Nimekatwa Tsh 5,300 kuhamisha Tsh 50,000 kutoka NMB mobile kwenda M-PESA

Nimekatwa Tsh 5,300 kuhamisha Tsh 50,000 kutoka NMB mobile kwenda M-PESA

Sasa hivi kila kona utakayotaka kupitia makato yapo yanacheka tu, yaani hakuna ujanja aisee! Weka sasa hivi milioni moja benki halafu nenda kesho kaitoe kwa njia ya foleni! Mbona utachekea Madaba!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
nilihamisha hela toka bank crdb kwenda tigopesa... aisee kwenye elfu 11 walikata elfu 3 nikasemaa sirudiii tenaaa
 
Nilikuwa sijawahi kutumia hii huduma lakini sasa nilijaribu wiki mbili zilizopita na sikuangalia salio.

Muda huu nimepata bank statement kwenye email ndio naona hayo makato.

Tsh. 5,300 (NMB Tsh. 4,491.53 na VAT Tsh. 808.47) imenishangaza kukatwa zaidi ya asilimia 10 ya fedha niliyohamisha.

Hongereni sana NMB Tanzania
Duh
 
Nimekupata mkuu 10% nyingi Sana angalau ingekuwa 2% kulingana na kipato Cha watanzania wengi. Yani wanashindana na Mungu kwenye makato kwasababu zaka lazima ukatwe 10% sasa nao eti wanaiga
Si sahihi. Kristo aliilegeza hiyo tozo ila mafarisayo na masadukayo ndio wanaoing’ang’ania to the letter 😃
 
Kweli kabisa, mimi sitaweza kufanya muamala tena. Watu wengi wataacha.
Serikali inapoambiwa inaweka mazingira magumu kwa wawekezaji ni kwa vitu kama hivi, sidhani kama kuna muwekezaji kwenye sector ya pesa mtandao anayeona kuna faida kwenye soko la Tanzania, na ndio maana wengi wanaishia Kenya
 
Ahhh unawalaumu bure,tumia kadi wenzako tuliacha kuamisha fedha
 
Yaani hiki wanachofanya ni wizi wa mchana kweupe. Hiyo transaction haitakiwi kukatwa zaidi ya Tsh 1000.

Hapo nilipomtumia mtu nilikatwa hela ya kutuma halafu na yeye akakatwa alipoenda kuitoa.
Mama anaupiga mwingi
 
Yaani hiki wanachofanya ni wizi wa mchana kweupe. Hiyo transaction haitakiwi kukatwa zaidi ya Tsh 1000.

Hapo nilipomtumia mtu nilikatwa hela ya kutuma halafu na yeye akakatwa alipoenda kuitoa.
Ladhima tutoe gawio Serikalini" Dikteta alikuwa ana bana wakurugenzi wapeleke magawio serikali, Sasa Mama ana wabana wa nanchi tupeleke gawio serikali.
 
Nilikuwa sijawahi kutumia hii huduma lakini sasa nilijaribu wiki mbili zilizopita na sikuangalia salio.

Muda huu nimepata bank statement kwenye email ndio naona hayo makato.

Tsh. 5,300 (NMB Tsh. 4,491.53 na VAT Tsh. 808.47) imenishangaza kukatwa zaidi ya asilimia 10 ya fedha niliyohamisha.

Hongereni sana NMB Tanzania
KODI hiyo Kama Hutaki Kuishi Tanzania hamia Burundi.
 
Hizi bank zinatupelekesha zinavyotaka yani hawajali chochote. Wakiamua kupandisha transaction fee wapandisha tu wanavyojua. BOT kama regulatory body nao wamechill tu wavuja jasho tunaumia.

Hii nchi ni Shenzistan.
Tozo ya serikali hiyo.
Wanaowapeleka wanavyotaka ni wanasiasa kina nchemba na ccm yake.
 
Sijailewa Serikali inataka ku discourage people from transferring money. This is too much. The Banks are also taxed from their earnings, this is double taxing.
 
Binadamu wote siyo sawa. Yani iyo shilingi 5,300 unaona nyingiiiii. Mara ya kwanza niliposoma nilidhani umeandika umekatwa 5.3 millions kuhamisha Billion 5.
Ulishakataa kuitwa Maghayo, sawa Tajiri Sir Winston Churchill.
 
"Mama" anakaba jiko na anakaba na choo.

Hakiliki wala hakuendeki.
Ndo maana Ndugai alisema tusubiri 2025 ili wananchi waamue kuchagua haya matozo au wachague atakayeachana na haya matozo.
UVCCM wakamfukuza uspika.
 
Ladhima tutoe gawio Serikalini" Dikteta alikuwa ana bana wakurugenzi wapeleke magawio serikali, Sasa Mama ana wabana wa nanchi tupeleke gawio serikali.
Kati ya mama na dikteta, nani "dikteta" sasa?
 
Back
Top Bottom