Nimeku "miss" kwa kiswahili

Nimeku "miss" kwa kiswahili

Nakutamani, natamani kukuona. Ndio maana yake. Ila si matamanio ya kuduu, enheee
 
nimekumiss= umeadimika
hii pia nzuri:clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down:
 
Hapana.

Unachanganya kukua kwa lugha na kukua kwa matumizi ya lugha, vitu viwili tofauti.

Tuchukue mfano wa kwamba Kiswahili kilikua sana miaka iliyopita kwa sababu hakukuwa na Kiingereza, kikafikia maneno takriban 200,000 yajulikane kwa kila muongea Kiswahili, watu walikipenda kweli...

Nakumbuka mwalimu wangu wa kiswahili aliniambia lugha inaweza kuzaliwa, kukua na hata kufa.
Je, haiwezekani kuwa lugha fulani kuwa na maneno fulani na baadaye yakawa kama yamekufa labda kwa kutotumika japo yapo kwenye kamusi?
 
maana ya ku(miss) ni "kosekana" au "kutokuwepe sehem furan tarajiwa"
 
Nakumbuka mwalimu wangu wa kiswahili aliniambia lugha inaweza kuzaliwa, kukua na hata kufa.
Je, haiwezekani kuwa lugha fulani kuwa na maneno fulani na baadaye yakawa kama yamekufa labda kwa kutotumika japo yapo kwenye kamusi?

Inawezekana kabisa na kamusi za Kiingereza huwa zina maelezo mbele ya maneno kama hayo.
 
Nakutamani, natamani kukuona. Ndio maana yake. Ila si matamanio ya kuduu, enheee

umepatia.....

....shida ni watu wanajaribu kutafsiri neno kwa neno badala ya neno kwa maana matokeo ni kuja na misamiati ya hovyo mfano:
1. Nimeku-miss=nimekukosa...tafsiri ya kijinga kabisa
2. Breaking News=habari mpasuko...huu ni ujinga uliopevuka
3. Newshour=habari za saa....upumbavu usio kifani
 
Aise! JF raha kwelikweli. Embu ngoja na mimi nijitutumue
1. I have missed you = Nimekuwa mpweke kukukoswa
2. Breaking news = Habari ya ghafla(Habari ya kushitukiza)
3. News hour = Wakati wa habari (Saa ya habari)
Vipi hapo
 
Habari mpasuko!
 
naungana na Mbute na Chai
katika khali ya kawaida "Ku-miss" ni hali ya kuwa na tamanio la kuona au kuwa karibu aidha na mtu au kitu au kuwa mahala fulani-hiyo hali inapelekea mtu kuwa na upweke ambao hauwezi kuondolewa mpaka amwone/aone hicho anachokihitaji!
mfano: nimemiss nyumbani kwetu; nimemmiss mpenzi wangu/mtoto wangu etc. kwa misingi hiyo nadhani si jambo baya sana kutumia neno "UPWEKE".
Pengine watu watakuja juu na kusema neno upweke lina maana fulani, inawezekana ikawa kweli lakini pia katika kukuwa kwa lugha neno moja laweza kubeba maana nyingi tofautitofauti au likatumika kulingana na muktadha uliopo kwa wakati huo. Hivyo: "I miss you=nina upweke juu yako"
..SAWA SAWAA!!!!

[
1. I have missed you = Nimekuwa mpweke kukukoswa
[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom