Nimeona post za kumkumbuka Magufuli zimeongezeka sana mitandaoni. Je, sababu ndiyo hii ninayohisi mimi?

Nimeona post za kumkumbuka Magufuli zimeongezeka sana mitandaoni. Je, sababu ndiyo hii ninayohisi mimi?

Inavyoonekana katika siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii, wakipost picha za hayati Magufuli na kuambatanisha na jumbe za kumkumbuka na wakati mwingine emoji za majonzi au moyo kuchanika.

Hii ikanifanya nijiulize, mbona viongozi wengine hufa na akisha kufa mnaishia kuomboleza na kusahau!?

Ndipo likanifanyi nihisi kwamba zipo sababu mseto za watu kumkumbuka huyu kiongozi ambazo ni kuondolewa machinga, bei za bidhaa kupanda hovyo, kutomkubali mrithi wake, kutoridhishwa na uendelezaji wa miradi aliyoisimamia na kurudishwa madarakani watu aliowatumbua.
Hiyo cha mtoto mbona.

2025 uchaguzi na Magufuli na wapinga magufuli.

Atakae cheza karata za Magufuli anaingia ikulu asubuhi tu.
 
Watu wa JF huwa mnaishi wapi mnapatikana wapi mbona mnaexperience tofaut na mitaa hamjui kama misosi kwa mama ntilie imepanda wali ni buku jero kwa elfu mbili hamjui kama dawa za meno zmepanda? Muda mwngine nashangaa siasa znapo watch akili zenu great thinkers

Sent from my SM-G960U1 using JamiiForums mobile app
Vitu vimepanda bei Kwa sababu pesa ipo mtaani.

Wakati wa jiwe vitu vilikuwa bei chee Kwa sababu hela haikuwepo na vyuma vilikaza.

Wakati huu vitu bei juu ila hela ya kununua ipo.

Kariakoo sasahivi biashara ni kama zamani.
 
Inavyoonekana katika siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu mbalimbali katika mitandao ya kijamii, wakipost picha za hayati Magufuli na kuambatanisha na jumbe za kumkumbuka na wakati mwingine emoji za majonzi au moyo kuchanika.

Hii ikanifanya nijiulize, mbona viongozi wengine hufa na akisha kufa mnaishia kuomboleza na kusahau!?

Ndipo likanifanyi nihisi kwamba zipo sababu mseto za watu kumkumbuka huyu kiongozi ambazo ni kuondolewa machinga, bei za bidhaa kupanda hovyo, kutomkubali mrithi wake, kutoridhishwa na uendelezaji wa miradi aliyoisimamia na kurudishwa madarakani watu aliowatumbua.
Basi mimi nitakuwa nina upungufu fulani.
 
JamiiForums1952969871.jpg
 
Aendelee kulala salama kipenzi chetu

Tuna kazi kubwa ya kutimiza wajibu kwa kuyaenzi mema yake na kuendelea kuliombea taifa letu ili kazi iendelee

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan
Amen
 
Back
Top Bottom