Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Wanawake hivi kwenye maisha huwa mnataka vitu gani hasa???
Mimi ninayemuona mpumbavu ni huyo mzee, huwezi kufanya heavy investment namna hiyo kwa mchepuko, bora hata angekuwa amezaa naye hapo Sawa mtoto wake angenufaika in future. Na unaweza kukuta mkewe wa ndoa hajampa zawadi ya nyumba na Gari kwa Jina lake.. Sasa subiri huyo mchepuko aolewe unaweza kusikia mzee kapata stroke au mzee kaua akaishia jela au mzee kauwawa na huyo Kijana wa mpya wa mchepuko.
 
Baada ya kujengewa nyumba,kununuliwa gari na kutafutiwa kazi.Sasa una kila kitu saivi ndo unaona anakubana.

Dada kama unataka kutoka clean kwenye hayo mahusiano

Atleast usinyongwe na ubaki na uwahi wako

Mambo mawili hayakwepeki
1.kurudisha nyumba ya watu
2.kurudisha gari ya watu

Sasa swali langu ni upo tyr kuachiwa nini na nini alichokupa ili uwe huru na maisha yako.Ukiweza kujibu hilo then nitajua nianzie wapi kukushauri

Otherwise wewe ni limbukeni mwingine uliyeinuliwa kimaisha na kuanza kuona aliyekuinua ni mjinga na hilo litaku cost sababu mtu unaye deal nae kwa jinsi navyomuona ni wale type za kupenda sana na hao ndo kutoa roho ya mtu ni sekunde tu

Be careful mbwa wewe
 
Akiamua kumloga jee?
 
Kwa ninavyojua mkewe atataka arudishe vitu vyote hasa nyumba na gari.
 
Chagua moja kati ya haya:
1) Mwambie umepima ukakutwa +ve, hapo nae atataka akapime na akikutwa - ve anakuacha kiroho safi.
2) Mlengeshe kwa shosti yako ambae unaona anam feel.
Hata mdogo wako wee mwachie tuu aruke nae maana tayari ni mbwai acha iwe mbwai.. Ili upate sababu ya kuachana nae
3) Rudisha nyumba, gari, fenitures, hama unapoishi, acha hiyo kazi aliyokutafutia na uvunje mahusiano
Na ukaanze maisha mapya (uhamie) kwa huyo mumeo mtarajiwa.
4) mweleze kuwa unahitaji kuolewa ila atabakia kuwa mchepuko wa kudumu
 
Pole sana binti kutoka kwenye mahusiano ya hivyo ni ngumu,maana hakuna mjinga atayewekeza vitu vyote hivyo alafu akubali kukuacha,yaani wewe kwake ni mchepuko wa kudumu,
Labda kwakujaribu ni kuamua kumrudishia kila kilicho chake,na mbaya zaidi huwezi kukubali kurudisha mali zake urudi zero

N.B wadada mwisho wa kudanga ni 27 years udangaji wenyewe ni udange kwa akili yaani unapata hela huko unaweka assets zako kimtindo wako lakini kama mwanaume anakujengea,anakununulia gari na vitu vingine usidhani ni rahisi kukuacha salama we sio binti yake et anakujengea afu badae ukaolewe na mwanaume mwingine
Danga ukijua badae nawe unataka kuwa na familia yako,sasa hapo ni akili kumkichwa
 
Kama unaweza tafuta no ya uyo mke wake alafu umtumie pics zenu( wewe pamoja na mmewe) kwa kutumia new no afu usikilizie [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mmh huu ushaur hapana
 
Kwa ninavyojua mkewe atataka arudishe vitu vyote hasa nyumba na gari.
ndio unatakiwa urudishe viende kwa mwenye navyo, hapo wewe ni mwizi kama wezi wengine tu, na ni mwizi anayejua anachokifanya, na Mungu anakuona. kifupi ni kwamba ukifa leo hii moja kwa moja jehanum na hizo mali utaziacha. tafuta kutengeneza maisha ya baadaye haya mengine ya hapa ni ya kupita, shetani amekuwekea hook/ndoana ya wizi wa ndoa na mali za watu ili atakapokuvua hata usitarajie, mkaungane naye motoni. upo kwenye wimbi la hatari ya milele, stuka na gauka ghafla kabla wakati wako haujaisha hapa duniani.
 


Mmnh hapo umelazimisha kupendwa!
 
Kwa nini usiolewe mke wa pili? Hivi unaujua uchungu wa kumchuna vyote hivyo halafu umuache? Hivi hujawahi kusikia matukio ya watu kuuana kwa sababu ya wivu wa kimapenzi? Fikiria kabla ya kutenda. Huo ndio ushauri wangu.


Hata kama hampendi? Je dini yake inaruhusu?

N.k.

Halafu mke original atakubaliana na uke wenza?

Akiamua kuondoka zake ?!
 
Ushauri wangu kama kakufanyia yote hayo na ukaridhika mzalie mtoto/watoto najua unataka uwe na mwenza wako akuoe lakini unaweza ukamuacha na ukajikuta unaangukia Kwa Jamaa akakumega na asikuoe na hapo wanaokutaka wote wanaona Kwa vile unagari na maisha Fulani mazuri, nakushauri endelea nae mpe moyo wako wote kama ni kwenda kwenu akajitambulishe mwambie
 


Sasa kama moyoni hampendi na wala hisia naye hana afanyeje ?

Iwapo akiwa naye raha ya nafsi haipati afanyeje?
 

Kwetu tayari wanamfahamu ila hawajui kama ni mume wa mtu.
 


Awe single mother?

Aweke doa kwenye ndoa ya huyo jamaa ?
 
Awe single mother?

Aweke doa kwenye ndoa ya huyo jamaa ?
Kwani wakati anakula malinzake hakumjua kuwa ni mume wa mtu? Mwanaume awekeze Kwa mwanamke hafu baada ya kuwezeshwa ajifanye hamtaki kama ni mm sikuachi salama ni zarau sana Bora ungenikataa mapema kabisa au ungempa Condition Ili na mm asijitoe sana kumsaidia
 
Siku zote Kaa ukijua Kila jambo unalofanya ni mbegu. Liwe zuri au baya. Haya uliyoyafanya ni makosa na tayari umeshajua. Ni heri ukafanya jambo sahihi la kutoka kuliko kuendelea kuharibu ndoa ya mwenzako.

Mbegu nzuri huzaa sana. Tendo zuri Lina matunda na baya Lina matunda vile vile. Machozi anayolia mwanamke kama wewe sio mazuri yasije yakaja kukugharimisha.

Acha vyote Anza upya hutakufa. Vyote hivi ni ubatili. Ni heri chako Cha amani kuliko Cha wizi, dhulma(umemdhulumu mwenzio upendo wa mume wake)..and you knew it...the greens zikakuvuta. Just leave him Anza upya.
Usiendelee kuharibu..tengeneza maisha yako mapya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…