nameless girl
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 4,195
- 2,690
Aliyesema mwanaume msimamo hakukosea
Hama nchi hamia MalawiNimeteleza mkuu nipe ushauri
Iko hivi mkuu, huyu mzazi mwenzangu anaishi mkoa tofauti na mumewe. Huwa wanaonana weekends tu. Ikitokea mmoja ana safari za kikazi ama amebanwa na ratiba za kazini hata mwezi unapita bila ya kuonana.Mimba ya miezi miwili tu tayari mme ‘keshaikataa’ kivipi, basi ujue huyo demu kimeo na wala sio wewe tu.... hii chai umeleta kwa lengo la kuwachafua singo mama’s.
Maana yake nini hili? Binafsi sijawahi kuisikia mkuu, nafahamu "mwanaume mashine".Aliyesema mwanaume msimamo hakukosea
Mwanaume huwa halaumu wala kujimbwambafai bali huwa anatoa ushauriWanaume tunapungua kwa kasi sana, wavulana wanakuja kwa spidi isiyo ya kawaida.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kwani mimba kaibeba yeye???? Si anaikataaa tuuAkili uliyoitumia kumshawishi ndio hiyo hiyo itumie kuchukua maamuzi
Kwa hiyo sisi ndio tuumize kichwa kuwaza utafanyaje pambana na hali yako.
Kwa maneno yako hayo we ikubali tuTatizo nina damu Kali. Toto litafyatuka kama mm. Jeusiiii
Miaka 9 iliyopita nilimtia mimba Mwanachuo wa mwaka wa 2 akajifungua mtoto wa kiume. Hatukuweza kuoana maana na mimi ndiyo kwanza nilikuwa nina mwaka mmoja mtaani sina mbele wala nyuma.
Hivyo kila mtu alishika 50 zake na kutafuta mwenza wake mpya wa maisha. Lakini malezi ya mtoto niliyabeba kama baba.
Yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kumpata mwenza wake wa maisha. Alimpata miaka 7 iliyopita na sasa wana watoto 2 ndani ya ndoa yao
Mimi nilichelewa kidogo kwasababu ya kujipanga kimaisha, ndoa yangu ndiyo kwanza ina miaka 2 na nina mtoto wa miezi 7.
Miezi 2 iliyopita nilienda semina mahali fulani. Nikakutana na mzazi mwenzangu naye akiwa ni mshiriki wa semina ile. Kwa kuwa mke wangu ana katoto kachanga ka miezi 7, na kwakuwa huyu mzazi mwenzangu tumekutana mazingira mapya ya semina, na kwakuwa jicho lilimtamani kwa jinsi alivyo nawiri na kustawi basi semina ilienda vizuri.
Juzi nimepigiwa simu na mzazi mwenzangu akidai ana mimba yangu na mumewe amegoma kuikubali.
Sasa mabibi na mabwana, nawauliza suala hili nilishughulikie vipi?
Naombeni suluhisho la suala hili pasipo kuvuruga ndoa yangu changa.
- Nikubali ama niikatae mimba hii?
- Nikiikataa itakuwaje endapo mtoto atafanana na mm na mumewe anaijua chapa yangu kupitia mtoto wangu wa kwanza?
- Je, nikikubali mke wangu patakalika?