Nimemwelewa sana Mbowe, usipoteze imani na Rais Samia. Alivyo kwa Kauli na Matendo hawezi kuwa ni yeye!

Huko kwa raisi ndio kabisa as an independent cadindate, kuunda kwa serikali bargaining power atakazotoa ni kutekeleza ilani ya chama kingine. Vinginevyo wanarudi kwenye chaguzi tena.

Fuatilia chaguzi za Israel, huko washakaa mpaka miezi 17 bila ya serikali kisa vyama avitaki kuungana. Miaka 5 uchaguzi mara tatu kisa ugumu wa kupata majority ya bunge na kuunda serikali.

Ni hivi kabla ya kukimbilia habari za mgombea binafsi, walau hao watoa hoja wangeelezea mechanics za hang parliament, utaratibu wa kuendesha nchi wakati hakuna serikali.

Huko Germany na Israel ambapo kuna mgawanyo mkubwa wa votes kwa vyama kama vitano, wakati wanasiasa wanalumbana na kujadiliana miungano ya kimkataba ili kuunda serikali kuna civil service imara ya kuendesha nchi.

Sisi kila kitu kwa sasa ni wanasiasa, hatuna experience ya kukaa hata week moja bila ya serikali kuu. Haya mambo kwa wenzetu wamejipanga na risk mitigation strategies kwa scenario kadhaa za matokeo ya uchaguzi. Na senior servants wao sio watu wa mzaha kabisa, uwezo wao auna mashaka kabisa hasa makatibu wakuu ni watu ambao wametengenezwa kuendesha nchi hadi kufikia hizo nafasi.

Sisi hata atujadili scenarios kadhaa tunazimudu vipi tunachotaka ni wagombea binafsi na wapiga kura wenyewe si unawaona it’s possible kabisa kwa watanzania chini ya uchaguzi huru na wa haki bunge likajaza over 70% ya independent candidates (kasheshe).

Watu wenyewe wa kuendesha nchi hakuna tunateua tu makatibu wakuu wa wizara kwa kujisikia na unakuta katibu mkuu kiongozi ajawahi ata kushika nafasi ya ukurugenzi ndani ya wizara let alone kuwa katibu wa wizara na ndio mtu wa kuongoza nchi kwenye scenario isiyo na serikali.

Sometimes it’s not about democracy, but common sense given the reality of social factors. Swala la kuendesha nchi sio la mzaha kama tunavyolichukulia.
 
Kuanzia siku ya kwanza alipokwenda Ikuku, nchi ilipigwa ganzi, dalili nzuri kabisa kwamba Watu hawakuridhika

Wananchi wakapaza suati za kumkanya kwamba maridhiano yake na SSH hayana mantiki, ni utapeli wa CCM
Mbowe akajibu kwa hoja rahisi '' S. Africa kama ilivyo Ukraine' wapo katika mazungumzo na 'Watesi wao'

Mbowe akawa msemaji wa CCM kuhusu maridhiano, CCM wakiwa kimya! Hakuna, hakuna! kiongozi wa ngazi za juu wa CCM aliyezungumzia 'maridhiano' hata kwa bahati mbaya. Mbowe akajitwisha wajibu huo

Mbowe akalinganisha Wanacha wa Chama chake na Wahafidhina wa CCM akisema wapo kila mahali. Aikaeli hakujali kwamba Wanachama wake ni 'loyal' siyo 'chawa' kwahiyo hakuna ulinganifu. Freeman akawa free katika maridhiano

Aliulizwa kuhusu COVID-19 kama 'bargaining chip' ya kwanza, Mbowe akajibu ' Bunge ni taasisi lina taratibu nyingi za kuwaondoa' akitetea urasimu uliokuwa unaendelea. Yaani kuondoa Wabunge haramu kama wale wa CUF ilikuwa kazi sana kwa mujibu wa M/Kiti wa Chadema.

Hili siyo tukio (event) wala siyo bahati (coincidence) ni mtiririko wa failures ( pattern) wenye jibu moja tu, ni wakati ima aondoke kwa heshima au aondolewe na chama chake. Hakuna option nyingine ni wakati aondoke!

