Nimelitathimini jengo la Makao Makuu ya CHADEMA pale Ufipa na nimeridhika chama hicho hakijali Maendeleo ya Vitu

Nimelitathimini jengo la Makao Makuu ya CHADEMA pale Ufipa na nimeridhika chama hicho hakijali Maendeleo ya Vitu

Makao makuu ya Chadema yapo mtaa wa UFIPA, wilaya ya Kinondoni mkoa DSM. Ukiwa na Kawawa Road, ukivuka Chuo kikuu huria kutokea Moroko unachepuka kushoto unasonga mbele katika barabara mbovu hadi unafika nyumba ya makazi ilyopo uchochoroni mtaa wa Ufipa. Nyumba hii ni ya kawaida iliyojengwa zamani kwa maana hiyo ni nyumba ya kizamani ikimilikiwa na familia ya familia ya mmoja wa waasisi wa Chadema Bob Makani. CHADEMA wamepanga hapo.

Kwa ujumla hata ofisi nyingi za CCM Wilaya kama sio zote ni nzuri na bora kushinda makao makuu ya Chadema.

Sabodo aliwapa Cinemax pale kituo cha ITV wafanye makao makuu na kuwapatia pesa za kuchimba visima lakini kuna ubadhilifu mkubwa wa pesa hizo ulifanyika na Sabodo akaghairi kila kitu.

Mpaka sasa CHADEMA inajinasibu kushika dola, inaomba waTanzania waiamini na kuipa dhamana ya kujenga nchi. Kwa miaka zaidi ya 20 chadema kikiwa chama cha kawaida hadi kuwa chama kikuu cha upinzani kikipokea ruzuku kubwa kimeshindwa kujenga ofisi ya makao makuu. Je, inawezekana kikaaminiwa na waTanzania kujenga nchi?

Hakika kwa namna CHADEMA inavyoongozwa, hilo pekee la kushindwa kuwa na ofisi ya makao makuu jkatika jengo wanalomiliki ni ishara tosha hakiwezi kujisimamia na viongozi wake kukosa maono hivyo kukosa sifa za kuongoza nchi. Kinaweza vipi kujenga uchumi wa nchi ikiwa wao kama chama wameshindwa kupanga, kuratibu, na kusimamia rasilimali zao ili kujenga japo jengo la ofisi kuu angalau nyumba ya chini kama walipopanga kwa zaidi ya miaka 20. Nyumba hiyo isingegharimu zaidi ya million 200. Lakini kwa sababu ya tamaa za viongozi na kuigeuza chadema kitega uchumi imeshindikana kuwa na jengo la ofisi kuu.

Sasa hawa watu wataweza kweli kujenga uchumi wa nchi? Watauza kila kitu na kukausha hazina yetu hakuna watakachofanya kwani hawana maono watageuza nchi Saccos yao
Huo ujumbe mpe meko ajenge makao ya ccm chato
 
Sasa huyo mropkaji wenu anamfikia hata robo Lowasa ?

Nimekwambia safari hii Chadema tutawafundisha nini maana ya Uchaguzi milipata kiburi kwa kivuli cha Lowasa

Huu ndio mwaka mtakaousimulia
mataga safari hii mtataga
 
Rudia kusoma maneno yangu ! Safari hii tutawafundisha maana ya Uchaguzi

Mlilelewa kama yai mkajivika kiburi hiyo chance hamtaipata tena
nyie tayari somo limeshawaingia kweri-kweri ndiyo maana mnaenda hadi kumuamsha kikongwe Mama Maria Nyerere hadi akawavua nguo ya ndani mchana kweupe 🤣 🤣 🤣
 
Tatizo kila mwenye jengo anaogopa kumkodishia chadema jengo kwa ajili ya ofisi kwa kuogopa fitna za serikali

Nina mfano halisi, Chadema walitaka kukodisha jengo zima la mtu fulani pale maeneo ya kijitonyama, mwenye jengo alikua na shida kweli ya pesa lakini alipoambiwa mpangaji ni chadema akasema serikali haitoniacha ngoja jibaki na shida zangu
Kwa nini msijenge ofisi? Mbona michango na misaada ya chama rafiki toka jeremani ni mabil ya shilingi. Mbona ruzuku kibao mmeitafuna kama kitimoto! Si ingetosha kushusha mjengo wa maana.
 
