Nimekoma walahi! Pilau la buku nimelinunua kwa 32,000 za dripu mbili

Nimekoma walahi! Pilau la buku nimelinunua kwa 32,000 za dripu mbili

Kwa hali ilivyo bado kuna wanaouza msosi buku darasalama?
Kuna mmoja alikula wali nyama (mwingi), na matunda. Alikua na uhakika ile menu haifiki 5,000.
Akaingiza mkono mfukoni akakamata buku tatu akawa ananyoosha mkono kulipa huku anauliza bei. Muuzaji akamwambia nipe hiyo 1,000, akauliza kivipi? Alipoambiwa chakula alichokula ni cha shilingi 850 tumbo likaanza kumkasnga hapo hapo
 
Tatizo wewe ni mchoyo ndio maana "unaendesha" peke Yako, toa location ya Hilo chimbo ugali mboga nne buku watu wapone
Mbagala hapa sokoni 🤣 alafu masokoni kote msosi wa kumwaga tu.. soko lenye chakula bei juu ni simu 2000 mawasiliano peke yake. Na wanauza 2500
 
Ijue nguvu ya buku 😂😂😂
Buku tu.. unashushiwa kifusi uhangaike nacho..

Nakumbuka tuko udsm 2018 nikapelekwaga kwa mafundi wale wanaojenga kijazi miaka hiyo. Msosi wa buku sikuumaliza mana mwingi sana lakin kutoka pale kwenda chuo niliishia Coet tu nikaanza kukimbiza mwenge
 
Pole
Hali hii leo mbona kazi ipo!

Katika pitapita zangu maeneo flani flani hiv nikasikia sauti kutoka katika kipaza ikinadisha "pilau buku, pilau nyama buku... njoo ujipatie". Nikaona yesss, dunia ni yetu sote.

Nikajikoki pale ndizi ya mia mbili na juisi ya muwa. Nikaketi taratiibu nijipimie. Wallahi punde baada ya kujishindilia pilau la nazi nikasikia "prrr prrrr prrr" tumbo linaunguruma na maumivu kias.

Nikajaa kujishtukia niko mlangoni mwa choo cha msikiti mana hata nauli iliishia kwemye choo cha kulipia. Nikajimaliza pale vya kutoshana nguvu ikatoweka, nikaomba msaada wa pikipiki ya msikiti nikapelekwa hospitali. Hapa nilipo nina drips ya pili na nishamaliza elfu 32 kwa matibabu haya yanayoendelea

Dua zenu wazee
Dah pole Sana rafiki
 
Back
Top Bottom