FAM jiuzulu umefeli sana, haya ya kutapeliwa maandiko yalikuwa ukutani ukajitia upofu. JIUZULU ni jibu rahisi na zuri kwako na Chama chako! Wakati umefika, achia ngazi haraka ili kunusuru chama chako na Taifa!

Ahsante kwa mchango wako katika demokrasia ya nchi, umelipa gharama kubwa hilo halitahaulika, lakini wakati si wako tena! umechoka!
 
Hivi wewe ni mwanasheria gani. Yaani umeisha Sema miswada iliyo pitishwa ni batili. Hapo hapo unashauri chadema washiriki uchaguzi kwa sheria batili. Halafu ndio wapumzishe serikali iliyopo kwa kutumia tume ya uchaguzi batili na inayo endeshwa kwa sheria batili. Halafu unatetea Samia kwa kuhalalisha batili wote huo. Wewe tu Sema unatafuta kitu kwa raisi au unanufaika na batili hiyo tujuwe moja.
 
Ni kweli na naongezea hapa, UK walikaa wiki 3 bila serikali na India walikaa miezi 3 bila serikali.
Sisi unadhani hatuwezi, si kwasababu hatuwezi bali mifumo yetu imesukwa 'tusiweze' ndio maana tunahitaji Katiba mpya na hilo litasaidia ikitokea kama India , UK, Israel, Ujerumani n.k.
Ni hivi kabla ya kukimbilia habari za mgombea binafsi, walau hao watoa hoja wangeelezea mechanics za hang parliament, utaratibu wa kuendesha nchi wakati hakuna serikali.
Hapana, wapewe nafasi ya kueleza. Kwasababu hata upuuzi unaofanywa wa 'makongamano ya miswada' watu wanalazimishwa kujadili miswada na si kutoa maoni ya hizo '' mechanics' unazosema. Unaona tatizo lilipo?
Huko Germany na Israel ambapo kuna mgawanyo mkubwa wa votes kwa vyama kama vitano, wakati wanasiasa wanalumbana na kujadiliana miungano ya kimkataba ili kuunda serikali kuna civil service imara ya kuendesha nchi.
Ni kweli na ndio maana tunahitaji Katiba mpya ili kujenga hiyo 'civil service' imara. Kumbe unakubali yetu si imara, sasa tuta fix vipi kama hatujadiliani kwa kutumia sheria mama ambayo ni Katiba?
Tunahitaji katiba ili kujenga civil service imara !
Sisi kila kitu kwa sasa ni wanasiasa, hatuna experience ya kukaa hata week moja bila ya serikali kuu.
Tuna miaka 60 Uhuru, unachosema hapa ni kwamba sisi ni Wajinga. Huwezi kumnyonyesha mtoto hadi miaka 5 halafu umlaumu kwa kunyonya na si wewe mzazi kutafuta suluhu.
Hapa unatusaidia sana kudai katiba mpya ili kujenga mifumo imara

Tuna miaka 60 sisi tutajipanga lini na 'mitigation strategies' kama unavyosema?
Tunahitaji Katiba mpya ili kujenga na kuingiza mawazo mazuri kama yako. Kama hatujadili tunaletewa ujinga na wale wale waliotufikisha hapa miaka 60 unategemea nani aje kutusaidia!
Hapa ndipo pa kuanzia kwasababu hawa wa vyama wamefeli.
Tafuta historia ya mataifa yaliyofanikiwa, ni kwamba yamepita katika majaribu.

Ningefurahi sana kama tungekuwa na independent candidates. Hivi tunakipi cha kupoteza zaidi?
Watu wenyewe wa kuendesha nchi hakuna tunateua tu makatibu wakuu wa wizara kwa kujisikia na unakuta katibu mkuu kiongozi ajawahi ata kushika nafasi ya ukurugenzi ndani ya wizara let alone kuwa katibu wa wizara.
Ni kweli kabisa, ndio maana tunahitaji Katiba ili kuondoa uozo huo. Kama hatutakaa na kujadiliana hali hii tutaimudu vipi? Si unaona jibu lake ni Katiba mpya.
Sometimes it’s not about democracy, but common sense given the reality of social factors. Swala la kuendesha nchi sio la mzaha kama tunavyolichukulia.
Yes na common sense zinasema miaka 60 na watu wale wale tumefeli. Hatuna taasisi imara kama za wenzetu. Tunahitaji mifumo mipya kama wenzetu ambapo Serikali ni watu si mtu.
 
