Nimeombwa hela na mwanafunzi

Nimeombwa hela na mwanafunzi

Mkuu vitu vingine umapaswa uangalie mara mbili mbili mwanafunzi wa form II amekuja kugongea mlango na kukuomba hela?! Kwani yuko mbali na wazazi wake? Je hapo shuleni kwao hadi unapokaa kuna umbali gani? Kituo cha polisi kipo umbali gani? Je ni mkoa gani? Nilisahau je ana wazazi au hana?
 
Kuomba siyo dhambi...na siyo kosa...kwa sababu hitaji lake la wakat huo nikula..

Mwez uliopita nikiwa ninatokea dodoma,nikasimama njian mitaa ya gairo hivi katika maeneo yale wanaouza mafuta yakupikia njian..nikanunua mafuta kwa binti(yupo kidato cha kwanza)..nilivyomaliza kumlipa wakat nataka kuondoka akaniambia
"Baba samahani naomba peni(kalamu)"..nikamuuliza kwa ajili ya nini?akasema kwa ajili ya shule.

Aisee nilijikuta ninapata furaha ya ajabu sana,kumbe kuna watoto ambao wanaweza hitaji ndoano na siyo samaki.

Nilimpatia hela akanunue box zima la kalamu.

Lakini njia nzima ilikuwa ni story ya aina yake tuliokuwa ndan ya gari..kwa hiyo ninafikiri kuwa bado kuna watoto wadogo wanaohotaji mambo ya msingi..tuwasaidie pale unapokuwa na uwezo na wakihitaji.
 
Babu seya kawala sana hao tena wa shule za msingi sasa hivi yupo mitaani na ikulu kafika Kwa sababu ya kuwala ,wewe na mm hata mlango wa ikulu atujauingia licha ya kutokuwatafuna hao watoto
 
natamani hii coment aisome Juma Kapuya then uone GUTUSI atalokutukana
Kwa miaka 35 mtoto wa form 2 ni mwanao kabisa, amekuchukulia kama baba yake na hauna madhara tena kwake.
Tembea kifua mbele kwa kupata heshima unayostahili.
Ungekuwa baharia wa miaka 21 asingethubutu.
 
Acha kukaza ubongo mkuu. Iyo ni tabia mbaya kwa mtoto wa kike kuombaomba ela wanaume
Kweli ni tabia mbaya, lakini muombwaji hapaswi kuendeleza tabia mbaya. Mpe kama unayo Kama huna usimpe. Mwache aende akijitafakari
 
Habarini!
Kuna jambo limenitokea, linanipa maswali na mshangao kiasi.

Ninakaa jirani na shule, jirani sana tu. Ni mtu mzima mimi.......35 yrs. Kwa sasa shule nyingi zipo ktk makambi kwa vidato vya 2 na 4, hii ni mojawapo pia.

Jioni ya leo, nikiwa sina hili wala lile nimepumzika tu nasikia hodi ikigongwa. Nilipomruhusu aingie bs alikuwa n mwanafunzi flan wa kidato cha pili.......aliamkia na kisha akaniomba tshs 500/=. Nilipigwa na bumbuazi kupita maelezo lkn nikajifanya sina nilichokishangaa. Nikamuuliza unataka kununua nn akajibu anataka kununua samaki alie ugali (akilini nilitegemea nisikie peni au daftari). Nikampa tshs. 2000/=. Aliipokea haraka, akashukuru kisha huyo haraka akaondoka.

Bandugu, tangu muda huo nimetafakari mara kutafakari ujadiri wa huyo binti bado sijapata majibu mpaka nimemua nifanye sharing nanyi kisa hiki.....
wapo wanafunzi wa dizain hiyo..mimi wakati nipo form 1 nilikua na rafiki angu alikuaga anakula ela yote shule alafu mda wa kuondoka anamuomba mtu yoyote atakaemuona mladi ni mwanaume ata akute mkaka amepaki bajaji anamsogelea anamuomba ata mia tatu yaan tulikua tunamshangaa sana.
 
Inakuaje mtoto wa kike anakosa balance huko kambi!!! Leo kakutana na mmungwana mwingine asiekua na utu c atataka malipo ya ngono hapo kumbukeni binti wa form two anafaa vizuri tu katika ngono. Na wazazi waishi kwa amani hipi ilihali binti yao anapitia hali kama hizo.
Jf acheni unafki hilo swala ni lakushangaza sana!!!!
 
watu mna vichwa vigumu sana..mimi nimemuelewa mkuu vzuri sana na nipo upande wake mtoto mwenye malezi mazuri ya baba na mama anaanzaje kwenda tuu kwa mtu kuomba ela tena mtu asiemjua? daaah ndo hao wanapewa na lifti kwenye noah wanaingia afu mkiwakuta wanaelea baharini mna.....
 
Huenda alichoka kula Maharage huku anatamani kula Samaki akaona akuombe lakini siyo tabia nzuri kwa namna moja au nyingine.
 
Ndio anaweza akawa na shida lakin je huyo anaemuomba huo msaada!!! Leo amekutana na muungwana lakin uungwana unakikomoa, binti ameji-expose katika mazingira ya kuliwa kingono
 
Angalia isije kuwa mtego ukajiingiza mwenyewe kwenye mtego
 
watu mna vichwa vigumu sana..mimi nimemuelewa mkuu vzuri sana na nipo upande wake mtoto mwenye malezi mazuri ya baba na mama anaanzaje kwenda tuu kwa mtu kuomba ela tena mtu asiemjua? daaah ndo hao wanapewa na lifti kwenye noah wanaingia afu mkiwakuta wanaelea baharini mna.....
Wazungu jambo la kwanza kufundisha watoto wao ni kutozoea "stranger" yoyote hata kumchekea kumuomba kumsalamia nk....sisi eti kila mtu mzima mwenye umri wa baba ako au mama ni mzazi wako eti muite uncle au aunt....madhara yake mabaya sana culture mbaya sana hiyo
 
Back
Top Bottom