kuna siku utakamatika hapo, hata kunyanyua ulimi uongee hutaweza, hata kunyanyua mguu uende chooni hutaweza. utahitaji msaada wa wanadamu hautakuwepo, utahitaji msaada wa madoctor hautakuponya, utaanza mwenyewe kuhitaji watu waje hapohapo nyumbani waimbe mapambio na kukuombea kwa Mungu. nina ndugu yangu alikuwa kama wewe, alikuwa na pesa, mtu mkubwa serikalini huko, shetani alikuja kumletea ugonjwa, nilipomtembelea nilikuwa nakuta muda wote ameweka channel za mahubiri tu tena ya walokole, mtu wa kulala tu kitandani kila kitu hapohapo hata tv wamemsogezea karibu na kitanda, imefika mahali akawa anaamini labda uwepo wa channel ya kidini utatransfer uponyaji uje kwake. kiburi chooote kwisha.
hata wewe ni kwasababu u mzima, na unaamini huhitaji hayo mambo. nakuhakikishia kuna siku utaikumbuka hii thread na utakuja kuwashauri watu wengine wenye moyo kama wa kwako.
jambo lingine, kila mtu atauchukua msalaba wake mwenyewe, na atahojiwa mbele za Mungu kwa habari zake binafsi, mke hatachukua mzigo wa mume wala mume kuchukua mzigo wa mke wala wa watoto wake. hivyo acha kubana mke wako. kwanza inaonekana ulimkuta akiwa mwamini ukambadilisha ili afuate imani yako ya dini isiyo ya kuokoka. baada ya miaka 9 bado unamchagulia cha kuamini na namna ya kuamini. huo ni ukoloni, mwache asali anavyoamini, si ukute yeye akawa sahihi akaja kukusaidia, au akakuta imani tofauti huko akaja kukushauri kuwa usiende huko alikokuwa ameenda.
kitu pekee ambacho tunaweza kukubaliana mimi na wewe ni kuhusu manabii wa mafuta, hao hata mimi siwaamini hasa hao wanaobase zaidi kwenye mafuta na materials na miujiza kuliko Jina la Yesu, na haao ambao kuwaona lazima utoe pesa, hao hata mimi ndugu zangu nitawashauri tu wasiende ila sitakuwa dictator kwao kama ulivyo wewe. ni ukoloni huo kuwa dictator nyumbani unachagulia watu namna ya kumtafuta Mungu, pia ni ushamba huo. ila kuokoka kupo palepale unatakiwa kuokoka ndugu, la sivyo haupo salama.