Mwanaume hutakiwi kushindwa chochote. Tafuta namna ya kumwongoza huyo mke akae sawa. Njia uliyotumia ya kukimbia tatizo utakuja kuijutia.
Kwa mfano, baada ya muda kidogo utaanza kusikia kuna kidume mwenzako amefanya makazi ya kudumu kwenye kitanda ulichonunua, nyumba uliyojenga kwa jasho lako, na anajenga kwenye viwanja vyako.
Ninaamini utawaza kubadili mawazo na kurudi kwenye mali zako kuzikomboa. Utakuja hapa upya kuomba ushauri namna ya kurudia mali, mke na watoto wako.
Kumbuka huyo mkeo hana cha kupoteza. Ukikimbia atapata nafasi nzuri zaidi ya kujiachia. Na vidume watakula mpaka atakolea.
Jitakari upya.