Ndugu angalia BRT kama mfano on paper ni mradi mzuri sana.

Tumejenga infrustructure nzuri ya njia na vituo, tumeanza na mabasi ya kutosha na wateja ndio wamejazana.

Huko serikalini hatuna watu wa kuendesha huo mradi, mabasi chali hayana schedule maintenance, ghala la spare parts watu wameiba inventory yote, service tunapeleka kampuni binafsi (with overpriced), vituo machine za electronic kila siku mbovu, vituo vyenyewe upkeep ni kama hamna vimeshaanza kuchakaa.

Hiyo inakwambia nini huko serikalini Hakuna watu wa kusimamia kitu.

Imagine hang parliament ya Tanzania. Budget za wizara wajiamuliwe wenyewe civil servants, OC, makusanyo wajiamulie allocations zake kwa miezi sita tu; huko kwenye afya, mashuleni, umeme, huduma za serikali kutaoza balaa.

Tuna mifano ya kutosha as warnings sign ya kutuambia kuna vitu tusijaribu kwa sasa unless tunataka kutengeneza matatizo makubwa kwa wananchi.

Hao wapiga kura wenyewe ukiwaachia wachague mtu kwa ridhaa yao usishangae wakakuletea Harmonize, jimbo la Kawe badala ya Pascal. Kama una kumbukumbu nzuri ‘Irene Uwoya’ alishinda kwa haki kabisa viti maalum (Tabora nadhani kama sijakosea) 2015 akakatwa tu jina baadae na CCM. Chezea akili za watanzania wewe.
 
Na huwezi kukaa kimya ukitegemea mifumo itajirekebisha , ni lazima ufanye jambo
Tukifanya haya haya kwa namna hii hii na njia zile zile tuakuwa tumekidhi definition ya Insanity kwa 100%

Tutengeneza Katiba itakayozuia madhara na kutupa mweleko. Hilo ndilo jibu.
 
Shida ya katiba ya Tanzania ni mamlaka ya raisi.

Huko serikalini wana utaratibu mzuri wa succession planning za watu wa kushika wizara but their ascendency ends at katika nafasi ya ukurugenzi.

Makatibu wakuu anachagua raisi, nafasi za mikoa na wilaya karibu zote anachagua raisi (wakati hizo ni meritocracy positions), kutakuwa na shughuli hapo ya utendaji makini kama raisi anajaza makada kwenye hizo na nafasi.

Bado uelewa mdogo wa wapiga ukifanya mzaha watakuletea darasa la saba kisa popular tu huko wilayani bunge lijaze watu aina ya kibajaji, babu Tale na msukuma.

Kuna vitu tunavyolilia bado ndio CCM ni shetani. Ila ni zimwi likujualo.

Siku ukiona watu wanapambana kupunguza madaraka ya raisi kwenye katiba ndio ntaamini watanzania sasa wameamka hapo ndio kwenye shida halisi ya katiba.
 
Nimecheka ila huu ndio ukweli, niliwahi kusema humu, Kwa mambo makubwa anayoyafanya mtoto wa Tandale, kama wananchi wakimuhitaji tuu, Kubenea mpishe!.
Kawe - Harmo
Ubungo - Mondi
Bagamoyo-Kiba
Ilala- Dully
Temeke- Nature
Mbagala- Mkubwa Fella
Etc.
Mimi nilipotupa karata yangu Kawe, nilikuwa na genuine agenda ya kusaidia hili Bunge kujipendekeza na kujikombakomba kwa serikali lisimame imara liisimamie serikali
View: https://youtu.be/Qr6j25jFGyI?feature=sharedKumbe Chama Chakavu Mbogamboga hakipendi watu critical!, wanatakiwa "Ndio Mzee" siku hizi "Ndio Madam...", hivyo watu kama Luhaga Mpina, 2025 ni end of the Road kwa CCM, lakini tungekuwa na independent candidates, Mpina akisimama na Kizimkazi..., by saa 4:00 asubuhi, Kizimkazi tupa kule!, Chama Chakavu chali!.
P
 
Kwa taarifa yako kwenye rasimu ya Warioba Kuna vipengele vya kupunguza madaraka ya rais, lakini wingi mbovu wa ccm ulitumika kuhujumu matakwa halali ya wananchi. Kila mtu anajua madaraka ya rais yaliyojuu ya Sheria, ndio chanzo halisi Cha udhaifu wa mifumo yetu ya kiutawala.
 
