Nimekubali elimu ya shule haina maana mtaani

Nimekubali elimu ya shule haina maana mtaani

MIMI SIO muhanga wala Muhenga nachangia mada tu km ilivyowekwa malumbano ya hoja, kuna tatizo kwani? Sipo tayari ku-support unachoki-support kila mtu ana uelewa na mtazamo wake iwe hasi au chanya Ila maoni ya kila mmoja wetu yaheshimiwe iwe kwa kujenga au kubomoa Ila ujumbe umefika
Siku zote hatuendi shule ili tupate ajira. Najua hili kwa Tanzania ni gumu na wahitimu siyo wa kulaumiwa. Uongozi wetu ndiyo ume-set mambo yawe hivyo.
 
DSM ndo rahisi kutoboa ukiwa Una fine tune unaweza kufikia lengo.

Huwa nashangaa graduate anakimbilia kijijini na kuacha Ku-hustle DSM .

Sio lazima ule madawa Ila waweza wewe Kuwa ndo hayo madawa yenyewe.

Sky is limit everyday RICH.
Unaonaje ma-gradiate wa nchi nzima wangehamia Dar ili kutoboa kirahisi?
 
Hahaha mkuu nitakupa mfano mdogo tu Ila sijui km utakufaa lakini ngoja nikuambie uelewe wapo watu hawajasoma Ile kusema eti wamesoma Ila wana Mafanikio elewa ninachokwambia wapo watu sio kwamba wamesoma Ila wana Mafanikio hio maana yake ni kwamba Elimu sio Mafanikio, unielewe vizuri nakuambia tena Mafanikio sio Elimu na Elimu sio Mafanikio, Mjinga huyo anamuajiri Msomi yeye anaingiza Million 30 kwa Mwezi alafu Msomi anaingiza Million 3 kwa Mwezi nani mjanja hapo?
Umesema vyema kwamba elimu sio mafanikio ila ujue kwamba kuwa na elimu ni sehemu mojawapo ya mafanikio ya mtu i.e. Elimu inachangia pakubwa sana ktk mafanikio ya mtu. Kama hoja ni kuajiriwa basi mwenye elimu atajiongeza na ataikubali ajira hiyo aliyopewa na mtu mjinga. La msingi hapo ni amepata ajira - hatoangalia eti anayemwajiri anaingiza kiasi gani kwa mwezi. Ni sawa na kuhoji mbona Serikali inaingiza trilions kwa mwezi e.g. kupitia TRA, kwa nini inalipa kima cha chini laki 3?
Yeah. Ni kweli unaweza kuwa na mafanikio licha ya kwamba huna elimu, lakini unaweza kushindwa kufanikiwa kutokana na kukosa elimu e.g.Tumewaona matajiri waliofanikiwa bila elimu lakini hao hao walipobaini kwamba wanakwama hapa na pale kwa sababu tu ya kukosa elimu walijitosa kuipata hiyo elimu japokuwa ni kwa njia ya private tuition tena kwa siri ili kuepuka fedheha.
Tukiweza kuyafuta mawazo potofu kwamba nikisoma/nikipata elimu nitaajiriwa au nitafanikiwa kimaisha (kitu ambacho si gerentii) tutakuwa tumejikomboa sana kifikra na kwa hilo tutajiepusha kupata sonona(Stress) pale mambo yatakapokwenda vinginevyo.
 
Siku zote hatuendi shule ili tupate ajira. Najua hili kwa Tanzania ni gumu na wahitimu siyo wa kulaumiwa. Uongozi wetu ndiyo ume-set mambo yawe hivyo.
Majibu kumbe unayo ndio maana nikasema suala la Mtoto kwenda Shule liwe la hiari ya Mzazi na Mtoto, sio inalazimisha watoto waende Shule alafu wakimaliza mtaani wanabakia wanazagaa tu mtaani huo ni usenge
Yeah. Ni kweli unaweza kuwa na mafanikio licha ya kwamba huna elimu
Itoshe kusema kwamba umekubariana na Mimi katika hili kwamba Mafanikio sio Elimu na Elimu sio Mafanikio,
 
Siyo vyuo vya Tanzania unazungumzia hapa. Elimu yetu ni hovyo kiasi ambacho wahitimu wanakuwa hawawezi kutafakari mambo madogo kabisa.
Huyo wa aina hiyo ni kwamba hakujua kilichompeleka shule. Yeye alikuwa anahudhuria darasani tu. Masomo mengi ya darasani esp.Science humjenga mwanafunzi kufikiri na hivyo kukua kiakili.
Hata kusoma na kuandika ujue kunamjenga mwanafunzi ili baadaye aweze kuwasiliana na watu nje ya nyumbani vizuri zaidi - Ni mojawapo ktk communication skills. Kwa mfano ukija huku umasaini ndani ndani huku utajua ninachokisema hapa.e.g. bado karne hii unahitaji mkalimani ww uzungumze kiswahili na mkalimani wako asaidie kuwaambia Jamii kwa kilugha na Jamii wachangie kwa kilugha halafu mkalimani akutafsirie kwa kiswahili! Kikao cha nusu saa kinachukua masaa manne(4hrs).
 
