Mwanaume hawezi kuandika uquma kama wako jiandae kuwa chakula
Kwa hiyo uanaume ni kutukana watu hovyo na kuita binadamu wenzako nguruwe kisa kutofautiana mawazo kama unavyo fanya ww?
Mnapenda kutukana wenzenu wakati hamna vifua vya kuhimili mapigano.
 
...afu clip imekatwakatwa vipande.

Aya mambo ya vita + hizi media Acha kabisa...

Anyway vita ni vita haichagui wapi pa kupiga na yupi.....imesomba vitoto,vizee,wagonjwa na vijana wengi uko Palestina
Duh!imekatwa vipande gani pale!?
 
Ukiwambia haya wanakataa
Hamas waendelee kupambana haki haiombwi inapambaniwa
 
Kwema humu,

Hivi karibuni imesambaa video kwenye mitandao inayosemekana ni ya Mtanzania Joshua Mollel akiuwawa na Kundi la Hamas. Sina uhakika na authentication ya video hiyo lakini vyovyote iwavyo kutoa uhai wa binadamu ni jambo la kulaani na kukemea Kwa nguvu zote bila kujali dini, utaifa au chochote kile kinachotofautisha Binadamu mmoja na mwengine.

Kama wale ni Hamas kweli basi wanapaswa kukemewa na kulaaniwa Kwa nguvu kubwa. Hakuna justification yoyote ya kile walochokifanya. Hata kama wako katika vita lakini Joshua Kwa utambulisho wake wa kawaida (Mwanafunzi) sio sehemu ya vita hiyo.

Lakini pia nguvu hizi hizi tunazotumia kuilaani na kuikemea Hamas Kwa walochokifanya tuitumie pia kuikemea na kuilaani Israel Kwa wanachofanya pia. Israel inaua Watoto na Wamama wa Ki Palestine kupitia maroketi na mabomu yao yasisyo na macho.

Embu bas kama kweli sisi ni waungwana tukemee na hili pia. Tumeanzisha nyuzi kadhaa (za kufanana) juu ya Kifo Cha Ndugu yetu Joshua (RIP) lakini katika sisi waanzisha nyuzi hakuna hata mmoja kati yetu aliewahi kuanzisha uzi kuhusu upande wa pili.

Ni kama vile Israel anavyoua Watoto na Wamama wa Ki Palestine hatuoni kama ni tatizo ila tu sababu Mtanzania mwenzetu ameuwawa ndio tunalipuka.

Labda niulize au tujiulize tu, ukitafuta idadi ya watu waliouliwa na Hamas ukalinganisha na Idadi ya waliouliwa na Mabomu ya Israel unadhani wapi wanaweza kua wengi?

Tuikemee na tuilaani Israel aame way as tunavyoilaani Hamas.
 
Imekuuma sana Hamas kuonekana kuwa huua makusudi.

Mwanzoni imekuwa ikisemwa kuwa Hamas hawana baya.

"Video kwenye mitandao inayosemekana ni ya mtanzania..."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…