Kwa katiba hii hata uweke mgombea wa aina gani, ccm itatangazwa washindi bila kujali box la kura linasema nini. Ni aidha machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi ili kupata mabadiliko ya kweli ya kiutawala hapa nchini. Lakini hizo 4R ni utapeli kama utapeli mwingine.
 
Kwa Katiba hii ni mjinga na mpumbavu tu atakayeshindwa uchaguzi wa aina yoyote
Mkapa alishindwa waka-force uchaguzi siku ya pili na kuvuruga kila kitu
JK alithibitisha hilo kule Zanzibar kwa kumtumia Jecha
Magufuli kafunua kila kitu hakuwa na mwamana na mtu. Yeye aliisigina na kuitupilia mbali

TLS kupitia Dr Nshalla ilieleza wazi Rais SSH alipaswa kuvunja Baraza la Mawaziri kama Katiba inavyoelekeza
Hakuna kilichotokea kwasababu Katiba ya 1977 inaumwa haiwezi kujitetea . Inapumulia mashine za Wahisani

Watu wote wakiwemo wa CCM wanasema Katiba mpya inahitajika. Ukiona hawasemi ni wanufaika wa mfumo kama Makamu Wastaafu, Mawaziri wakuu wastaafu, Maspika wastaafu n.k. wanaogopa mafao yao au dhambi zao kuanikwa

Waliohujumu mchakato ni CCM na walifanya hivyo kwa msingi ule ule wa kwamba bila katiba ya 1977 hali ni mbaya.

Ndiyo maana tunajiuliza hivi lifikiri nini kwenda kwenye kuasisi maridhiano maana alipotoka Ikulu yeye ndiye alikuwa msemaji, siyo CCM.

Hakuna namna tunaweza ku justify fyongo ya Mbowe!

Mbowe amezotesha sana harakati zilizokuwa na moto kabla na hata akiwa Magereza. Baada ya kukimbilia Ikulu akawa submissive na kugeuzwa kauzu, sasa ameuzwa tena kwa bei ya kutupa.
 
You are absolutely right!
 
Upo sahihi hii katiba inanufaisha koo chache sn tena zilezile miaka yote
 
Mayala alikuwa mayara kabla ya magufuli kumtisha baada kumuuliza swali gum
 
Mkuu Pascal Mayalla Baadhi ya watumishi kwa nafasi zao wana Fanya kiongozi mkuu wa nchi kuonekana hatendi haki, dawa yao wakithibitika watumbuliwe, washtakiwe na waadhibiwe... Kuna sekta zinanuka kwa kupindisha haki, Siku watu wakichoka itakuwa too late, Mungu AMJALIE kiongozi wetu mkuu wa nchi maono haya ya kuchukua hatua atufikishe pazuri, Taifa letu litainuliwa kwa haki kutamalaki
 
Paskal umemdogosha Mhe.Rais.Kwamba yeye hajui chochote kinachoendelea.
 
Hizi ndizo hoja ambazo watu waelewa tunaweza kusoma na kuona jinsi gani Tanzania amelindwa na Wazalendo wa kweli walioipokea nchi toka kwa " wazungu"...mbegu ile ndio itaiweka nchi hii salama kwa miaka mingi .Vyama vya siasa( vya hapa kwetu) ni mchezo mzuri na mbinu kuu tuliitumia wakati ule wa shinikizo toka kwa watawalq wa Dunia.Tembea duniani,sikiliza wanadamu wanavyopambana kuielewa Tanzania yetu ,ndipo utawaheshimu Viongozi na wazalendo wa kweli waliotufikisha hapa!
Tutafanikiwa kucheza na mambo mengine mengi lkn issue ya hili Fumbo ( lenye kheri)...hakuna mzungu wala mtanzania wa kulibadili..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…