Mayor Quimby
JF-Expert Member
- Mar 13, 2021
- 4,950
- 10,977
Huko kwa raisi ndio kabisa as an independent cadindate, kuunda kwa serikali bargaining power atakazotoa ni kutekeleza ilani ya chama kingine. Vinginevyo wanarudi kwenye chaguzi tena.Katika yoote, bila shaka hoja hapa ni mgombea binafsi..
Umejitetea kuwa ni hatari kuwa na mgombea binafsi.
Kwamba, ni vyema kuendelea na mfumo wa sasa wa kila atakaye uongozi wa kuchaguliwa ktk nchi yetu apitie kwenye chama cha siasa..
Sababu yako ni kuwa, mgombea binafsi hadhibitiki, hana chama cha kumdhibiti... Na hapa ndipo upogo wa hoja yako ulipo..
Inaelekea wewe ni miongoni mwa wana CCM waoga wa mabadiliko wanaofaidika na mfumo huu mbovu kiasi cha kuutetea kwa sababu za kitoto sana..
Unaandika kana kwamba hatuwezi kujiwekea utaratibu wa checks & balance ktk mambo haya. Na woga, hofu na wasiwasi wako huu unaweza kuondolewa kwa kukaa wote chini na kutengeneza utaratibu kupitia kutengeneza katiba mpya inayoweza ku - harmonize haya yote..
By the way, uzoefu wa nchi zote zilizoruhusu mgombea binafsi unaonesha kuwa it's very rare wagombea binafsi kuingia kwa wingi ktk vyombo vya maamuzi kama bunge au mabaraza ya miji nk nk..
Hata kama ikitokea mgombea fulani asiye na chama (mgombea binafsi) ameshinda ktk nafasi ya u - Rais, lazima katiba ieleze ni kwa namna gani mgombea huyu ataunda serikali yake. Ndivyo ilivyo ktk nchi za wenzetu..
Tatizo ni Moja kuwa, CCM hawataki mwafaka wa kitaifa kupitia katiba mpya na ndiyo maana wana - reject kila kitu hata ambavyo ni vya muhimu na vinavyoweza ku - fast track maendeleo yetu ya kiuchumi na kijamii kwa sababu kama unazotoa wewe..
Haiwezekani ktk kupiga kura watu wote wanaweza kupiga kura kuchagua viongozi wao ktk uchaguzi bila kujali ni wanachama wa vyama vya siasa au la...
Lakini ktk kugombea nafasi za uongozi Ili upigiwe kura, eti watu haohao wanachama na wasio wanachama wa chama chochote cha siasa eti unawawekea sharti la kuwa wanachama wa vyama vya siasa..!!
This is very ridiculous and undemocratic arrangements..!!
Fuatilia chaguzi za Israel, huko washakaa mpaka miezi 17 bila ya serikali kisa vyama avitaki kuungana. Miaka 5 uchaguzi mara tatu kisa ugumu wa kupata majority ya bunge na kuunda serikali.
Ni hivi kabla ya kukimbilia habari za mgombea binafsi, walau hao watoa hoja wangeelezea mechanics za hang parliament, utaratibu wa kuendesha nchi wakati hakuna serikali.
Huko Germany na Israel ambapo kuna mgawanyo mkubwa wa votes kwa vyama kama vitano, wakati wanasiasa wanalumbana na kujadiliana miungano ya kimkataba ili kuunda serikali kuna civil service imara ya kuendesha nchi.
Sisi kila kitu kwa sasa ni wanasiasa, hatuna experience ya kukaa hata week moja bila ya serikali kuu. Haya mambo kwa wenzetu wamejipanga na risk mitigation strategies kwa scenario kadhaa za matokeo ya uchaguzi. Na senior servants wao sio watu wa mzaha kabisa, uwezo wao auna mashaka kabisa hasa makatibu wakuu ni watu ambao wametengenezwa kuendesha nchi hadi kufikia hizo nafasi.
Sisi hata atujadili scenarios kadhaa tunazimudu vipi tunachotaka ni wagombea binafsi na wapiga kura wenyewe si unawaona it’s possible kabisa kwa watanzania chini ya uchaguzi huru na wa haki bunge likajaza over 70% ya independent candidates (kasheshe).
Watu wenyewe wa kuendesha nchi hakuna tunateua tu makatibu wakuu wa wizara kwa kujisikia na unakuta katibu mkuu kiongozi ajawahi ata kushika nafasi ya ukurugenzi ndani ya wizara let alone kuwa katibu wa wizara na ndio mtu wa kuongoza nchi kwenye scenario isiyo na serikali.
Sometimes it’s not about democracy, but common sense given the reality of social factors. Swala la kuendesha nchi sio la mzaha kama tunavyolichukulia.