Mimi nikijana nna miaka 27, mwezi wa 1 mwaka huu 2026 nilikutana na bint nikampenda tukaanzisa uhusiano lakini katika muda wote niliyokua nae zaidi ya miezi 7 sijaai kukutana nae kimwili, sababu anaesema yy ni bikra anataka mpk akiolewa ndio afanye akiwa ndani ya ndoa, hila nna muhudumia anachotaka kwani mm nimeajiliwa hila yy kamaliza uhasibu degree hila hajapata ajira bado,sasa weekend hii nilikua nna ahadi nae twende sehemu tukakae tule hila sikumwambia sehemu gani tunayotaka kwenda, lakini akatoa excuse ana matatizo ya kifamily hatotoka,mimi nikampigia simu jamaa yangu tukaenda hyo sehemu cha ajabu tulipofika hyo seemu nikamkuta yy yupo na jamaa mwengine anakula anakunywa, hakuniona na sijamshtua nikakaa mpk nikaondoka sikumshtua, ukizinatia nishapeleka mpk barua na mahali nilipanga kupeleka mwezi huu wa tisa ,usiku nikampigia simu nikamwambia nilipomuona lakini anakataa sio yy lakini mwisho akakubali hila akasema yule ni mume dada yake alikua na kikao akaomba msamaha,nilikua nnaomba ushauri jamani nisamehe tu tuendelee na mipango ya ndoa ukizingatia nishawambia nyumbani mpk tarehe ya kupeleka posa ,naombeni ushauri wenu jamani hii issue imenikalia vibaya maana ndugu ikifika ijumaa taree 2/10/2026 wanaanza kuja kwa ajili ya kupeleka mahali nifanyaje ?nivunje mipango yote au nisamehe maana kinachoniuma zaidi mimi nimekomaliwa miezi kibao kumbe wengine wanakula tu mzigo