Nimemtia mimba mzazi mwenzangu akiwa kwenye ndoa yake ya miaka 7. Nifanye nini?

Mimba ya miezi miwili tu tayari mme ‘keshaikataa’ kivipi, basi ujue huyo demu kimeo na wala sio wewe tu.... hii chai umeleta kwa lengo la kuwachafua singo mama’s.
Iko hivi mkuu, huyu mzazi mwenzangu anaishi mkoa tofauti na mumewe. Huwa wanaonana weekends tu. Ikitokea mmoja ana safari za kikazi ama amebanwa na ratiba za kazini hata mwezi unapita bila ya kuonana.

Sasa yasemekana kabla ya mzazi mwenzangu kwenda semina alikuwa hajakutana na mumewe kwa mwezi na wiki moja. Ndiyo chanzo cha mumewe kuikataa mimba hii.
 
Du hapo sasa pagumu....amua lolote Kaka mie nmeshindwa kukusaidia
 
Ni vibaya sana kuishi bila kujua kusudi la maisha yako na kujiwekea malengo kulifikia na hili ndo chanzo cha wengi kukosa discipline katika maisha ya kawaida katika jamii.

Ukiwa na sababu ya kuishi na kuwa tayari kufanya lolote ili kuliishi huwezi fanya mambo ya ajabu kama haya na kuja kuyaanika huku ukitaka ushauri wa kila mmoja ambao nao huwajui.

Wanaume tunapungua kwa kasi sana, wavulana wanakuja kwa spidi isiyo ya kawaida.

Eeeh Mungu fungua fikra zetu sisi watoto wa kiume ili kutengeneza kizazi kitakachokupendeza, kwakuwa wanawake na watoto wote wanatuangalia sisi wakiume.
 
Pole zako, mzazi mwenzako yeye anasemaje juu ya hiyo issue?
 
Mimi nadhani ifike mahali wanandoa muamue kuwa wazi muishi pamoja na msichepukiane au muachane kilamtu awe huru
Hizi mambo zinaleta ukakasi sana, ugomvi na mauaji mengi ndani ya wanandoa
Tuwe wakweli kwa maslahi ya watoto na jamii
 
Wakati unaendesha semina chumbani ulikuja kutuuliza?

Ushauri mzuri utaupata kwa mkeo...
 
Siku hizi ile harufu ya mumeo hiisikii tena?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…