Nimempiga mke wangu milioni 2 kizembe sana

Kama ananunua vitu vya ndani, kukitokea dharura anasaidia kubeba pale ulipokwama, na ukikwama sana ukimuomba anakupa. Basi huyo hupaswi kumuuliza hata kama ana 80M kwenye account. Huyo ni mwenzako, tatizo lipo kwako huwa humshirikishi mkeo kwenye mipango ya maendeleo ya familia. Kwa maana nyingine ni matokeo ya baba kuwa mbinafsi
 
Mbona ulivyompa hio idea alitoa hela? Au ukimuuliza huwa anasema hana hela? Kukubali kutoa hela yake kununua shamba ameonesha Hana issue.
Afadhali wewe umekuja na hoja madhubuti. Tatizo limeanza pale ambapo mke anaumwa, mume anahangaika, pesa imeisha, anakopa huku na kule kwa ajili ya kumsaidia mke. Lkn mke kakalia hela kwenye akaunti!!! Hiyo ndio inastaajabisha...
 
Kama mke wako ni "Kigwasa" umefanya jambo zuri sana. Ila kwa wale tuliobahatika ambaye unaweza muomba hata 1M ukikwama akakugea sioni sababu ya kumchapa.
 
Umenena vyema sana. This is a matured mind. Umeweza linganisha vizuri sana mabadiliko ya nyakati. Watu wengi wanaleta mifano ya Saudi arabia ambako mwanamke hata kuendesha gari haruhusiwi. Huku kwetu mazingira hayo haya apply, jamii imetoa fursa sawa na zaidi sana mwanamke amepewa fursa zaidi hadi za upendeleo. Katika mazingira haya mke na mume wanapaswa kuwajibika kikamilifu kwa hali na mali zao ndani ya familia bila kuhitaji kukumbushwa.
 
Fact, ukweli na uwazi ndio wake zetu wanataka. Kama wewe mwenyewe unaficha ulichonacho, usitarajie mkeo awe muwazi kwako hata siku moja. Mimi binafsi huenda mke wangu ni muwazi kwangu kwasababu kila jambo tunalipanga pamoja na tunaenda pamoja katika kulitekeleza. Kila mali tunayonunua tunaandika majina yetu sote, zipo zingine namwandika yeye peke yake kwa ajili ya kumpa moyo kutokana na kujitoa kwake ndani ya familia. Mwanaume kuwa mkweli na muwazi ni nguzo muhimu katika kujenga familia ya mwili mmoja
 
Fact, umeeleza vyema sana. Mi naona familia ambazo mume na mke hawashirikiani na wanafichanafichana, chanzo chake kitakuwa ni familia walizolelewa zilikuwa na ubinafsi uliopindukia mipaka.
 
Exactly- The back stops with him.
 
Nawe ukamuibia mkeo 2m!
 
Hahahahah mke ambaye anaficha hela yake na kujidai mchungu sana hio ndio dawa yake. Kuna mwanamke unaweza kuwa on your dead end na hela anayo unajua kabisa ila hakupi huyo ni kumchapa tu.

Ila kama mke ni generous sio mchoyo ukihitaji support yake huyo kumuibia ni dhambi hata Mungu hafurahii. Kuna midemu mibinafsi bana we ila kwenye kula hela zako yuko mstari wa mbele kama tai.
 
Utetezi wa kijinga kabisa, kuna mwana namjua ana mke na watoto mkoa. Ila yuko bongo anagonga jimama flani ndio linamuweka mjini kistaa kabisa hizi 2-3M hazimpi shida kabisa.

Sio kwamba ni Marioo, jamaa ni lecturer chuo flani ila kama mnavyojua mshahara wa Lecturer hauwezi endesha maisha ya dar na mke mkoani.

Mke mkoa amenunuliwa Raum, jamaa ana premio mayai ila hela nyingi inatoka kwa jimama. Linalipa na kodi maeneo flani katikati ya mji kabisa limemuwekea na Harrier tako la nyani uwani.

Sasa kwa scenario hii utasema justification ya kuwa eti hujui hela ya mke imetoka wapi ina maana hela ya mwanaume kama huyu nae mke asiitumie sababu hajui imetokea wapi?
 
Kuna uzi humi ulishapita na kusema usimuonee huruma mwanamke never ever wanawake wengi ni wana roho ya kichawi na uselfish ni wachache sana ambao wako na roho ya utoaji panapo hitajika utoaji kwa mwanaume wake.
Wewe ni mimi haswaaaa siwezi kuwa na kopeshwa na mke wangu ina kua haina maana ya mke na mume sasa
 
UPENDO ndio nguzo muhimu katika ndoa.... upendo unajumuisha mambo ya msingi na ya kujenga taasisi ya ndoa....... Upendo unaokuza na kujenga ndoa unajumuisha juhudi za pande zote mbili na kila mmoja akijitoa kwa ajili ya huo Muunganiko.......

Unapotoweka upendo ndio huzaliwa ubinafsi......kwa kuwa upendo unajumuisha huruma, kujali, kuthamiana na kuthaminiana.........ubinafsi unazaa utengano wa nafsi na mwili na matokeo huzaa chuki..........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…