Wanabodi,
Nimemsikiliza Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe katika bandiko hili Mbowe: Najutia kumuamini Rais Samia
View: https://youtu.be/Xjao83Ghy04?si=qSQTeSxIx_8B5a-L
Kiukweli kabisa mimi nimemwelewa sana Mwenyekiti Freeman Mbowe hapa, na hata ningekuwa mimi!, I would have felt the same!.
Namuomba sana Mhe. Mbowe, please usipoteze imani na Rais Samia!, kwasababu Rais Samia ninaye mfahamu mimi, sio mtu mwenye ndimi mbili!, namfahamu fika Rais Samia kwa kauli na matendo, yeye kama yeye, hawezi kabisa kusema hivi hakafu akaja kutenda vile!. She is straight and firm, tena usikute yeye wala hajui kuwa mswada sheria ya uchaguzi ni batili kwasababu yeye sio mwanasheria!.
Kwa bahati nzuri, mimi ni miongoni wa watu wanaomfahamu Rais Samia sio tuu kwa kauli na matendo, bali kwa kufanya nae mahojiano ya ana kwa ana mara mbili. Mara ya kwanza akiwa Waziri Ofisi ya Makamo wa Rais na mara ya pili akiwa Makamo Mwenyekiti wa Bunge la Katiba.
Wakati akiwa VP nilimfanyia uchambuzi mara mbili
Mara ya kwanza ni hapa Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” na mara ya pili ni hapa "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Na baada ya kuwa Rais wa JMT, pia nilimfanyia uchambuzi Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila... na Ili kupata Viongozi Bora baadae, Watanzania tujifunze kuwasoma watu kwa asili zao. Mjue Samia alivyo kwa asili yake
Hivyo kwa kauli na matendo, hiki kinachofanyika kwenye miswada hii, naamini kabisa watu waonayafanya haya sio Rais Samia, naamini kabisa yeye wala hajui kuwa muswada wa sheria ya uchaguzi ni muswada batili unaokiuka ibara ya 11 ya katiba ya JMT.
Kwa vile yeye sio mwanasheria, hajui kuwa katiba yetu ni batili, kwa kuchomekewa ubatili unakokwenda kinyume cha Ibara ya 5 na ibara ya 11 ya Katiba yetu.
Nimesema ninaamini kabisa Rais Samia hayajui haya na hapa niliandika Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!.
Hivyo kitendo cha Freeman Mbowe Kutomwamini Rais Samia, ni kumuonea bure, niliwahi kushauri Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
Bahati nzuri sana na mimi nimehudhuria vikao vyote vitatu vya kukusanya maoni ya wadau na mara zote 3 nilipata bahati ya kuchangia.
Mchango wangu kikao cha kwanza ni huu
View: https://youtu.be/PBpjDhH2XiA?si=9dtqZ-1-ZkzWo69t
Mkutano wa pili maoni yangu ni haya
View: https://youtu.be/3a4SjkV46JY?si=98HTkiMGNsmlLBGz
Na Mkutano wa tatu wa Kamati ya Bunge pia nilitoa maoni.
Nimeandika makala zifutazo kuhusu sheria hizi
-
Licha ya Mapungufu, Sheria Mpya ya Uchaguzi Pia ina Mazuri Yake!, Imerejesha Mamlaka ya Uchaguzi kwa Wananchi, Hakuna Kupita Bila Kupingwa!.
Wanabodi, Hili ni bandiko mwendelezo wa three series za uchambuzi wangu wa sheria mpya ya Uchaguzi, 2023. Kama hukuona 1st series, anzia hapa Asante Rais Samia kwa Muswada huu. Umuhimu wa mabadiliko ya Katiba kabla ya Sheria hii bado ni muhimu sana. Huu ni uchambuzi Wangu - Part 1 kisha uje...www.jamiiforums.com
- Maoni yangu kwenye Mkutano wa Vyama vya Siasa kuhusu Muswada wa Sheria Mpya ya Uchaguzi. Muswada sio batilifu, ni Muswada batili
- Asante Rais Samia kwa Muswada huu. Umuhimu wa mabadiliko ya Katiba kabla ya Sheria hii bado ni muhimu sana. Huu ni uchambuzi Wangu - Part 1
- Je Wajua Muswada Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani 2023 ni Batili?. Ni Mvinyo wa Zamani, Kwenye Chupa Mpya?. Why Ubatili Huu?!.
- Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!.
- Tujifunze kuwa na Shukrani kwa Madogo ili Tupatiwe Makubwa!. Japo Tulitaka Kikubwa, Tumepewa Kiduchu!, Tukipokee Tushukuru, au Tususe Kudai Kikubwa?.
- Lile fupa lililowashinda marais wanaume 4, rais mwanamke 1 aligegeda kama mlenda!. Miswada 3 ya ukombozi mpya wa taifa letu yatua bungeni asubuhi hii
- Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi: Je Tupige Ndege Wawili kwa Jiwe Moja kwa Uchaguzi Serikali za Mitaa/Mkuu, Ufanyike Siku Moja au Tuendeleze Mazoea?
- Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
- Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
- Prof. Lipumba: Nina Matumaini Makubwa na Rais Samia, Chaguzi Zijazo Zitakuwa Huru na Haki!, Mambo ya 2019/2020 Yasijirudie!
- Face 2 Face with Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo: "Tunafanya Politics of Engagement kwa kuwa Pragmatic on What is Possible"
- JNICC: Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia Kutathmini Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi na Hali ya Siasa Nchini
- Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana!
-"Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do
-"Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
Baada ya Mhe. Freeman Mbowe kutangaza maandamano nimetoa ushauri issues za kisiasa zitatuliwe kisiasa, halafu issues za kisheria zitatuliwe kisheria, utungaji miswada ni issue ya kisheria, baada ya watu kutoa maoni yetu, Bunge likitutungia sheria batili, this time around, we'll have to do something!.
Tangu Rais Samia ameingia madarakani ile March 21, mimi tuu mwenyewe, nimelisemea jambo hili zaidi ya mara 20!.
Mhe. Freeman, rudisha moyo, applies zile 4R za Rais Samia tulisongeshe mbele kwa mbele.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali.
Nilisema hapa
Mambo manne makubwa ambayo yataweka mwelekeo wa kisiasa Tanzania
Kuna Mambo manne muhimu kwa miezi ya karibuni ambayo yataleta mwelekeo wa taifa letu kisiasa katika mambo haya manne matatu ni ya Chadema na mmoja ni la CCM. Chedema inatakiwa kufanya maamuzi magumu kwenye haya mambo matatu 1. Bila katiba na tume huru ya uchaguzi wajitoe kabisa kwenye chaguzi...