Nimemgombeza askari wa usalama barabarani, wenzake wameniomba msamaha

Nimemgombeza askari wa usalama barabarani, wenzake wameniomba msamaha

Gulwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2008
Posts
10,597
Reaction score
16,394
Ni kituo cha mabasi cha mawasiliano. Wako maaskari wengi lango wa kuingilia, kila gari linaloingia linasimamishwa na kuchukua hela kwa konda. Bahati nzuri nikashuhudia askari wa kike akipokea hela, nikamfuata na kumweleza nichokiona, akanijibu vibaya.

Nikatishia kuchukulia hatua zaidi lakini wenzake wa kiume wakaniomba msamaha. Hili jeshi limeoza kabisa.
 
Hilo nalo ni jeshi? Jeshi gani lisilozingatia maadili na sheria! Hata wao huwa wakiowaona wanajeshi wanataharuki na kujiadabisha. Kwa sasa Tanzania Polisi siyo jeshi ni genge tu lenye wahuni wanatenda uovu wakiwa na magwanda. It is sad we have bet our lifes to these hooligans!

Kimsingi raia huwa wanaogopa magwanda tu maana kumpiga polisi akiwa na vazi la serikali unaweza ukageuziwa kibao.
 
Kwa asubuhi hii hiyo inaitwa ya chai, baadae mchana watatafuta ya lunch, na jioni watatafuta ya chakula cha usiku.

Mishahara yao wanajengea tu mijumba.
Hao hawawezi hata kujenga banda la kuku kwa kupitia mshahara labda wachuke mkopo.
 
Kwa jinsi jeshi la polisi linavyo jidharaulisha ndio maana hata Sungusungu/ polisijamii nao sasa wanavaa uniform zao
 
Hyo mbona Kawaida mkuu,mm naonaa hvyo Kila day nasina Cha kufanyaa,yaan Hadi cku Moja nikapiga picha kbs lkn wahiiii naonaa Kila mbuzi anakula Kwa urefu wa kamba zakee
 
Mkuu ungemuacha tu, hao ni dagaa tu a mbao wanachukua 2000 na wengine 5000 ambazo haziwewi kiathiri sana.

Wanaotuumiza ni ma papa ambao wametajwa kwenye ripoti ya CAG kama vile upotevu wa trillioni moja ya tanrod, matumizi makubwa ya mama kwenda dubai na kulipa mabilioni ya pesa huku watz tunataabika na miundombinu mibovu nchi nzima.
 
Bora wao wanaomba wanapewa kuliko wale wanaopiga mabilioni chini ya serikali ya samia. Huyo askari umemuonea tu.
Hili nalo jinga kabisa ! Unasaport rushwa? Unajua nin kinafuata hapo baada ya kumnyima? Lkn pia ukitazama riport ya cag wezi wote waliotajwa wanatokea sukuma gang! Kaka mkuu ni masanja kadogosa!
 
Hili nalo jinga kabisa ! Unasaport rushwa? Unajua nin kinafuata hapo baada ya kumnyima? Lkn pia ukitazama riport ya cag wezi wote waliotajwa wanatokea sukuma gang! Kaka mkuu ni masanja kadogosa!
Sijui hujaelewa nini we bata. Nimekuambia kaomba. Kwani umeambiwa kamkata mtu kisha anachukua rushwa? We unawashwa kweli nyuma hukk. Na tunapoenda tutahakikisha wanaowakuna tunawamaliza
 
Ni kituo cha mabasi cha mawasiliano. Wako maaskari wengi lango wa kuingilia, kila gari linaloingia linasimamishwa na kuchukua hela kwa konda. Bahati nzuri nikashuhudia askari wa kike akipokea hela, nikamfuata na kumweleza nichokiona, akanijibu vibaya. Nikatishia kuchukulia hatua zaidi lakini wenzake wa kiume wakaniomba msamaha. Hili jeshi limeoza kabisa
Watumishi wa chini Sasa hivi wote Wana hasira sana baada report ya CAG kutoka,nao wameaamua kula kwa urefu wa kamba yao,liwalo na liwe!!
 
Screenshot_20230330_094039_Twitter~2.jpg
 
Back
Top Bottom