Nimemtimua Nabii aliyekuja kumtembelea Mke wangu

Nimemtimua Nabii aliyekuja kumtembelea Mke wangu

Paragraph ya kwanza umetumia maneno makali sana, lkn chini kuendelea umepiga nyundo mnooo umesamehewa hiyo kwa ukali wa maneno...shida kubwa hatusomi bibilia na kuitafakari....umenyooka na kuja na.mstari....SADAKA NA.MANABII
Ha ha ha! Wanauzi Sana Hawa wa ongo na kufanya Mungu haonekane hafai
 
Kama ni mkristo na umefunzwa maandiko utajua kwanini wakina Elia/Elisha/Yeremia/Daniel na wengine weengi walifanya miujiza na wengine hawakufanya

Huyo pastor na nabii alikuja na Subaru:

Elisha/Petro/Daniel na wengine walikuwa na ndevu tu bila Subaru.
 
Well done, hakuna watu wanagonga wake za watu kama manabii
Mughonile!

Nilimuoa Mke wangu miaka 9 iliyopita. Kwa sasa tunawatoto wawili.
Mke wangu alikuwa amebobea kwenye Makanisa haya ya upako.

Baada ya kukubaliana na vigezo vyangu, ambacho kimoja wapo nilimuarisha aachane na manabii wa upako, akakubali.
Ndipo nilipomuoa Kwa ndoa takatifu ya kikristo.

Ni miaka 9 sasa imepita, juzi Yule Nabii na waumini wengine walikuja kumtembelea Mke wangu. Tuliwapokea vizuri wakapiga Stori zao.

Tatizo wakataka waanze kuomba na kabla ya kuomba waimbe mapambio Yao. Kwa kweli niliwazuia, niliwaambia tuheshimiane. Kelele nyumbani kwangu ni mwiko na ndio maana ninaishi sehemu yenye makazi tulivu.

Tukazozana, nikawafukuza! Mke wangu ananiambia ninaroho ngumu,
Nikamjibu sio roho ngumu tuu Bali roho mbaya kabisa.

Nimewapiga marufuku kuja kwenye nyumba yangu kujifanya wanajifanya wanaombea ombea watu. Nani anashida na kuombewa hapa!

Nimewaambia wakija waje Kwa inshu nyingine.

Pumbavu!
 
MTU aliyezaliwa kama we we,aliyetoka kwenye uke wa Mwanamke kama wewe atakuombea nini?.
Kama hayo maombi yanafanya Nazi aoembe Mungu ampe maisha yasiyokuwa na kifo.

Mbona Yesu Kristo alizaliwa na kutokea kwenye uke wa mwanamke??

Je unatupanujumbe gani kwenye hilo
 
Mkeo atakuwa anajilaumu kuolewa na kakisi
 
Viongozi wa kidini wanakula sana wake za watu.
Sema mara nyingi ni wanawake wenyewe wanajilengesha.
Ni kweli mimi mwenyewe mchungaji wangu ni mshikaji wangu sana sema ni mtu mzima namuhunganishiaga mademu au nampa namba zao

Utaskia dogo nipe namba ya pisi kali kwenye hizo jumuiya zenu vijana
 
kuna siku utakamatika hapo, hata kunyanyua ulimi uongee hutaweza, hata kunyanyua mguu uende chooni hutaweza. utahitaji msaada wa wanadamu hautakuwepo, utahitaji msaada wa madoctor hautakuponya, utaanza mwenyewe kuhitaji watu waje hapohapo nyumbani waimbe mapambio na kukuombea kwa Mungu. nina ndugu yangu alikuwa kama wewe, alikuwa na pesa, mtu mkubwa serikalini huko, shetani alikuja kumletea ugonjwa, nilipomtembelea nilikuwa nakuta muda wote ameweka channel za mahubiri tu tena ya walokole, mtu wa kulala tu kitandani kila kitu hapohapo hata tv wamemsogezea karibu na kitanda, imefika mahali akawa anaamini labda uwepo wa channel ya kidini utatransfer uponyaji uje kwake. kiburi chooote kwisha.

hata wewe ni kwasababu u mzima, na unaamini huhitaji hayo mambo. nakuhakikishia kuna siku utaikumbuka hii thread na utakuja kuwashauri watu wengine wenye moyo kama wa kwako.