Kama milioni Mia tano inajjenga kituo cha afya, inashindikana nini chadema kujenga jengo lake yenyewe iii asipatikane mtu wa kuogopa kukodisha wakati wanpata ruzuku nyingi?
Michango ya wanachama kujenga jengo imeshindikana?
Chadema hawajui nini wanongea hata lisu hajui anongea nini bali akiingia kwenye mtandao anatazama washabiki wao wnasemje kisha ndo ataongea kwenye mkutano kesho yake.

Hata ilani yao inatokana na maoni ya washabiki wa chadema na sio mahitaji ya mtanzania.
 
Kwa hiyo wakishinda uchaguzi huu tutegemee miradi yote inayoendelea nchini ile ya "maendeleo ya vitu" kutelekezwa halafu tunahamia kwenye "maendeleo ya watu" ya ujenzi wa masoko ya usiku?

Ikitokea basi tutashuhudia nchi ya ajabu sana chini ya jua.
 
Kama milioni Mia tano inajjenga kituo cha afya, inashindikana nini chadema kujenga jengo lake yenyewe iii asipatikane mtu wa kuogopa kukodisha wakati wanpata ruzuku nyingi?
Michango ya wanachama kujenga jengo imeshindikana?
Chadema hawajui nini wanongea hata lisu hajui anongea nini bali akiingia kwenye mtandao anatazama washabiki wao wnasemje kisha ndo ataongea kwenye mkutano kesho yake.

Hata ilani yao inatokana na maoni ya washabiki wa chadema na sio mahitaji ya mtanzania.
Kama mmeweza kuchoma ofisi za chadema za kanda kwa kuogopa moto wa Lissu, vipi wangekua wamejenga jengo lao wenyewe, si mngelipua kabisa mseme ni magaidi wamelipua

Hata hicho kibali cha ujenzi sidhani kama serikali hii inaweza kuwapa,itakua ni figisu mwamzo mwisho

Subiri tuchukue nchi October tutashusha ofisi nzuri kuliko ikulu ya chattle[emoji6]
 
Kwa nini msijenge ofisi? Mbona michango na misaada ya chama rafiki toka jeremani ni mabil ya shilingi. Mbona ruzuku kibao mmeitafuna kama kitimoto! Si ingetosha kushusha mjengo wa maana.
Jeremani ndio wapi huko mkuu, vipi ulipokea hito michango toka huko jeremani? Na ulisaidia kutafuna hiyo michango kama kitimoto? Mataga bana
 
Ile ni nyumba ya makuti tu,mbowe anaswaga 326m za ruzuku kila mwezi plus michango ya wabunge wa chadema,kujenga ofisi hata yenye ukubwa wa banda la kuku imeshindikana 😃😃😃
Kwani nyumba ya Ufipa wanapanga?
 
Watanyimwa kibali au hata wakishajenga wataambiwa ni ipen space or either baada ya kujenfa wakapitisha greda kwa madai kuwa wanapanua barabara
Mmmh! umezidisha mahaba na wewe, angalia unavoongea pumba sasa.
 
Ungeenda ubalozi wa China uwaombe waisaidie Chadema kujenga majengo ya chama kama inavyofanya kwa CCM
Mara kadhaa viongozi wa CHADEMA wamesikika wakinadi maendeleo ya watu badala ya vitu. Na wakati mwingine wameibeza CCM kwa kujikita kwenye maendeleo ya vitu ( miundombinu)...
 
umewahi ona ofisi za jubilee chama tawala pale Kenya?...wana ofisi mbovu kuliko za cdm lakini wameaminiwa na wananchi
 
Tatizo kila mwenye jengo anaogopa kumkodishia chadema jengo kwa ajili ya ofisi kwa kuogopa fitna za serikali

Nina mfano halisi, Chadema walitaka kukodisha jengo zima la mtu fulani pale maeneo ya kijitonyama, mwenye jengo alikua na shida kweli ya pesa lakini alipoambiwa mpangaji ni chadema akasema serikali haitoniacha ngoja jibaki na shida zangu
Kwani haiwezekani wanunue eneo na kujenga jengo la ofisi makao makuu
 
Jeremani ndio wapi huko mkuu, vipi ulipokea hito michango toka huko jeremani? Na ulisaidia kutafuna hiyo michango kama kitimoto? Mataga bana
Kwa hiyo ulitaka niseme Germany ndio unielewe? Mlikula michango na ruzuku,na misaada toka Germany.
 
Back
Top Bottom