili ya kawaida ya kuyatafakari haya. Mbona ile G55 ya akina Kasaka, tena chini ya Bunge la chama kimoja, walijenga hoja, walisimama imara katika akili zao, na hatimaye Bunge kuridhia kwa kauli moja kuwa lazima tuwe na Serikali tatu? Kama usingekuwa ushetani wa CCM, kwa azimio lile la Bunge, huu upuuzi unaoendelea usingekuwepo sasa hivi.