jambo lingine, kila mtu atauchukua msalaba wake mwenyewe, na atahojiwa mbele za Mungu kwa habari zake binafsi, mke hatachukua mzigo wa mume wala mume kuchukua mzigo wa mke wala wa watoto wake. hivyo acha kubana mke wako. kwanza inaonekana ulimkuta akiwa mwamini ukambadilisha ili afuate imani yako ya dini isiyo ya kuokoka. baada ya miaka 9 bado unamchagulia cha kuamini na namna ya kuamini. huo ni ukoloni, mwache asali anavyoamini, si ukute yeye akawa sahihi akaja kukusaidia, au akakuta imani tofauti huko akaja kukushauri kuwa usiende huko alikokuwa ameenda.

kitu pekee ambacho tunaweza kukubaliana mimi na wewe ni kuhusu manabii wa mafuta, hao hata mimi siwaamini hasa hao wanaobase zaidi kwenye mafuta na materials na miujiza kuliko Jina la Yesu, na haao ambao kuwaona lazima utoe pesa, hao hata mimi ndugu zangu nitawashauri tu wasiende ila sitakuwa dictator kwao kama ulivyo wewe. ni ukoloni huo kuwa dictator nyumbani unachagulia watu namna ya kumtafuta Mungu, pia ni ushamba huo. ila kuokoka kupo palepale unatakiwa kuokoka ndugu, la sivyo haupo salama.


Mtu akikamatika watu wanahangaika kutafuta pesa za matibabu na sio manabii.

Kuwa na Akili hata kidunchu
 
Kuna siku utawatafuta mwenyewe ili wakuombee, wao wamekunguta mavumbi mzigo umebaki kwako
Ni ujinga tu kumwita mtu aje akuombee, Mungu hana ubaguzi anamsikiliza kila mwenye shida.hao watu ni wajanja tu hakuna cha nabii wala mchungaji.
 
Unaona sifa mwenyew, yaani unajiona mwamba, hahahah ipo utawatafuta hao wakat huo utazitamani hizo kelele na mapambio yao, kwani ungewacha wakafanya ibada wakaondoka ungepungukiwa nini?


Ibada wakafanyie kanisani.

Nyumba yangu inamiongozo sio kila mtu anaweza kuja kufanya maombi atakayo.

Wapo watu siwezi waruhusu waombe kwenye nyumba yangu.
Wake wasalimie wapite kushoto.

Mimi sitishwi na wapumbavu Kama wewe, na Maneno ya KIPUUZI. Ati ipo siku,
 
Mughonile!

Nilimuoa Mke wangu miaka 9 iliyopita. Kwa sasa tunawatoto wawili.
Mke wangu alikuwa amebobea kwenye Makanisa haya ya upako.

Baada ya kukubaliana na vigezo vyangu, ambacho kimoja wapo nilimuarisha aachane na manabii wa upako, akakubali.
Ndipo nilipomuoa Kwa ndoa takatifu ya kikristo.

Ni miaka 9 sasa imepita, juzi Yule Nabii na waumini wengine walikuja kumtembelea Mke wangu. Tuliwapokea vizuri wakapiga Stori zao.

Tatizo wakataka waanze kuomba na kabla ya kuomba waimbe mapambio Yao. Kwa kweli niliwazuia, niliwaambia tuheshimiane. Kelele nyumbani kwangu ni mwiko na ndio maana ninaishi sehemu yenye makazi tulivu.

Tukazozana, nikawafukuza! Mke wangu ananiambia ninaroho ngumu,
Nikamjibu sio roho ngumu tuu Bali roho mbaya kabisa.

Nimewapiga marufuku kuja kwenye nyumba yangu kujifanya wanajifanya wanaombea ombea watu. Nani anashida na kuombewa hapa!

Nimewaambia wakija waje Kwa inshu nyingine.

Pumbavu!
Da! Hongera sana nazani mkanye mkeo asirudi kwenye hayo madhehebu asali dhdhebu mlilofungia ndoa kama hataki mwambie atalaka itamfuata
 
Shwaini
me nilifurumusha wanatembea na msalaba kwangu.

Na niliwaeleza kwangu kuleta miti ya mifano hapana kabisa .

Na nikamkanya wife mbele yao ili kileta hali ya uhalisia .

Binafsi sijawahi kuwapenda roman churches na mambo ya unabii.

Ni vitu vya kupigwa sana.
Roman Churches,hakunaga makelele,mzee.
 
Back
Top Bottom