Nimeoa wiki mbili tu zilizopita, lakini tayari nimechoshwa na maisha haya. Nahisi kama ninaishi maisha ya kipumbavu . Nashangaa jinsi watu ambao wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka mitano au zaidi wanawezaje kuvumilia huu ujinga!
Niko kitandani na huyu Binadamu , lakini ameninunia tangu jana. Nimejaribu kuzungumza naye, lakini hataki kuonyesha ushirikiano .
Nafikiria kumfukuza arudi kwao.
Nadhani ni bora niishi peke yangu kuliko kuishi na mtu huyu.
Ninahisi kuchanganyikiwa na kukata tamaa. Je, kuna mtu yeyote anaweza kunipa ushauri?