Nimempiga mwizi mapanga mawili ya kichwa, akifa Mungu nisamehe

Ebwana niko zangu maskani hapa, masela kibao (wamataifa mbali mbali) wenye kuvuta wanavuta wenye kunye kunywa wanakunywa, wengine wana chafua kamali (hayo ni maisha yetu ya kila siku wachimbaji tusipo ingia porini) stori kubwa ni madini tu, jana kazi ilifanyika na machizi kibao wana machenji mfukoni.

Nimejaribu kusikilizia story ya yule ladrao (mwizi kireno) bado sija sikia watu kuzungumzia, labda kutokana hapa matukio kama haya ni ya kawaida tu.
Niongee ukweli, hapa kitu kufa sijui mtu kuumia sio novidade (sio mpya ki reno) hapa watu wanashindana migao tu (pesa baada ya kugawana)

Naendelea kufuatilia, ila kuna wazo la baadhi ya wadau hapo juu, nimeamua kulifanyia kazi.
Nategemea kutoa vitu vyangu vyote nipeleke kwa mchizi wangu, ifikapo saa saa kumi na mbili niingie zangu maporini nikajaribu bahati yangu maana walio ingia jana usiku wengi wamerudi na migao ya kibabe.
Tupo pamoja lolote nitawajulisha.
 
Kumuua MWIZI ni sawa na kumiliki BUNDUKI uswahili,,, maisha yako na wewe yako hatarini.
Mkuu usiwe na wasi, maisha yangu yenyewe tu ni ya hatari.
Fikiria, naingia chini ya shimo la chepe tisa, kumi na nne, mpaka kumi na sita.
Hapo bado natakiwa niingie ndani ya fonka (mwana ndani) iliyo tembea chepe mpaka sita kwenda kupiga mchanga (unao tembea na madini) unadhani shimo likijifukia nitatoka kweli?
Mkuu, sikuongopei, watu kila siku wanakufa, lakini wachimbaji kauli yetu ni moja tu, "kufa kulala, kaburi tuta".
Ukiachana na kufa, kuna jela.
Kumbuka hili pori ni la mwekezaji (mzungu kutoka marekani) kwahiyo ukikamatwa ni jela miezi kuanzia sita, mpaka mwaka mmoja, ukiwa na gundu mpaka miaka miwili.

Ebwana ee we acha tu.
 
Wenzake wanajua alipo uwawa jamaa yao hama hapo.
Natoa vitu vyangu napeleka kwa rafiki yangu anae kaa mtaa mwingine, me mwenyewe najipigilia machakani hata ikiwa week mbili, naimani yatakwisha tu.
Kwanza hapa kuuana sio habari ya mjini, nisawa na mtu kupakaa mafuta ya mgando kipindi hichi cha kipupwe.
 
Pole na Hongera kwa kumkomesha mwizi ila asife, Sasa ndio nimeelewa ule mwito wa Simon Sirro, Kuwa kila mtu awe na panga walau, BORA YAKO Umetii bila shuruti.
 
Jinga sana hawa, mwaka jana waliniamisha mtaa, baada ya kunisafisha kila kitu changu na kuniacha na nguo nilizo vaa mwilini tu.

Walinilaza kwenye mkeka week mbili kenge hawa.
pole mkuu nakumbuka ulileta na uzi humu
 
Upo Msumbiji?
 
Mshana umenifanya niwaze kuwa kwanini majambazi wakikubana wanakuua hawachukui kitu kumbe zana alizotumia ni dili.
Imenikumbusha nondo Mbeya.
 
Noma sana
 
Mwizi ninkuacha afe tu, wamewahi safisha geto langu enzi hizo na kuniachia ndala na mapazia tu, siwapendi wezi na wafage tu...nilianza upya kila kitu.
Mmh Acha tu.. Flat yangu inchi 32 mpya na godoro inchi 10..vyote havina hata miezi 3.
Na nilivinunua muda mfupi baada ya demu wangu kusafisha gheto geto lote.
Nikikumbuka NATETEMEKA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…