Nimekutana na rafiki yangu mwarabu tuliesoma shule ya Msingi, Nasikitika kuona wageni wanavyotajirika huku wenyeji tumeridhika na vimafanikio vidogo

Nimekutana na rafiki yangu mwarabu tuliesoma shule ya Msingi, Nasikitika kuona wageni wanavyotajirika huku wenyeji tumeridhika na vimafanikio vidogo

Suala la kufanya biashara kwa wakuja sio jambo geni duniani
Kila nchi utakuta wenye asili ya hapo wanaburuzwa kwenye uchumi unajua kwa nini?

Kwa sababu wahamiaji wanapokuja kwenye nchi yoyote hawawezi kujihusisha na kazi za serikali kwa sababu hawawezi kwa sababu sio wazawa na wanahitaji hela za haraka, hapo ni lazima wafanye biashara tu hakuna kingine

Awe Irishman huko 🇺🇸 au Msomali Nairobi wao ni biashara tu maana hata mda wa kuimba wimbo wa Taifa hana
Siasa hawawezi kuingia labda wawe ni generation ya Tatu tena mmoja katika milioni
Hapo ni kuwaiga na kupata mbinu zao na sio kuwa na jicho la husda
Tumia mfano huo huo kwa wabongo nje ya nchi
 
Tumia mfano huo huo kwa wabongo nje ya nchi
Itawachukua generation 4 au tano kufika huko labda kwa elimu na kufanya kazi zenye malipo makubwa lakini kwa biashara ni wachache sana

Huu sio mfano bali ni ukweli yaani wachache sana kufika mbali
Ni kupambana na kuweka akiba kubwa ili kuendeleza biashara idumu na ikuwe kwa miaka na miaka hata wajukuu waje kuikuta
 
Wangoni waliopo hapa hawana ndugu wala hawajui asili yao tena huko SA ILA wahindi wa hapa unaowahita watanzania haswa kuliko wabantu, wanarudi INDIA kila mara!

Ni nadra kusikia majumba yale ni ya wahindi ila waarabu; wanajenga INDIA na huwasikii wakilalama kuhusu URAIA PACHA.

Unajiuliza kwanini wanafanikiwa, masikini wa kihindi au kiarabu, ni sawa tu na masikini mmakonde, hatoboi hata iwaje?

Hebu tafuta watu wa ukoo wa akina Mareale, kisha linganisha umasikini na utajiri kwao, unadhani ni kwasababu ya rangi? Ni ukoo uliotajirika kitambo sana, kutoboa kwao ni lazima. Same applies to hao Arabs na Asians, walichukuliwa kama binadamu grade 2, 3, wakapewa fursa hivyo enzi hizo za ukoloni, wakafuata akina Mareale(chiefs) etc.

Unadhani wakina Kikwete, Nyerere, Sykes, Salim walitokea tu from nowhere kama Magu?
wahindi waliopo hapa ukiwachukua na kwenda kuwadondosha india hawana hata pa kwenda. kama wanapo basi wamenunua tu siku hizi. hao walikuja karne nyingi sana kabla ya wangoni hawajaja. wangoni hawajaja zamani sana, miaka ya 1800 juzi tu hapa wakati wahindi karne za nyuma kabisa. katiba ya Tanzania inamtambua mtu kuwa mtanzania (hata kama angekuwa mzungu) kama alikuwepo kabla ya uhuru kutangazwa 1961, na wengine waliozaliwa hapo baadaye au walioupata utanzania kisheria.
 
Then kutoboa MAISHA ni kuwa na ramani sahihi za kufika Sehemu husika haina haja ya kulalamika mambo ya kupita haya


MAFANIKIO au PESA kila mtu anaweza kuzipata sio lazima tupewe backup na mtu kikubwa kuwa na MAARIFA tu.


Then hata hao tunaowaona wapo financially stable ni umasikini tu ndo unatufanya tuone Kuna Gap ila tukikaza tunafika popote .

Sisi watu weusi Ni watu wa kulalamika then tukipewa Kazi tunaiba na kudharu walio chini we need to Fuc**y our Ego
Dah kwel man
 
Umleavyo mtoto ndo jinsi akuavyo,kuna makabira ya wafugaji,wakulima,wachongaji vinyago,wavuvi ,wafanya biashara nk

Sasa wewe umekulia katika jamii ya watu gani.
Hapa duniani mara nyingi mambo ni kucopy na kupasate
 
Bongo nchi yangu kwenye familia kila mtu anataka yeye awe ndio aonekane ana hela kuliko wengine huyu atamsupport mwenzake saa ngapi ndio kwanza anamtoa kafara kama sio kumloga😅
 
Binafsi nimesoma na waarabu, yaani wenzio wanapelekwa shule wajue kusoma na hesabu basi,

Yaani wakitoka shule saa nane wanakaa dukani kuuza, nyie waswahili si hamuwakabidhi wenu mnaogopa mtoto ataiba Pipi.

Niliosoma nao waliishia darasa la saba na kukabidhiwa maduka kuuza/kufanya biashara, now kuna limoja lina miliki sheli.
Mtoto ataiba pipi 😂🤣
 
Ndyo[emoji23][emoji23]
Mzazi anajiona kapatia kumbe ana jikaanga kwa mafuta yake mwenyewe 😄
Na hili la waarabu nimelishuhudia pia wanaishia f4 moja kwa moja kusimamia kituo cha mafuta
Ukitafakari unaona linawezekana maana kununua na kuuza mafuta tu kwan lazm uwe na masters 🥴
 
waarabu na wahindi wa Tanzania, sio wageni, ni kabila la wahindi na waarabu tu ambao ni watanzania, na wengine ni watanzania kuliko hata wewe mwenye kabila la kibantu kwasababu wazazi wao wamekuja hapa miaka ya 1700 uko wakati wangoni wamekuja bongo miaka ya 1800 au 1900 kama sikosei. usiseme watu ni wageni kwa sababu ya rangi.
hapa kwetu ubaguzi wa rangi ni kawaida tena ukiwa mwarabu utanyanyasika sana
 
Kanuni za Asili ndo wahindi na wazungu hutumia that is way they are on top
Unapotoa hata Kama kidogo ukitoa kwa menye uhitaji lazima uongeze mara dufu.

Wahindi huwa wanatoa kwa Masikini ombaomba Hawa jamaa katika Ulimwengu wa roho wapo vizuri Sana.
Hawa jamaa ni kweli kwenye utoaji aisee
Kuna siku binafsi na wenzangu tulienda pale mburahati kituo cha kulea wasiojiweza
Aisee misaada mingi pale inatoka jamii ya wahindi yule dada wa pale alitueleza kuna mmoja jioni lazima apeleke misosi pale
 
Then kutoboa MAISHA ni kuwa na ramani sahihi za kufika Sehemu husika haina haja ya kulalamika mambo ya kupita haya


MAFANIKIO au PESA kila mtu anaweza kuzipata sio lazima tupewe backup na mtu kikubwa kuwa na MAARIFA tu.


Then hata hao tunaowaona wapo financially stable ni umasikini tu ndo unatufanya tuone Kuna Gap ila tukikaza tunafika popote .

Sisi watu weusi Ni watu wa kulalamika then tukipewa Kazi tunaiba na kudharu walio chini we need to Fuc**y our Ego
Shout out to you, this is among the best comment in 2023 DR HAYA LAND 🙏💪💪
 
Back
Top Bottom