Nimeolewa ama nimeoa? Naombeni ushauri

Sasa mkuu mtu wangu aliniambia ili nmuoe akubali kumpa mtaji kwanza? Ndio aondoke kwao anasema yeye Ana degree yake hawezi kuwa mama ya wa nyumbani moyo wangu ulisita
 
Mnyime binadamu kila unachoweza ila chakula sio kitu cha kumnyima mtu

Si mlikubaliana kwenye shida na raha au ulifikiria shida wanazo sema huwa ni kula Kempisky kila siku na vacation Maldives, Santorini, Hawaii ,Bali,kila mwezi???

Fikiria wewe ndio ungekuwa unafanyiwa unavyomfanyia
 
Sema unamcheati nyuma ya pazia na hukumu umetoa tayari .kwenye ulimwengu huu hakuna waoaji,wanawake wanahonga sana wanaume Tena vijana wadogo,wewe kazi yako ishakwia tiyari(ushakuwa shangazi).hata ndugu zangu wa karibu sioni wakioa wanasema hawataki matatizo !
 
Imagine angekuwa kapigwa na stroke 🥴🥴
 
Huyo anahitaji mentorship shirikiana na ndugu zake wa karbu,


Ungekuw wew umeach kaz ungeish kwa aman tuu
 
Yap mimi nipishapitia situations kama hizo! nilikuwaga nafanya kazi zangu vizuri tu gafla mambo yakajaga kubadilika 2022-2023... (2 years).. ilifikia hatua nikifanya kazi naacha mwenyewe sitaki kazi, Sitaki kwenda kazini, Alafu nasema sijui niende nikatukane mabosi nifukuzwe kazi maana ndo furaha yangu nikifukuzwa nikakae tu nyumbani nilale, sitaki watu, sitaki ndugu, hasira e.t.c Mambo ni Mengi Nitakuja kuleta kisa changu humu hadi Mungu kuja kuniokoa na kuja kufanikiwa.
Mimi nikulala ndani tu, ikafikia hatua nilikua nataka nikagongwe na gari nife tu maana nilikua sioni thamani ya maisha tena...
Daah ashukururiwe yule mwanamke aliyenitoa kwenye dhahama ya mauti hiyo..

Nililogwa vibaya sana sana na wahusika nawahifadhi
 
Halafu unamnyima mtu hata chakula anaweza vipi kuwa na itimamu wa kufanya kazi,wewe ukiondoka mwachie hata 5000 ya nauli atajiongeza, psychological hawezi kuwa sawa ni vizuri uzungumze nae maneno mazuri ya kumfariji.
 
Hapa tumeskiza upande wakowa story, je upande wa mwamba upo hivyo mmh!
 
Duuuh pole sana,, muhimu umetoka aiseeee
 
Ulivyo kuwa unakula kiapo kwamba utashirikiana naye kati hali zote ikiwemo iyo ya umasikini,, ulikuwa unatania sio? Na ikitokea akarudi kwenye hali yake ya kawaida bado utaendelea na mchakato wa talaka? Dada kuna nyakati za neema na nyakati za uharibifu,, mumeo anapitia nyakati za uharibifu mvumilie
 
Chukulia Imetokea Upande Wako,,,alafu Huyo Unaemuita Mume Wako Unakuchabanga Kwenye Sosho Media Namna Hii Ungejisikiaje Kwa Mfano??Mume Wako Zungumza Nae Na Sio Mambo Ya Ndoa Unakuja Kuyatapanya Humu,,Kisa Umejaaliwa Kauwezo Basi Unaona Umemaliza?Jitahidi Kuwa Na Haiba Ya Utu Kwa Mumeo Hata Kama Mambo Hayako Poa,,Kwani Yeye Amekuvumilia Mangapi,,,Ametenda Mema Mangapi Hadi Hilo Uone Ni La Kuja Mtangaza Humu,,Kaa Chini Na Mumeo Muongee,,Acha Kujidhalilisha Humu...Nje Ya Mada Naomba Namba Yako Ya Nida Kama Hutojali Lakini.
 
Chukulia Imetokea Upande Wako,,,alafu Huyo Unaemuita Mume Wake Unakuchabanga Kwenye Sosho Media Namna Hii Ungejisikiaje Kwa Mfano??Mume Wako Zungumza Nae Na Sio Mambo Ya Ndoa Unakuja Kuyatapanya Humu,,Kisa Umejaaliwa Kauwezo Basi Unaona Umemaliza?Jitahidi Kuwa Na Haiba Ya Utu Kwa Mumeo Hata Kama Mambo Hayako Poa,,Kwani Yeye Amekuvumilia Mangapi,,,Ametenda Mema Mangapi Hadi Hilo Uone Ni La Kuja Mtangaza Humu,,Kaa Chini Na Mumeo Muongee,,Acha Kujidhalilisha Humu...Nje Ya Mada Naomba Namba Yako Ya Nida Kama Hutojali
 
achan naye huyo jamaa .

Ni mpuuzi, ni kweli Kuna wakati mambo yanayumba lkn kama mwanaume huwa nilazima usichoke kujihangaisha hata Kwa lolote

ACHANA NAYE, NA USIMPE K.
 
Mkuu tuongee kwenye uhalisia wa mambo.

Unajua Wanawake hawakuumbwa kutunza familia., wao wlaiumbwa kua walezi.

Msomi ,aloachishwa kazi ,miaka nane ( nahizi ni zile Enzi za Magufuli).

Miaka nane, Msomi katulia tu, Hivi hiyo familia Maendeleo yatapatikana kweli?.

Haya utasema Kuna Siku atakua sawa, atakaaje sawa kutwa kucha ni nyumban ,hatoki akanyangamana na jamaa, mishe ndogondogo ??.


Huyu mwanamke tutamlaumu Bure .


Mungu anachukia watu wavivu sana kula kulala.
 
Kuna wanawake toka wameolewa wapo nyumbani hawajawahi toa hata mia yao

Wengine wamefunguliwa biashara kadha wa kadha zimekufa

Lakini hakuna mwanaume anakuja jukwaani kuwananga

Ila rudi siku hiyo mwambie mkeo huna kazi au Anza likizo mwambie tumeachishwa kazi kwa muda usiojulikana uone moto wake......

Kama bi dada una kazi mpe mumeo kamtaji hata ka Banda la matunda au juice ya miwa au ukopee maake nyie ni mwili mmoja....
 
Afuate Utaratibu,,Amuache aende Kwa Huyo Atakaye Timiza Kikamifu Hicho Akitakacho Na Si Kuja Kumdhalilisha Humu,,Mbona Kipindi Yuko Vizuri Hakuja Msifia Humu?
 
ok, ulichokitegemea kwenye hiyo ndoa haujakipata?, fanya uamuzi mwenyewe siyo kwa ushauri wa wenginge ambao haukuwahusisha wakati mnaamua kuoana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…