Miaka kadhaa nyuma katika pita pita za social media nilikutana na binti mmoja ambae nilisoma nae Primary, takriban miaka 25 iliyopita.
Nikawasiliana nae na kama ilivyo ada tukabadilishana namba (hata hakuwa ananikumbuka zaidi ya kuamini maneno yangu tu baada ya kumtajia shule na darasa).
Katika maongezi kabla hata ya kukutana, ghafla akapatwa na 'shida', 'mzigo' wake ulikwama bandarini na kuwa alihitaji Mil. 1 ya haraka.
Kwanza nilimwambia subiri nitakucheki, ila ikawa kama deni. Nikaona kwanini najitesa kwa mtu ambae hata hanijui. Nilimchana live tu kuwa sio kwamba sina hiyo pesa lakini siwezi kukupa sababu kwanza ulikuwa hata hunijui hata baada ya kukumbusha, kama isingekuwa unawasiliana na mimi ungeomba kwa nani hiyo pesa, sio kila anaekuomba namba ana nia ya kukutongoza kimapenzi na mwisho kabisa sio kila mwanaume utakaempata ni ukombozi wa ufukara wako.
Japo ilikuwa ni kwenye simu, lakini sauti yake ilisikika kabisa kuwa alifedheheka. Na baada ya hapo sikupokea tena simu zake japo alijaribu sana kunipigia.
Kuna wakati ni bora kuwachana ukweli tu hawa viumbe.