Nimemgombeza askari wa usalama barabarani, wenzake wameniomba msamaha

Kama ni Kwa asubuhi hilo limezoeleka ukishatoa hiyo husumbuliwi Tena labda ufanye makosa ya mengine Kila daradara ndivo ilivyo
 
Ni kituo cha mabasi cha mawasiliano. Wako maaskari wengi lango wa kuingilia, kila gari linaloingia linasimamishwa na kuchukua hela kwa konda. Bahati nzuri nikashuhudia askari wa kike akipokea hela, nikamfuata na kumweleza nichokiona, akanijibu vibaya.

Nikatishia kuchukulia hatua zaidi lakini wenzake wa kiume wakaniomba msamaha. Hili jeshi limeoza kabisa.
acha tuwape we inakuuma nini, bora kutoa elf 2 kuliko fine ya elf 60, hamna daladala lililokamilika 100%, hiyo haiitwi rushwa hiyo mlishaambiwa ni yakubrashia viatu, huwezi kumpeleka popote boya wewe, hiyo chain ya mgao ni mkubwa kuliko kichwa chako kibovu
 
Bora wao wanaomba wanapewa kuliko wale wanaopiga mabilioni chini ya serikali ya samia. Huyo askari umemuonea tu.
Naunga mkono hoja yako 💯. Hivi vielfu elfu ni vioffer offer tu vya kawaida tunavyopeana peana hata huko mitaani ! Na wala havina madhara makubwa kwa Taifa !! Tupige makelele kwa mabilioni yetu yanayopigwa kila kukicha Wajameni msituhamishie magoli !! Hivi vipesa vya supu na kiwi ni bure tu hata kuviongelea !!
 
Ni kote kila sehemu huu mchezo unapigwa sana ni kama SHERIA!!!!
 
Wee bibi mlinda legacy una taabu san au kwakua JPM aliruhusu rushwa kwa hao jamaa na kusema ni kwaajil ya ku brush daluga? Rusha ni rushwa haimaanishi iwe trln au buku yote ni rushwa!!
Rushwa unaithibitishaje we mama? Au unaongea tu kama shimo la maji taka?
 
Masikini 🤣🤣na hapa umefoka na kutumia akili zote mpaka ya akiba!! Still ni pointless!! Mtoa mada kasema waz ameshuhudia Askari wa usalama barabaran akichukua rushwa toka kwa konda. Kitu ambacho ni uvunjaji wa sheria mtoaji na mpokeaji!! Ukitaka uthibitishiweje?? Tatizo lenu mpo very upset, kubalin matokeo and let life goes on...
 
Unamgombeza anayechukua elfu 2 ila unampigia kura na kumwita mh. Anayekuibia trilioni 1.2 na kuongeza gharama kwenye invoice.
 
Ni kituo cha mabasi cha mawasiliano. Wako maaskari wengi lango wa kuingilia, kila gari linaloingia linasimamishwa na kuchukua hela kwa konda. Bahati nzuri nikashuhudia askari wa kike akipokea hela, nikamfuata na kumweleza nichokiona, akanijibu vibaya.

Nikatishia kuchukulia hatua zaidi lakini wenzake wa kiume wakaniomba msamaha. Hili jeshi limeoza kabisa.
Uliyemfokea ndiye anayepaswa kucbunguza na kuchukua hatua dhidi ya waliopita na pesa zilizoonekana kwenye screens za CAG.

Nchi ipo pabaya hii
 
acha tuwape we inakuuma nini, bora kutoa elf 2 kuliko fine ya elf 60, hamna daladala lililokamilika 100%, hiyo haiitwi rushwa hiyo mlishaambiwa ni yakubrashia viatu, huwezi kumpeleka popote boya wewe, hiyo chain ya mgao ni mkubwa kuliko kichwa chako kibovu
Wewe inaonekana unatumika kinyume
 
Ni kituo cha mabasi cha mawasiliano. Wako maaskari wengi lango wa kuingilia, kila gari linaloingia linasimamishwa na kuchukua hela kwa konda. Bahati nzuri nikashuhudia askari wa kike akipokea hela, nikamfuata na kumweleza nichokiona, akanijibu vibaya.

Nikatishia kuchukulia hatua zaidi lakini wenzake wa kiume wakaniomba msamaha. Hili jeshi limeoza kabisa.
Hongera kwa ushujaa huo Mkuu.

Ila sema maslahi yao nayo ni duni sana.
 
Back
Top Bottom