Sawa mkuu unacheka /unazomea lakini ikitokea e.g. zimetoka ajira Serikalini au Private Sector ni lazima kunakuwa na vigezo kwa waombaji na kiwango cha elimu kikiwa ni mojawapo. Sasa huyo asiyekidhi vigezo simply kwa kukosa elimu au hana elimu, anakuwa Naturally Disqualified.
Wewe ndio unasema hivyo Ila sicho ninachomaanisha Mimi, ninachomaanisha km kwamba mtoto/kijana akimaliza kusoma hapati kazi/ajira ilikua na umuhimu gani wa kwenda kusoma? Si angefanya kazi za kumuingizia kipato let say hio zaidi ya miaka 10 anayoisotea kutafuta Elimu angeisotea kufanya Jambo linalomuingizia kipato mpaka anafika umri wa kumaliza elimu yake si angekua mtu mwenye Mafanikio sana, sijui unanielewa vizuri lakini?
 
Unaonaje ma-gradiate wa nchi nzima wangehamia Dar ili kutoboa kirahisi?
Namna gani ya kifiri hii

Kamshauri Nyanda aka DSM itakuwa fursa zaidi kwake. Suala la Graduates wote kuhamia DSM linamuhusu nini Nyanda au aloyepewa ushauri yaani hao Graduates wote yeye wanamuhusu nini.

Hii haina tofauti na Mfano mtu umshauri mdogo wako oa ambae hana mtoto then wewe unahoji je ma-single mother wote wataolewa na nani.
 
Wewe ndio unasema hivyo Ila sicho ninachomaanisha Mimi, ninachomaanisha km kwamba mtoto/kijana akimaliza kusoma hapati kazi/ajira ilikua na umuhimu gani wa kwenda kusoma? Si angefanya kazi za kumuingizia kipato let say hio zaidi ya miaka 10 anayoisotea kutafuta Elimu angeisotea kufanya Jambo linalomuingizia kipato mpaka anafika umri wa kumaliza elimu yake si angekua mtu mwenye Mafanikio sana, sijui unanielewa vizuri lakini?
Nakupata vizuri.Hoja yangu ni pale uliposema hakuna haja ya elimu. Mimi nikakuambia elimu inaanzia tangu chekechea hadi huko juu. Sasa kama unapata elimu basic na ukaona hiyo inatosha mie sipingani na hilo ila sio mtu anakuwa empty kabisa.
 
Naona sasa tunaanza kuelewana
 
Sawa mkuu unacheka /unazomea lakini ikitokea e.g. zimetoka ajira Serikalini au Private Sector ni lazima kunakuwa na vigezo kwa waombaji na kiwango cha elimu kikiwa ni mojawapo. Sasa huyo asiyekidhi vigezo simply kwa kukosa elimu au hana elimu, anakuwa Naturally Disqualified.
Yaani mkuu don't take serious mi nipo nipo tuu kusogeza mada mbele...

Hapa nilipo sina A wala B na nimemaliza hayo mambo kitambo hikoo...
 
Wewe ndo hauna maana mtaani wala siyo elimu, kwa dunia ya sasa ya utandawazi umemaliza chuo na bado unaongea huu ujinga?
Umeshindwa hata kuwa mwizi wa kutumia akili!
Fact📌🔨
✅️Pesa zipo mikononi mwa wajinga
Wajinga ndo waliwao
✅️Now days kuna remote work nyingi sana.
✅️Kuna hii network marketing kashindwa kabisa,
Kuna duka la mtandaoni
✅️mfano samart watch t800 utra ni 15000 lakin mtaani washazoea 25000 kwenye maduka ya rejareja,chaja kama zile super fast charge za samsung mtaani hadi 25000 lakini dukani ni 130000 za watr 45,10000 watt45 na 9000 za watt 15
✅️kuna line za cooperate ambazo unapa gb15 kwa 10000 na unaweza kuzirusha kwa wafumiaj wengine wa halotel ukiamua kufocus na online marketing hasa kwa wanachuo pia mtaani pia ukaamuu kuuza 1300 kwa qb 1 na gb kwa 1000 kwa wateja wa jumla kuanzia gb10+
 
Yaani mkuu don't take serious mi nipo nipo tuu kusogeza mada mbele...

Hapa nilipo sina A wala B na nimemaliza hayo mambo kitambo hikoo...
Hiyo cm unayotumia kuandika koment unaweza kuitumia na ikakuwezesha ktk. mambo mengine A and B . Itumie kuwasiliana na wenzako, Ndugu, Marafiki au Jamaa wakupe ramani - Using'ang'anie kukaa Dar.
 
Mambo ya kusoma na kutosoma ni nadharia Ila ukiwa smart na Una sense of who you are , unaweza kushindwa kulaza hata buku 20 kwa siku.

Vijana mnatishana Sana kiukweli wakati nipo Bukoba niliambiwa maisha ya DSM magumu Sana haya maneno niliambiwa na kaka zangu Ila to be honest ukiwa smart DSM kufanikiwa 90%

Pia ukitaka utoboe maisha na uishi bila stress kuwa na kitu kinaitwa "seed perspective"

Chochote ulichonacho kitazame kwa mfumo wa mbegu iwe, pesa ,elimu, nguvu , akili n.k

So ukiwa na mbegu tayari unaanza kutafuta mahali pakwenda kuipanda mbegu yako.

Ikiwa Una nguvu angalia sehemu ya kuiwekeza hiyo mbegu the same ukiwa na akili au Elimu na pesa.

Elimu imekunyima mavuno Ila imekupa mbegu just use it .

Then hawa watu ambao wapo Kari u yako jaribu kuwafanya kuwa mabalozi wako wa kukusemea .

Kukosa hela inaweza kuwa kawaida Ila kukosa mchongo wowote hii maana yake hauna watu.
 
Exactly. Naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom