Utetezi wa kijinga kabisa, kuna mwana namjua ana mke na watoto mkoa. Ila yuko bongo anagonga jimama flani ndio linamuweka mjini kistaa kabisa hizi 2-3M hazimpi shida kabisa.
Sio kwamba ni Marioo, jamaa ni lecturer chuo flani ila kama mnavyojua mshahara wa Lecturer hauwezi endesha maisha ya dar na mke mkoani.
Mke mkoa amenunuliwa Raum, jamaa ana premio mayai ila hela nyingi inatoka kwa jimama. Linalipa na kodi maeneo flani katikati ya mji kabisa limemuwekea na Harrier tako la nyani uwani.
Sasa kwa scenario hii utasema justification ya kuwa eti hujui hela ya mke imetoka wapi ina maana hela ya mwanaume kama huyu nae mke asiitumie sababu hajui imetokea wapi?