Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Watanzania hatukuwa na Rais bali kutokana na ajali ya kisiasa ya mwaka 2015 tulipata Shetani aliyejifanya anajuwa kila kitu.Inavyoonekana katika siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii, wakipost picha za hayati Magufuli na kuambatanisha na jumbe za kumkumbuka na wakati mwingine emoji za majonzi au moyo kuchanika.
Hii ikanifanya nijiulize, mbona viongozi wengine hufa na akisha kufa mnaishia kuomboleza na kusahau!?
Ndipo likanifanyi nihisi kwamba zipo sababu mseto za watu kumkumbuka huyu kiongozi ambazo ni kuondolewa machinga, bei za bidhaa kupanda hovyo, kutomkubali mrithi wake, kutoridhishwa na uendelezaji wa miradi aliyoisimamia na kurudishwa madarakani watu aliowatumbua.
Bado kuna Watanzania wapumbavu wengi tu ambao wanamsifia na ndiyo hao wanalazimisha hiyo legacy. Legacy haijadiliwi inakuja yenyewe.
Kwa kweli sioni cha kukaa na kumsifia Magufuli ambaye ameturudisha nyuma miaka 20 kiuchumi.
Lakini tumshukuru Mungu analipenda Taifa letu, alipomuona anapata kiburi na kutaka kubadili ukomo wa utawala akamtupilia Jehanam.