Binafsi Huwa ninafanyaga baadhi ya arguments na Mzee wangu, ambaye namshukuru Mungu kwa kumweka hai mpaka sasa. Huwa ananiambiaga kama kijana wake, mwanaume ni lazima uwe na high bar kwenye maswala ya kimaadili na hekima kama baba, mwanaume ni lazima awe na busara kwelikweli na uongozi usio na hitilafu na mwenye uwezo wa kufanya maamuzi yenye mantiki pasipo mabavu maana yeye ndo symbol ya familia nzima, Ili pale familia inapopata changamoto nzito na ngumu aweze kuwa kimbilio na source of wisdom, solution, and stability. Mwanaume akishakosa moral authority kwa kujihusisha na mambo ya hovyo atatengeneza instability ndani ya familia kupitia chaos either baina yake na mke wake au watoto, atadharaulika kutokana na uovyo wake na hakuna atayemsikiliza Wala kumheshimu Ikiwemo mbwa wake mwenyewe. Mwanaume akiwa mdokozi na mwenye makandokando ya kijinga Hana tofauti na kibaka wa mtaani. Baba ni lazima achape kazi kwelikweli Ili amtunze mke wake, wazazi wake,jamii inayomzunguka na watoto wake kwa juhudi na maarifa.