Imekukuta kama mimi, mimi namba ya siri ya mke wangu ya benki na SIM card zak zote nazijua vizuri tu, yeye hajui yangu ya benki ila za SIM zote anazo na wakati fulani huwa namtuma kutoa hela au kulipia vitu nikiwa busy.
Kuna siku sijui roho gani ilinituma kufungua app yake ya SIMBANKING nikaangalia salio nikakuta 8.4M (jamani hawa wenzetu wanatunza hela), nilishangaa sana kwasababu ni mtu wa kupenda kuomba hela kwa 70% ya matumizi yake na kiukweli hata mimi roho iliniuma bwana, ila niliamua kutulia kwakua sikuwa na namna ya kukisanua.
Baada ya miezi kadhaa kuna ugomvi ulitokea( wa kawaida tu) akawa anaomba msamaha ila nikawa navunga kama nimekasirika sana kumbe moyoni silichukulii hata kama ni kosa kubwa, hapo sasa likaja wazo la kumtoa hela kutokana na majuto yake, ghalfa tu nikamwambia nisaidie 1.5M kama unazo nimekwama sana.
Bila kuuliza ni za nini, aliuza tu atume kwenye namba gani na akatuma na wala hajawahi kuziomba.
Sema hanipi hela ila vitu vya ndani na mavyombo kila siku yanaongezeka, kwakweli simlaumu sana.