Nimemgombeza askari wa usalama barabarani, wenzake wameniomba msamaha

Angekuwepo Magufuli lupango ilikuwa halali yako kwa kumugombeza askari kwa kuchukua hela ya kiwi.
 
Mkuu hiyo hela ni ya kubrush viatu! Ukisikia mishahara yao utaona huruma.
 
Ungempiga picha akichukua rushwa
 
Nchi imejaa majangili tupu
 
Shukuru sana mkuu 'Gulwa', bahati yako nzuri hukuumizwa kwenye mkasa huo.

Nchi inaoza tukiiangalia kwa macho yetu sisi wenyewe!
 
Kuna siku nilikwenda kwenye ATM ya CRDB kutoa pesa nadhani ilikuwa siku ya Jumamosi, nilitoa pesa kwenye ATM mara 3, huo muda nilikuwa peke yangu kwenye kutoa pesa kwenye mashine ya ATM.

Sasa wakati nataka kutoka, ndani ya zilipo Mashine za ATM pembeni pana kijumba wnakaa Askari Polisi, walikuwa 2 wa kike na wa kiume.

Yule askari wa kiume ambaye alikuwa na silaha akaniita akaniomba pesa kwa ajili ya kupata chochote mchana, basi nikatoa 5,000 nikampatia akashukuru nikaondoka zangu.

Askari Polisi hawa wa kawaida na trafiki nawachukia sona, wakiniomba pesa ama lifti uwa siwapi.

Kabla ya hiyo siku nilishafikiriaga nikaweka mtazamo wangu kama ikitokes natoa pesa kwenye ATM alafu askari aliyepo akaniomba pesa sitoweza kukataa sababu ya kiusalama uwezi fahamu hiyo siku yuko katika hali gani, mtu anayo salaha anaweza akakufanya chochote.
 
Kwa asubuhi hii hiyo inaitwa ya chai, baadae mchana watatafuta ya lunch, na jioni watatafuta ya chakula cha usiku.

Mishahara yao wanajengea tu mijumba.
Mh mijumba wakati kuna jamaa ni jirani yangu kabla sijanunua kiwanja yeye alishajenga ila mpka leo nimehamia kitambo kidogo yeye kaweka wavu madirishani nikikaa nae anajisifu ana ng'ombe wengi kanda ya ziwa ila haishi kuniomba hela muda mwingine mkewe anamuomba wife hadi mafuta ya kula. Hela za rushwa zinalaana na mwamba yupo mataa ya veta pale anawapuna boda hela zao kama zote. Ila hana cha maana anachofanya zaidi ya kunywa pombe.
 
Bora wao wanaomba wanapewa kuliko wale wanaopiga mabilioni chini ya serikali ya samia. Huyo askari umemuonea tu.
Lah, inabidi kukubaliana nawe katika hili.

Kwa kweli ni bora kabisa kwa hao wanaoomba, kwa sababu unayo hiari ya kukataa, hata kama utanyimwa haki yako kwa kutotaka kushiriki kwenye hujuma hiyo.
Hawa walioko huko serikalini, hata hawatupi nafasi ya kuwakatalia wasizoe mali zetu!
 
Sasa 2k kwa mwezi mzima si 60k na bado maisha yanakua hatarini kwa kuwa na gari mbovu barabarani. Inaeleweka rushwa sio leo wala kesho itaisha ila kuikemea ni jukumu letu.
 
Acheni kuyafanya maisha kuwa magumu kiasi hicho, sijaona haja ya wewe kubishana na huyo askari
Wewe na hao waliofurahia haya maneno yako ni polisi hao hao wabovu. Baada ya hapa mtakuwa mnaingia hata kwenye majumba ya watu na kuwapora mali zao, na bado utaona hakuna sababu ya kulalamikiwa majambazi nyie.
 
Mimi nimewagombeza Dstv na nimewaambia warudishe hela yangu niliyolipa.

Hovyo kabisa wanapandisha vifurushi na bei zao kandamizi sana wanyonyaji hawa
 
Ndio urefu wa kamba yake huo.
Si unasukia wengine wanajitwalia na T huko
 
Vijana mna masifa kweli kweli mkipata vi cheo kidogo tu basi ,sasa ulimgombeza Askari alikuomba wewe hiyo rushwa?
 
Kama ni Kwa asubuhi hilo limezoeleka ukishatoa hiyo husumbuliwi Tena labda ufanye makosa ya mengine Kila daradara ndivo ilivyo
Na huo ni mradi wa watu,wenyewe wapo wametulia tuli
Hao askari barabarani wanatumwa tu

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…